RS Berkane vs Simba SCRS Berkane vs Simba SC
  • RS Berkane vs Simba SC 17/5/2025, kwa Wanasimba na Watanzania huu ni zaidi ya mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho, bali ni nafasi ya kuandika rekodi ya kubeba ubingwa wa kwanza mkubwa wa mashindano ya Afrika.
  • Mchezo wa marudiano ambao unatarajiwa kupigwa Dar es Salaam na tayari uongozi wa Simba umetangaza viingilio wa pili wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ni kama ifuatavyo; Mzunguko  Tsh. 7,000. VIP C Tsh. 20,000. VIP B Tsh. 30,000. Platinum  Tsh. 250,000.
  • Katika Fainali hii ya kihistoria itapigwa michezo miwili ambapo fainali ya kwanza inapigwa nchini Morocco Mei 17, mwaka huu huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kupigwa Mei 25, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

RS Berkane vs Simba SC 17/5/ 2025, kwa Wanasimba na Watanzania huu ni zaidi ya mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho, bali hii ni nafasi ya kusisimua kwa Watanzania kuandika rekodi ya kubeba ubingwa wa kwanza mkubwa wa mashindano ya Afrika.

Katika Fainali hii ya kihistoria itapigwa michezo miwili ambapo fainali ya kwanza inapigwa nchini Morocco Mei 17, mwaka huu huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kupigwa Mei 25, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

RS Berkane vs Simba SC 17/5/2025: Simba yatua Morocco Kibabe!

RS Berkane vs Simba SC 17 Mei 2025
Safari ya kwenda Morocco imewadia- #WenyeNchi #NguvuMoja

Kuelekea mchezo huo, kikosi cha Simba tayari kimewasili Morocco baada ya safari ya masaa 7 angani kwa Ndege ya moja kwa moja ambayo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

SOMA HII PIA: Simba SC vs Stellenbosc FC Moto utawaka Jumapili 20/04/2025, haya hapa yanatarajiwa

image

Semaji, Ahmed atoa tamko zito

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally kwa niaba ya Uongozi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia kwa kutoa Ndege ambayo imewapeleka Simba na ikitarajiwa kuwarudisha.

Hii yote ni katika kuhakikisha kikosi kinakuwa na utulivu kwenye maandalizi ya mchezo huo ambapo kikosi kitatua moja kwa moja katika Jiji la Casablanca, kabla ya kuelekea Berkane ambapo mchezo huo utapigwa.

Kauli mbiu ya mchezo ni ‘TUNABEBA’

------------------------------------------------n
Semaji, Ahmed

Ahmed ameongeza kuwa kuelekea mchezo huo wamekuja na kauli mbiu ambayo ni ‘TUNABEBA’ wakiwa na maana kuwa wamejipanga kuhakikisha wanalibakisha taji la Kombe la Shirikisho Afrika.

Ahmed ameenda mbali zaidi na kuwaomba Wanasimba kuwa wamoja na kila mtu kwa nafasi yake ahakikishe anaiwezesha timu kuchukua taji la Kombe la Shirikisho msimu huu.

“Kama kila mtu alifanya jitihada hadi timu kufika hapa ilipo, basi anatakiwa kuongeza jitihada hizo mara 100 ili kuhakikisha Simba itabakisha Kombe la Shirikisho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Berkane ni timu bora na ina historia nzuri kwenye michuano hii, lakini tumeapa kuwa hatutaki yajitokeze ya mwaka 1993 safari hii tunataka kubeba taji,” amesema Ahmed.

SOMA HII PIA: Yanga, Simba, Azam usajili ni balaa zito 2025

Mashabiki Simba wavamia tiketi za Simba SC vs RS Berkane 25 Mei 2025

RS Berkane vs Simba SC 17/5/2025
Mashabiki wa Simba na timu yao

Kuelekea mchezo wa marudiano ambao unatarajiwa kupigwa Dar es Salaam tayari uongozi wa Simba umetangaza viingilio vya mchezo, ambapo viingilio vya mchezo wa pili wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ni kama ifuatavyo;

Mzunguko – Tsh. 7,000. VIP C – Tsh. 20,000. VIP B – Tsh. 30,000. Platinum – Tsh. 250,000.

Uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa umeamua kutangaza viingilio mapema, ili kuwapa nafasi mashabiki kukata tiketi mapema na kuondoa usumbufu usio wa lazima siku ya mchezo.

“Tumedhamiria kubeba ubingwa wa michuano hii, tunahitaji sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wetu. Tunaamini furaha ya kila Mwanasimba ni kuiona timu yetu ikitwaa ubingwa wa Afrika kwahiyo tunahitaji kujitoa ili kufanikisha malengo haya,” amesema Ahmed.

Steven Mukwala aongoza jeshi la Simba kutua kibabe Morocco

Steve Mukwala v KMC FC
Steve Mukwala v KMC FC

Simba wanatua Morocco kibabe huku wakiwa na kumbukumbu nzuri ya mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu Bara, ambapo waliiadhibu KMC na kupata ushindi wa mabao 2-1 ukiongozwa na straika Mganda, Steven Mukwala.

Simba waliingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 5-1 walioupata dhidi ya Pamba, katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa siku ya Alhamisi iliyopita,

Alichosema Kocha Simba baada ya ushindi

Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola amesema pamoja na ubora walionao KMC lakini bado hawapo nafasi nzuri kwenye msimamo, hivyo walifahamu kuwa ni lazima wapambane kutafuta alama tatu.

Matola ameongeza kuwa ratiba yao ni ngumu kutokana na kucheza mechi kila baada ya siku mbili ndio maana wamekuwa tukifanya mabadiliko ya kikosi mara kwa mara.

“Nikiri tu, tuna ratiba ngumu, hatupati muda mwingi wa maandalizi lakini tuna kikosi kipana ambacho kinaweza kutuwezesha kupata ushindi popote. Tulitegemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa KMC lakini tulijipanga kupata matokeo chanya,” amesema Matola.

Ikumbukwe katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Uwanja wa KMC Complex, Novemba 6, Simba pia iliibuka na ushindi wa mabao 4-0. Mabao hayo yalifungwa na Awesu Awesu, Jean Charles Ahoua aliyefunga mawili na Edwin Balua.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.