- Wachezaji wa Simba SC watakao achwa msimu wa 2025/26 ni wale ambao hawakuwa na nafasi kubwa kuanza kikosi cha kwanza katika mechi za ushindani.
- Che Malone beki wa kati anatajwa kuwa kwenye uangalizi mkubwa ndani ya kikosi cha Simba SC kuelekea msimu mpya wa 2025/26.
- Aishi Manula nafasi yake kubaki inatajwa kuwa finyu na anatajariwa kusaini kwa matajiri wa Dar, Azam FC.
- Hussen Kazi, atajipata nje ya Simba SC kwa kuwa hajawa chaguo la kwanza kwenye mechi za ushindani.
Simba SC huenda ikawapa Thank You nyota zaidi ya watano kuelekea maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26 ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Sababu kubwa za kuachana na nyota hao ni kuporomoka kwa viwango, mikataba ya nyota hao kutarajiwa kufika tamati, wachezaji kupata timu mpya na nyingine zilizopo kimkataba. Wapo nyota wegine ambao watapewa kwaheri na Simba SC kutokana na kupata changamoto mpya kwenye timu nyingine ambazo zinahitaji huduma zao kwa ajili ya kuwa nao katika timu zao. Hivyo ni jambo la kusubiri na kuona.

Ni Aziz Ki wa Yanga tayari amepewa Thank You. Hapa tunakuletea baadhi ya nyota waliopo ndani ya kikosi cha Simba SC ambao tetesi zinaeleza kuwa huenda wakakutana na Thank You na wengine kupewa angalizo zaidi namna hii:-
Aishi Manula ni mmoja ya wachezaji wa Simba SC wanaotajwa kuachwa msimu wa 2025/26

Kipa namba tatu wa Simba SC, Aishi Manula mkataba wake unagota mwisho msimu utakapoisha kwa kuwa aliongeza mpaka 2025. Hajawa na nafasi kikosi cha kwanza msimu wa 2024/25 jambo linalotoa picha kwamba huenda akaondoka mazima.
Matajiri wa Dar, Azam FC timu ambayo alicheza hapo kabla ya kuibukia ndani ya kikosi cha Simba SC inatajwa kuwa itamchukua kipa huyo kwa ajili ya kuanza kupata changamoto mpya msimu wa 2025/26. Kwenye dirisha dogo Azam FC walionyesha nia ya kuhitaji saini yake ila mabosi wa Simba SC wanatajwa kuwa waligomea dili hilo.
Soma hii: Simba SC 1-0 Singida Black Stars 28 Mei 2025: Matokeo, magoli, wafungaji, h2h, Kifuatacho Kariakoo Dabi

Hussen Kazi beki wa kazi
Beki huyu wa kati ambaye ni mzawa hajawa na nafasi katika kikosi cha Simba SC ndani ya msimu wa 2024/25 jambo ambalo linatoa picha kuwa huenda akakutana na mkono wa Thank You mazima kwa ajili yakutafuta changamoto mpya.
Ally Salim kipa namba mbili wa Simba SC
Kipa huyu msimu wa 2024/25 kwenye ligi ni mechi mbili pekee alipata nafasi yakucheza kati ya 27 ambazo Simba SC imecheza.Chaguo la kwanza ni Moussa Camara ambaye amekaa langoni kwenye mechi 25.
Katika dakika 180 ambazo Ally Salim alikaa langoni kwenye ligi hajafungwa akiwa na hati safi mbili. Kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Singida Black Stars uliochezwa Mei 31 2025 aliingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Camara ambaye alipata maumivu.
Ally Salim wakati anaingia tayari Camara alikuwa ametunguliwa mabao mawili, alifanya kosa moja kwenye kutoa pasi iliyokutana na Emmanuel Kayeke ambaye alifunga bao la pili, kiungo huyo alifunga bao la tatu kwa pigo la faulo akiwa nje kidogo ya 18. Huenda Ally akatolewa kwa mkopo ikiwa hataongeza umakini.
Che Malone kwenye uangalizi

Beki wa kikosi cha Simba SC ambaye ni mfungaji wa bao la kwanza kwenye ligi msimu wa 2024/25 Che Malone huyu anatajwa kuwa kwenye uangalizi katika mechi za mwisho zilizobaki kuongezewa mkataba ama kupewa mkono wa Thank You.
Soma hii: Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC anatajwa Raja Casablanca, Maxi, Farid Mussa kuondoka
Che Malone ikumbukwe kwamba alifungua ukurasa wa mabao kwenye mchezo wa kwanza wa Simba SC msimu wa 2024/25 uliochezwa Uwanja wa KMC Complex. Bao hilo alifunga dhidi ya Tabora United kwa pigo la kichwa ilikuwa ni Agosti 18 2024.
Sababu kubwa ambazo zinafanya beki huyo awe kwenye uangalizi mkubwa ni kutokuwa kwenye mwendelezo wa ubora kwenye mechi ambazo anapata nafasi kucheza kitaifa na kimataifa. Ikumbukwe kwamba Simba SC kwenye mbio za kuwania kutwaa taji la CRDB Federation Cup imegotea hatua ya nusu fainali.
Katika mchezo wa funga Mei dhidi ya Singida Black Stars, Mei 31 2025 aliruhusu bao mbele ya Jonathan Sowah jambo ambalo limezua gumzo kutokana na kushindwa kuwa katika uimara hivyo anatazamwa kwa ukaribu na mabosi wa timu hiyo.
Edwin Balua wa Simba SC anatajwa Mbeya City
Kiungo wa kazi ndani ya kikosi cha Simba SC, Edwin Balua anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaopewa Thank You. Wakati akitajwa kuwa ataondoka ndani ya kikosi cha Simba SC Mbeya City inatajwa kuwania saini yake.

Balua ambaye alisajiliwa na Simba SC akitokea ndani ya kikosi cha Tanzania Prisons msimu wa 2024/25 hajawa na nafasi kikosi cha kwanza. Nyota huyo mechi nyingi za ligi amekuwa akianzia benchi. Chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids rekodi zinaonyesha kuwa hajacheza mechi zaidi ya 15 kwenye ligi kati ya 27 ambazo zimechezwa na kikosi cha Simba SC kilicho nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi 72.
Soma hii: Yanga SC vs Simba SC deni la watani kubwa eneo la ushambuliaji, Kariakoo Dabi mmoja alipotezwa
Balua ni mechi 10 kapata nafasi ya kucheza ndani ya ligi akikomba dakika 332 jambo ambalo linaonyesha kuwa sio chaguo la kwanza ndani ya benchi la ufundi la Simba SC. Hivyo kuna nafasi ndogo kwake kubaki ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao.
Simba SC ikiwa imetupia mabao 63 kiungo huyo kahusika kweye mabao mawili ambayo yote alifunga akiwa hajatengeneza nafasi ya pasi ya bao kwa wachezaji wengine. Kinara wa utupiaji ndani ya Simba SC ni Jean Ahoua ambaye amefunga jumla ya mabao 15
Taarifa zinaeleza kuwa kiungo huyo Edwin Balua huenda akapewa mkono wa Thank You kupisha usajili wa nyota wengine ndani ya kikosi hicho kilichogotea nafasi ya pili kwenye Kombe la Shirikisho Afrika huku mabingwa wakiwa ni RS Berkane.
Bado Simba SC hawajatoa taarifa rasmi kuhusu wachezaji waliopo katika kikosi hicho ambacho kinashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo yanayoendelea kwa sasa ni tetesi kwa kuwa msimu unakaribia kuisha na wapo wachezaji ambao mikataba yao inakaribia kufika ukingoni.

