Fadlu MastaFadlu Masta
  • Fadlu Davids kocha wa mpira huenda akaondoka ndani ya kikosi cha Simba SC kutokana na ofa ambazo zipo mezani kutoka kwa timu kubwa Afrika zikihitaji kufanya naye kazi.
  • Yanga SC kumchomoa mkali wa mabao kutoka kwa matajiri kuwa mbadala wa kiungo Aziz Ki ambaye ameshauzwa.
  • Simba SC kuivuruga Yanga SC kwa kumchomoa kiungo tegemeo anayejua kufunga na kutengeneza pasi za mabao.

Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC anatajwa Raja Casablanca ambao wanahitaji kuipata saini yake kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho. Timu yao imekwama kufika fainali ya mashindano makubwa Afrika 2024/25. Je, wakimpata Fadlu Davids wataeza kukomoka?

Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC
Coach Fadlu wa Simba SC.

Taarifa zinaeleza kuwa kutokana na rekodi nzuri alizonazo Fadlu Davids, Raja Casablanca ya Morocco inamfuatilia kwa ukaribu kocha huyo ili kufanya naye kazi kwenye msimu ujao wa 2025/26 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kitaifa na kimataifa.

Mbali na Raja Casablanca kutajwa kuweka ofa mezani kupata huduma ya Fadlu inaelezwa kuwa Esperance De Tunis ya Tunisia nayo ipo kwenye hesabu za kutaka kumpa mkataba kocha huyo rai awa Afrika Kusini ili awa kocha katika timu yao.

Ikumbukwe kwamba timu hiyo imempa kazi kocha Maher Kanzari ilikuwa Machi 2025 bado imani yao ipo kwa Fadlu kuwa ni miongoni mwa makocha ambao wanauwezo mkubwa kuongoza timu hasa kutokana na uzoefu alionao na kujenga timu ya Simba SC iliyogotea hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa nini jina la Fadlu linaimbwa Afrika?

Jina la Fadlu limekua ghafla kutokana na mwendo wake akiwa na kikosi cha Simba SC kuwa na rekodi zinazovutia licha ya kutokuwa na wachezaji wenye majina makubwa katika timu hiyo. Simba SC ni timu ambayo ilikuwa haipewi nafasi kufika hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika na ilipofika wengi walistaajabu kutokana na matokeo iliyopata.

Ilipotinga hatua ya fainali hapo gumzo likawa kubwa kwa kuwa awali ilikuwa inatabiriwa itagotea hatua ya robo fainali kwa kuwa haikuwa na wachezaji ambao walikuwa wanatisha kwa namba uwanjani. Jean Ahoua, Ellie Mpanzu, Kibu Dennis ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa tegemeo kikosi cha kwanza na walifanya kazi kubwa kutimiza majukumu na mbinu za Fadlu mpaka timu ikatinga hatua ya fainali.

Fainali dhidi ya RS Berkane gumzo

Ngoma kimataifa
Ngoma vs RS Berkane, fainali Kombe la Shirikisho Afrika. Source: Simba SC.

Fainali ya Simba SC dhidi ya RS Berkane ilikuwa gumzo, mchezo wa kwanza ugenini Simba SC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 na fainali ya pili ikawa Simba SC 1-1 RS Berkane, Uwanja wa New Amaan Complex.

Simba SC kupoteza fainali kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya RS Berkane ni miongoni mwa mchezo uliofuatiliwa kwa ukaribu na wengi duniani jambo lililoongeza ukubwa wa kocha Fadlu. Hivyo kocha yupo kwenye hesabu za matajiri wa Afrika.

Soma hii: Simba SC 1-1 RS Berkane ya Morocco yatwaa ubingwa wa CAF Mei 25 2025

Farid Mussa anatajwa Singida Black Stars

Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Farid Mussa anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Singida Black Stars na Mbeya City ambao wanahitaji huduma yake kwa ajili ya changamoto mpya. Mbeya City imepanda daraja kwa mara nyingine hivyo inahitaji kuwa na wachezaji wenye uzoefu na ligi na mashindano ya kimataifa ili kupata matokeo mazuri.

Clement Mzize anatajwa na Zamaleki FC

Mzize kwenye jezi ya Zamalek (iliyotengenezwa)
Mzize kwenye jezi ya Zamalek (iliyotengenezwa)

Kwenye eneo la ushambuliaji Clement Mzize anafanya kazi kubwa akiwa kafunga mabao 13. Anatajwa kuwa kwenye hesabu za Zamaleki FC ya Misri. Ofa kubwa inatajwa kuwekwa na matajiri wa Zamalek ambao wanahitaji saini yake.

Soma hii: Baada ya Aziz Ki: Mzize na Aucho wanaondoka Yanga? Tetesi usajili bongo

Jonathan Sowah- Yanga SC na Simba SC

Yupo ndani ya kikosi cha Singida Black Stars Jonathan Sowah akiwa katuma jumla ya mabao 11 msimu wa 2024/25. Kwenye mabao ambayo amefunga Sowah hayo 11 alimfunga pia kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra katika mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.

Kwenye mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 2-1 Singida Black Stars, pointi tatu zilibaki kwa Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi. Anatajwa kuwa kwenye rada za Yanga SC na Simba SC. Aliwafunga Simba SC kwenye CRDB Federation Cup.

Maxi Nzengeli anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC

Maxi Nzengeli kiungo mshambuliaji wa Yanga SC anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Simba SC ambao wanahitaji saini yake kwa ajili ya kuwa naye katika kikosi hicho ambacho kimetinga hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Gibrli Sillah anatajwa Yanga SC

Sillah Gibril
Sillah Gibril kiungo wa Azam FC. Source: Azam FC.

Kiungo mshambuliaji wa Azam FC ambaye yupo kwenye viunga vya matajiri wa Dar, anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Jangwani, Yanga SC. Sillah ni mkali kwenye kufunga na kutengeneza nafasi za mabao ambapo kwa msimu wa 2024/25 kafunga mabao 9 na kutengeneza pasi mbili za mabao amekuwa akitajwa kuwa katika hesabu za Yanga SC.

Ibrahim Keita wa TP Mazembe anatajwa Yanga

Ibrahim Keita ni mlinzi wa kulia ambaye mkataba wake na timu ya TP Mazembe unakaribia kufika mwisho na inaelezwa kuwa hayupo tayari kuongeza kandarasi nyingine. Hivyo kuna uwezekano mkubwa nyota huyo akawa ndani ya ligi msimu ujao.

Singida Black Stars walianza kuulizia saini ya nyota huyo kisha Yanga SC wakafuata kuulizia ili kuinasa saini yake. Mwenye kisu kikali kuelekea kwenye dirisha la usajili atakula nyama kwa kuwa kinachoshinda katika sanaa ya usajili ni mkwanja mezani na maamuzi ya mchezaji wapi atapenda kucheza.

Share this: