Ratiba ya mechi za YangaRatiba ya mechi za Yanga
  • Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali ya CRDB ni kilele cha mashindano ya Kombe la Shirikisho maarufu (FA) kwa msimu 2024/25.
  • Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa Desemba 29, 2024 na Singida kukubali kipigo cha mabao 5-0
  • Fainali inatarajiwa kupigwa kupigwa siku ya Juni 28, 2025 kwenye Uwanja wa Amaan.

Hatimaye msimu wa ligi unaelekea ukingoni kwa mashindano mbalimbali, huku  mchezo wa Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali ya CRDB ndio mchezo wa kukata na shoka unaotupiwa jicho na wadau wa soka, kujua nani atakuwa mfalme mpya kwa kushinda ubingwa wa mashindano hayo..

Yanga SC vs Singida Black Stars kupigwa Zanzibar

Uwanja wa New Amaan Complex
Uwanja wa New Amaan Complex

Imeelezwa kuwa upo uwezekano mkubwa wa mchezo huu wa fainali kuchezwa visiwani Zanzibar, ambapo inatarajiwa mchezo huo kupigwa siku ya Juni 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Amaan.

Mchezo huu wa fainali katika msimu wa 2024/2025 unatarajiwa kuwa kivumbi cha soka, ambapo timu hizi mbili zitapigania taji la pili kwa ukubwa, thamani na umuhimu nchini Tanzania huku timu hizo zikitajwa kuwa na vikosi bora.

SOMA HII PIA: Yanga SC vs Simba SC Juni 15 2025 Dabi ya Kariakoo mechi ipo, au haipo?

Safari ya Yanga SC fainali ilikuwaje?

Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na Kombe hilo la CRDB, wameonyesha kiwango cha juu katika michuano msimu huu ambapo katika hatua ya nusu fainali, walikutana na JKT Tanzania na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Ushindi huo unaonyesha ubora wa kikosi cha Yanga chini ya kocha Miloud Hamdi, ambaye ameweza kuunda timu imara inayocheza soka la kuvutia na kushambulia kwa kasi na kuwa na wastani msuri wa kufunga mabao.

SOMA HII PIA: Dickson Job beki wa Yanga SC anatajwa Simba SC, Jean Ahoua kuondoka

Safari ya Singida Black Stars kufuzu fainali

Simba - Singida Black Stars
Simba – Singida Black Stars

Singida Black Stars ambao ni wageni katika fainali hii, walifanya maajabu katika mchezo wa nusu fainali kwa kuifunga Simba SC mabao 3-1, magoli ya Singida yalifungwa na Jonathan Sowah (17′) na  Emmanuel Keyekesh (35′ na 48′)

Ushindi huu unaonyesha uwezo mkubwa wa Singida Black Stars, ambao wamejijengea jina la kuwa timu ngumu kupambana nayo chini ya kocha wao mpya ambaye ameleta mabadiliko makubwa katika timu, akiwafanya wachezaji wake kuwa na ari na nidhamu ya hali ya juu.

Mchezo wa Fainali

Fainali ya CRDB Confederation Cup kati ya Yanga SC na Singida Black Stars inatarajiwa kuwa kivumbi cha soka kwelikweli, Yanga SC wakiwa na uzoefu mkubwa katika michuano ya kimataifa, wanatarajiwa kuwa na faida ya uwanja wa nyumbani na nguvu ya wapenzi wao wengi.

Hata hivyo, Singida Black Stars hawatakuwa na hofu yoyote, kwani wameonyesha uwezo wa kushinda dhidi ya vigogo wa soka nchini Tanzania.

Utabiri wa Matokeo

Ingawa Yanga SC wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na uzoefu wao na ubora wa kikosi chao, Singida Black Stars wameonyesha kuwa wanaweza kushinda dhidi ya timu yoyote. Hivyo mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kusisimua na wenye ushindani mkubwa.

Mashabiki wa soka nchini Tanzania wanatarajia kuona burudani ya soka safi na la kuvutia kutoka kwa timu hizi mbili, hasa kutokana na ujuzi na ufundi ambao kila upande umeonyesha msimu huu.

Kwenye ligi Yanga washikilia msimamo mzito Juni 15 2025, Dabi ya Kariakoo

Ukiachana na mchezo huo wa fainali dhidi ya Singida Juni 28, bado Yanga wameendelea kusimamia msimamo wao juu ya mchezo namba 184 kati ya Yanga vs Simba ambao umepangwa kupigwa Juni 15, mwaka huu.

Mchezo huo wa watani wa jadi maarufu kama Derby ya Kariakoo, unatarajiwa kuchezwa tena tarehe 15 Juni 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Ikumbukwe awali, mchezo huu ulipangwa kufanyika tarehe 8 Machi 2025, lakini uliahirishwa kutokana na mivutano iliyozuka kabla ya pambano hilo.

Hitimisho

Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali ya CRDB
Yanga Bingwa Muungano Cup

Fainali ya CRDB Confederation Cup kati ya Yanga SC vs Singida Black Stars ni tukio muhimu katika historia ya soka nchini Tanzania, hasa kwa msimu huu wa mashindano ambao umekuwa na mafanikio makubwa kwa timu zote mbili hususani Yanga wanaojinasibu ya kubeba makombe.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.