Jean Ahoua (-)Jean Ahoua (-)
  • Stellenbosch FC ilichapwa bao 5-0 kwenye anga la kimataifa ugenini.
  • Simba SC kwenye mechi 5 zakimataifa ilichapwa moja ugenini ndani ya dakika 450.
  • Jean Ahoua na kigugumizi cha mguu kwenye jambo zito dakika 90.

Stellenbosch FC vs Simba nusu fainali ya wababe wawili inatarajiwa kuchezwa Aprili 27 2025 nchini Afrika Kusini kusaka mshindi atakayetinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, (CAF)

Ahoua v Stellenbosch FC
Ellie Mpanzu wa Simba SC kwenye mchezo dhidi ya Stellenbosch FC, nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika.Source: Simba SC.

Aprili 20 2025 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya nusu fainali uliochezwa Uwanja wa Amaan baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 1-0 Stellenbosch FC ya Afrika Kusini ikiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya fainali

Bao pekee la ushindi kwenye mchezo huo uliokamilisha dakika 90 za mwanzo lilifungwa na Jean Ahoua kwa pigo la faulo akiwa nje ya 18 kwa mguu wa kulia dakika ya 44 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.

Simba itakuwa ugenini kukabiliana Stellenbosch FC ambayo iliwafungashia virago Zamalek kwenye hatua ya robo fainali kwa ushindi wa jumla ya bao 1-0 ambalo walifunga wakiwa ugenini.

TANO ZA STELLENBOSCH FC

Januari 12 2025 ilikuwa Stellenbosch FC 2-0 Stade Malien de Bama, Januari 19 2025, Berkane 5-0 Stellenbosch FC hizi ilikuwa ni hatua ya makundi.

Robo fainali ya kwanza ilikuwa Aprili 2 2025, Stellenbosch FC 0-0 Zamalek na robo fainali ya pili ilikuwa Zamalek 0-1 Stellenbosch FC, Aprili 9 2025.

Stellenbosch FC kete yake ya tano ilikuwa ni nusu fainali ya kwanza ikiwa Uwanja wa Amaan ilipoteza kwa kushuhudia ubao ukisoma Simba 1-0 Stellenbosch FC.

MECHI TANO ZA SIMBA

Januari 12 2025 ilikuwa Bravos 1-1 Simba SC mchezo huu Simba SC ilikuwa ugenini katika hatua ya makundi ilivuna pointi moja, Simba SC 2-0 Constantine mchezo huu Simba Iilikuwa nyumbani Uwanja wa Mkapa ilikomba pointi zote tatu ilikuwa Januari 19 2025.

Kibu v Stellenbosch FC
Kibu Dennis kiungo mshambuliaji wa Simba dhidi Stellenbosch FC nusu fainali ya kwanza. Source: Simba SC.

Kwenye mechi mbili za hatua ya robo fainali, Simba SC ilianzia ugenini nchini Misri ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Al Masry ilikuwa Aprili 2 2025  Simba ikipoteza ugenini mazima.

Ngoma ilipochezwa Uwanja wa Mkapa Aprili 9 2025 ilikuwa Simba SC 2-0 Al Masry na Simba SC ilipenya kwa ushindi wa penati 4-1 ambapo Moussa Camara kipa namba moja wa Simba aliokoa penati mbili kwenye mchezo huo na Simba ikatinga hatua ya nusu fainali.

KETE YA TANO NUSU FAINALI YA KWANZA

Kete ya tano kwa Simba ilikuwa ni nusu fainali ya kwanza ikiwa Uwanja wa Amaan ilipoibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao ambao wanatarajiwa kumenyana nao kwenye nusu fainali ya pili Aprili 27 nchini Afrika Kusini ambao ni Stellenbosch FC.

REKODI ZA NUSU FAINALI YA KWANZA

Kwenye mchezo wa Aprili 20 2025 kulikuwa na matumizi makubwa ya nguvu na faulo ambapo miongoni mwa wachezaji ambao walichezewa faulo kwa Simba SC ni Kibu Dennis, Ellie Mpanzu na Jean Ahoua.

RS Berkane Simba SC CS Constantine Stellenbosch FCThe ------- #TotalEnergiesCAFCC semi-finalists have their eyes set on victory- Who will reach the finals
Mshindi mchezo kati ya RS Berkane dhidi ya Constantine atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Stellenbosch FC dhidi ya Simba SC fainali. Source: CAF.

 Faulo ambazo zilichezwa zilisababishwa mwamuzi wa kati kuonyesha kadi za njano ni Stellenbosch FC waliianza kuingia kwenye orodha hiyo kupitia kwa Enninya dakika ya 35 baada ya kumchezea faulo nyota wa Simba, Ellie Mpanzu.

Mchezaji huyo hakukomba dakika 90 za mchezo ambapo aligotea dakika ya 57 nafasi yake ikachukuliwa na Mcaba ambaye alikamilisha dakika zilizobaki kwenye mchezo huo.

Nyota mwingine ni Ibrahim Jabaar ambaye alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 37 ya mchezo huku kwa upande wa Simba SC nyota aliyeingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Mohamed Hussen Zimbwe Jr, Chamou alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 90.

KIKOSI CHA SIMBA KILICHOANZA

Moussa Camara, Chamou, Hamza Jr, Mohamed Hussen, Shomari Kapombe, Fabrice Ngoma. Jean Ahoua, Steven Mukwala, Ellie Mpanzu, Yusuph Kagoma, Kibu Dennis. Akiba ni Ally Salim, Duchu, Nouma, Edwin Balua, Okejepha, Mavambo, Awesu, Mutale, Leonel Ateba.

Mutale aliingia kipindi cha pili ilikuwa dakika ya 70 akichukua nafasi ya kiungo mshambuliaji Kibu Dennis ambaye hakukomba dakika 90 kwenye mchezo wa kimataifa.

UMILIKI WA MPIRA MCHEZO ULIOPITA

Rekodi zinaonyesha kuwa Simba SC ilikuwa na umiliki wa mpira kwa asilimia 57 na wapinzani wao ni asilimia 42 huku mashuti ambayo yalipigwa kuelekea langoni ni 22 kwa Simba SC na wapinzani wao mashuti matano pekee.

Stellenbosch FC walikuwa wakifanya mashambulizi yakushtukiza kuelekea kwenye lango la Simba SC ambapo langoni alianza kipa namba moja Camara.

Share this: