ChalobahChalobah
  • Chelsea FC itakuwa darajani kusaka pointi tatu dhidi ya Everton iliyovurugwa.
  • Moto wa Mohamed Salah ambao hauzimwi kwenye kucheka na nyavu.
  • Wanaoburuza mkia nao watakuwa kazini dhidi ya timu iliyo ndani ya 10 bora

Leo Jumamosi Aprili 26 2025 kuna mechi kali ambazo zinatarajiwa kuchezwa ndani ya Premier League kwa wababe kuwa uwanjani kusaka pointi tatu muhimu.

Sancho
Sancho

Miongoni mwa timu hizo ikiwa ni wiki ya 34 ni Chelsea ambayo ipo nafasi ya sita kwenye msimamo ikiwa imekusanya pointi 57 itakuwa kazini kumenyana na Everton iliyo nafasi ya 13 na pointi 38.

Rekodi znaonyesha kuwa wababe hawa walipokutana uwanjani Desemba 22 2024 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Everton 0-0 Chelsea hivyo waligawana pointi na walipokutana Aprili 15 2024 ilikuwa Chelsea 6-0 Everton na Desemba 10 2023 ilikuwa Everton 2-0 Chelsea.

Wababe hawa watakuwa kazini kwa mara nyingine Uwanja wa Stamford Bridge katika msako wa pointi tatu muhimu uwanjani ndani ya dakika 90 zamoto.

SOUTHAMPTON KAZINI

Southampton iliyo nafasi ya 20 na pointi 11 baada ya kucheza mechi 33 itawakaribisha Fulham ilyo nafasi ya 9 na pointi 48. Southampton haijawa na mwendo mzuri ndani ya mechi za 2024/25 kutokana na kutopata matokeo chanya.

Ugochukwu
Ugochukwu nyota wa Southampton itakayowakabili Fulham. Source: Southampton.

Baada yakucheza jumla ya mechi 33, ushindi ni kwenye mechi 2 na ilipoteza jumla ya mechi 26 na kupata sare kwenye mechi 5 ndani ya uwanja huku ikiwa inakama nafasi ya mwisho kwenye msimamo.

Wapinzani wao Fulham wapo ndani ya 10 bora kwa kuwa ni nafasi ya 9 kwenye msimamo wapo huku wakipata ushindi kwenye mechi 13, waliambulia kichapo kwenye mechi 11 wakikusanya sare 9.

BRIGHTON NA WEST HAM UNITED

Brighton yenye pointi 48 nafasi ya 10 itakuwa kazini dhidi ya West Ham yenye pointi 36 nafasi ya 17 kwenye msimamo. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa wababe hawa kusaka pointi tatu ndani ya uwanja.

Brighton ilipata ushindi kwenye mechi 12 ilizoshuka uwanjani na iliambulia sare 12 ikipoteza mechi 9 ikiwa ndani ya 10 bora kwenye msimamo wa ligi na wapinzani wao West Ham sio timu yakubeza kwa kuwa imekuwa ikipata matokeo kwenye mechi zake.

Ni ushindi kwenye mechi 9 huku ikipoteza mechi 15 na sare 9 ni mchezo ambao unawakutanisha wachezaji wakubwa wanaojua kusaka ushindi na namna yakuvuna pointi moja.

NEWCASTEL UNITED

 Kutoka ndani ya tano bora Newcastle United iliyo nafasi ya 5 baada yakukusanya jumla ya pointi 59 itakuwa kibaruani kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya Ipswich iliyo nafasi ya 18 na pointi 21 kibindoni.

Isak
Isak nyota wa Newcastle United mwenye zali lakucheka na nyavu. Source: Newcastle United.

Matajiri Newcastle United ushindi walipata kwenye mechi 18 wakiambulia sare katika mechi 5 huku wakipoteza mechi 10 msimu wa 2024/25.

Safu yao ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 62 wakiruhusu kufungwa mabao 44 wanakutana na Ipswich ambayo haijawa kwenye mwendo bora katika ushindi ikiwa imeambulia ushindi kwenye mechi nne pekee kati ya 33.

 Ipswich ilipata sare katika mechi 9 ikipoteza jumla ya mechi 20 na ukuta wao umefungwa jumla ya mabao 71 huku safu ya ushambuliaji ikifunga mabao 33.

JUMAPILI SIO YAKITOTO

Wolves yenye pointi 38 nafasi ya 15 itakuwa kazini  dhidi ya Leicester iliyo nafasi ya 19 na pointi 18 huku Bournemouth iliyo nafasi ya 8 itawakaribisha Manchester United iliyo nafasi ya 14 na pointi 38 hizi zote itakuwa ni Aprili 26 na unaweza kubashiri kupitia SportPesa ukakunja mkwanja wako.

Vinara wa Ligi, Liverpool wao wanatarajiwa kuwa kazini Aprili 27 dhidi ya Tottenham kwenye msako wa pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.

Ndani ya Liverpool mchezaji ambayo ni hatari zaidi anaitwa Mohamed Salah huyu ni namba moja kwenye eneo la kucheka na nyavu kwenye Premier League 2024/25 akiwa ametupia jumla ya mabao 27.

Mohamed Salah
Mohamed Salah mshambuliaji namba moja kwa utupiaji Premier League akiwa na mabao 27.Source: Liverpool.

Salah amekuwa katika ubora kwenye mechi za Premier League kutokana na kuhusika kwenye mchango mkubwa wa mabao ndani ya timu hiyo ambayo inaongoza ligi ikiwa na jumla ya pointi 79 baada yakucheza jumla ya mechi 33.

Mbali na suala la kufunga mabao, Salah katengeneza pasi 18 za mabao akiwa ni namba moja katika eneo hili pia anafuatiwa na Bukayo Saka wa Arsenal ambaye katoa pasi 10 za mabao sawa na Antonee Robinson wa Fulham na Jacob Murphy wa Newcastle United.

Salah amehusika kwenye mabao 45 kati ya 75 yaliyofungwa na timu hiyo ukiwa ni mchango mkubwa kwa nyota huyo ndani ya uwanja katika mechi za ushindani jambo ambalo linaongeza thamani yake.

Source: Premier League

Share this: