- Barcelona vs Real Madrid El Clasico ya 261 ni zaidi ya chezo wa ligi, hii ni vita ya kisasi dhidi ya rekodi inayotarajiwa kupigwa leo Jumapili kwenye dimba la Olímpic Lluís Companys, Hispania.
- Katika michezo mitano ambayo timu hizo zimekutana hivi karibuni Barcelona wameshinda mechi 3, Real Madrid wameshinda mechi 2 hakuna sare na mara ya mwisho Barcelona waliibuka na ushindi wa mabao 3–2 Aprili 26, 2025 kwenye Fainali ya Copa del Rey.
- Kocha, Hans Flick amekuwa na mafanikio dhidi ya Ancelotti msimu huu ambapo katika michezo mitatu waliyokutana Barca imefunga jumla ya mabao 12 dhidi ya 4.
Barcelona vs Real Madrid El Clasico ya 261 ni mchezo wa vita ya kisasi dhidi ya rekodi ambao unatarajiwa kupigwa leo Jumapili kwenye dimba la Olímpic Lluís Companys, Hispania.
Barcelona wataikaribisha Real Madrid katika El Clásico ya nne na ya mwisho msimu huu, mechi ambayo inatarajiwa kutoa taswira ya ubingwa wa La Liga msimu huu zikiwa zimesalia mechi tatu za mwisho za ligi kuu ya Hispania.
Mpaka sasa msimamo unasemaje?
Mpaka sasa kwenye msimamo wa La Liga ni pointi nne tu, ndizo zinawatenganisha mahasimu hawa kwenye mbio za ubingwa, huku Barça wakiwa juu kwenye msimamo na rekodi ya kutopoteza mechi 15 mfululizo za ligi tangu kuanza mwaka huu.
Real Madrid ambao walipoteza nafasi ya uongozi wa ligi mnamo mwezi Februari, wameendelea kuifukuzia Barça, ambapo kila timu imefanikiwa kushinda mechi zake nne za mwisho za ligi.
Rekodi zao msimu huu, Barcelona ni mfupa mgumu kwa Real Madrid

Barcelona wameitawala Real Madrid msimu huu, wakifanikiwa kuibuka na ushindi katika michezo mitatu ambayo wamekutana katika mashindano mbalimbali hadi sasa ikiwa ni pamoja na fainali za Super Cup ya Hispania na Copa del Rey.
Hata hivyo, Barcelona wanaingia katika mechi hii wakiwa na majeraha ya kihisia baada ya kutolewa kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hali ambayo Madrid wanaweza kuitumia kama faida ili kushinda Clásico muhimu zaidi msimu huu.
SOMA HII PIA: Inter Milan Vs FC Barcelona ‘live’: Vikosi, uchambuzi, utabiri
Dondoo muhimu kuhusu Barcelona vs Real Madrid El Classico ya 261

Mechi: Barcelona dhidi ya Real Madrid
Mahali: Barcelona, Hispania
Uwanja: Estadi Olímpic Lluís Companys
Tarehe: Jumapili, Mei 11
Rekodi ya Mechi Tano za Hivi Karibuni (Head-to-Head)
Katika michezo mitano ambayo timu hizo zimekutana hivi karibuni Barcelona wameshinda mechi 3, Real Madrid wameshinda mechi 2 na hakuna sare, huku walipokutana mara ya mwisho Barcelona waliibuka na ushindi wa mabao 3–2 Aprili 26, 2025 kwenye Fainali ya Copa del Rey.
Fomu ya hivi karibuni (Mashindano Yote)
Barcelona
Inter Milan 4–3 Barcelona 5/6/25
Real Valladolid 1–2 Barcelona 4/3/25
Barcelona 3–3 Inter Milan 4/30/25
Barcelona 3–2 Real Madrid 4/26/25
Barcelona 1–0 Mallorca 4/22/25
Real Madrid
Real Madrid 3–2 Celta Vigo 5/4/25
Barcelona 3–2 Real Madrid 4/26/25
Getafe 0–1 Real Madrid 4/23/25
Real Madrid 1–0 Athletic Bilbao 4/20/25
Real Madrid 1–2 Arsenal 4/16/25
Habari za Kikosi cha Barcelona

Jules Koundé anaweza kuwa mchezaji pekee muhimu anayetarajiwa kukosekana huku Robert Lewandowski akirudi uwanjani baada ya kuwakosa Inter, Alejandro Balde pamoja na Marc Casadó pia wakirudi mazoezini japo huenda bado mapema kwao kucheza.
Swali kubwa ni nani ataanza golini hasa baada ya kipa, Ter Stegen kurudi kutoka kwenye majeraha na alianza mechi ya mwisho ya La Liga, lakini Flick anaweza kuchagua kumchezesha Wojciech Szczęsny aliyekuwa golini dhidi ya Inter.
Gerard Martín na Eric García walionyesha kiwango kizuri dhidi ya Inter na wanatarajiwa kuanza tena. Pau Cubarsí na Iñigo Martínez watakamilisha safu ya ulinzi.
Katika ushambuliaji, Dani Olmo anaweza kuanza mbele ya Fermín López. Raphinha na Lamine Yamal wanahitaji ushindi wa La Liga ili kuendeleza ndoto zao za Ballon d’Or.
Kikosi kinachotarajiwa cha Barcelona
Szczęsny; Eric, Cubarsí, Martínez, Martín; de Jong, Pedri; Yamal, Olmo, Raphinha; Lewandowski.
Mfumo unaotarajiwa kwa Barcelona ni 4-2-3-1.
SOMA HII PIA: Real Madrid 3-2 Celta Vigo: Mbappe airudisha Madrid kwenye mbio za ubingwa
Habari za Kikosi cha Real Madrid

Madrid inaendelea kupambana na janga la majeraha mengi msimu huu na wataenda Barcelona bila walinzi muhimu kama David Alaba, Éder Militão, Dani Carvajal, Ferland Mendy, na Antonio Rüdiger.
Eduardo Camavinga, ambaye mara kadhaa amecheza kama beki, naye pia hayupo kutokana na jeraha. Hii inamlazimu Tchouaméni kucheza kama beki wa kati sambamba na Raul Asencio.
Katika ushambuliaji, Rodrygo anaweza kurudi upande wa kulia, isipokuwa kama Arda Güler ataendelea kupewa nafasi kwa mechi ya tatu mfululizo.
Kikosi kinachotarajiwa cha Real Madrid
Courtois, Vázquez, Tchouaméni, Asencio, García; Valverde, Ceballos; Rodrygo, Bellingham, Vinícius; Mbappé
Mfumo tarajiwa ni 4-2-3-1
Utabiri wa Matokeo: Barcelona vs Real Madrid Barcelona vs Real Madrid El Classico ya 261
Barcelona wanaweza kuwa na uchovu kutokana na ratiba ngumu ya wiki za karibuni, jambo ambalo safu ya ushambuliaji ya Madrid itajaribu kulitumia.
Lakini, Flick amekuwa na mafanikio dhidi ya Ancelotti msimu huu kwa ushindi wa jumla wa mabao 12–4 katika mechi zote walizokutana. Kwa kuwa ushindi unaweza kuwapatia taji, Barcelona watapambana hadi mwisho na kutumia udhaifu wa Madrid iliyojaa majeruhi.
Kutokana na hali hiyo utabiri: Barcelona 3–1 Real Madrid

