- Man United 4-1 Athletic Club Europa League, ilikuwa stori ya kutisha kwa Athletic Club, huku kwa Man United ni ukamilifu wa ndoto ya kutinga Fainali.
- Fainali ya Europa 2024/25 ni vita ya Waingereza ambapo Spurs wametinga fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1, huku United wao wakiicharaza Athletic 7-1.
- Fainali ya Tottenham vs United itapigwa Jumatano 21, Mei 2025. katika Uwanja wa San Mamés huko Bilbao.
Man United 4-1 Athletic Club Europa League, ni stori ya kutisha kwa Athletic Club, huku kwa upande wa mashabiki wa Man United ni ukamilifu wa ndoto yao ya kutinga Fainali. Ushindi wa jumla wa mabao 7-1 katika michezo miwili umewafanya Mashetani wekundu watinge Fainali kwa kishindo kikubwa na kutuma ujumbe mzito kwa Tottenham Hotspurs watakapovaana fainali.
Fainali Europa League 2024/25 ni vita ya Waingereza.

Kwa mara nyingine Waingereza wamefanikiwa kuingiza timu mbili katika hatua ya fainali ya mashindano makubwa ya Ulaya. Spurs na Manchester United katika fainali huku klabu zote mbili zikitaka kumaliza kwa kishindo msimu ambao ulikuwa mbaya kwao.
Spurs wanatafuta kombe lao la kwanza tangu 2008 na wanajaribu kutimiza ahadi ya, Ange Postecoglou ya kuleta tena mafanikio katika msimu wake wa pili na klabu hiyo.
Tayari tetesi za soka England zimethibitisha kuwa kocha huyo ataondoka mwishoni mwa msimu hata kama atashinda ubingwa huo. Mwenendo mbaya wa kikosi chake ikiwa sababu kubwa ambapo mpaka sasa wanakamatia nafasi ya 16 kwenye Ligi Kuu ya England.
SOMA HII PIA: Athletic Club Vs Man United 1/5/2025: Vikosi, uchambuzi, utabiri
Ni fainali ya mabao Bilbao

Spurs walicheza kwa ustadi katika mechi ya pili ugenini na kuwashinda Bodo/Glimt jumla ya mabao 5-1 na kufuzu safari ya fainali itakayopigwa Bilbao.
United ambao wamefuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 7-1 pia kwa upande wao hali yao kwenye ligi ni dhoofu ambapo wako nafasi ya 15 katika jedwali na wanahitaji kushinda mashindano haya ili kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Kikosi cha, Ruben Amorim kilishinda kwa urahisi 3-0 dhidi ya Athletic Bilbao nchini Hispania katika mechi ya kwanza, kabla ya kuanza kwa hofu kwenye uwanja wa Old Trafford.
Hata hivyo, United walikuja juu kipindi cha pili na kushinda jumla ya mabao 7-1 na kuweka jukwaa la fainali ya timu mbili kutoka Ligi Kuu ya England.
Dondoo muhimu kuhusu Fainali

Mechi ya wababe hao imepangwa kuanza saa 3 usiku kwa saa za Uingereza (BST), siku ya Jumatano tarehe 21 Mei 2025.
Mchezo utachezwa katika Uwanja wa San Mamés huko Bilbao.
Mastaa, Mason Mount, Romero na Solanke ndio walioteka vichwa vya Habari katika michezo ya nusu fainali na kuzisaidia timu hizo za England.
SOMA HII PIA: ‘Manchester Derby’ ni Man United vs Man City kinapigwa leo Jumapili
Habari za vikosi vya Tottenham na Man United
Kuelekea mchezo huo hofu imezidi kwenye kambi ya Spurs na hii ni baada ya kutoka kwa taarifa kuwa kiungo, James Maddison huenda akakosekana baada ya kuumia goti na huenda akawa ameumaliza msimu.
Lucas Bergvall pia anatarajiwa kukosa mechi zote zilizobaki kutokana na jeraha la kifundo cha mguu. Spurs wanatumaini kupata tena huduma ya nahodha wao Heung-min Son, ambaye amekuwa nje kwa mwezi mmoja kwa jeraha la mguu.
Kwa upande wa Man United, Diogo Dalot anapambana kurejea kutoka kwenye jeraha la mguu, lakini Matthijs de Ligt anatarajiwa kuwa amepona jeraha la goti kwa wakati.
Amorim hata hivyo ataendelea kumkosa Joshua Zirkzee na Lisandro Martinez.
Utabiri wa Tottenham vs Man United:

Ni vigumu kutabiri matokeo kutoka kwa klabu hizi mbili, ambazo zimekuwa na msimu mbovu, japo zimefanikiwa kufuzu katika hatua kubwa ya fainali.
Spurs wameshinda mechi zote tatu dhidi ya United msimu huu na hawajafungwa na United tangu Oktoba 2022.
Hata hivyo, kikosi cha Amorim kimekuwa dhabiti katika mechi kubwa, kikichukua pointi dhidi ya Arsenal, Liverpool na Manchester City, na huenda wakaaminika zaidi katika fainali hii yenye presha kubwa.
Utabiri: Man United kushinda 2-1.
SOMA HII PIA: North London Derby: Tottenham vs Arsenal – A Clash to Remember
Rekodi mechi ya Tottenham vs Man United:
Baada ya Man United 4-1 Athletic Club Europa League ‘live’ Hii itakuwa mara ya kwanza kwa klabu hizi mbili kukutana katika mashindano ya Ulaya, tangu ushindi wa jumla wa mabao 4-3 wa Manchester United katika Kombe la Washindi la Ulaya mwaka 1963.
Katika historia yao Spurs na United wamekutana katika michezo 204 ambapo Spurs wameibuka na ushindi katika michezo 57, sare 51 huku United wakifanikiwa kushinda michezo 96.

