Clement Mzize na DubeClement Mzize na Dube

YANGA v Coastal Union dakika 90 za jasho zinatarajiwa kutumika Uwanja wa KMC, Complex kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika kuwa kazini Uwanja wa KMC, Complex kusaka pointi tatu dhidi ya Coastal Union.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid baada ya dakika 90 ubao ulisoma Coastal Union 0-1 Yanga, pointi tatu zikirejea Dar.

Jean Baleke v Coastal Union
YANGA v Coastal Union mzuunguko wa pili wanatarajiwa kumenyana Uwanja wa KMC Complex, Aprili 7 2025. Source: Yanga.

Kwenye mchezo huo bao pekee la ushindi wa Yanga inayodhaminiwa na SportPesa lilifungwa dakika ya 24 na mshambuliaji Jean Baleke ambaye alikutana na mkono wa Thank You. Ni mechi tano alipata nafasi kucheza kwenye ligi akikomba dakika 188 na kutupia bao moja.

MILOUD KOCHA YANGA KUHUSU COASTAL UNION

Miloud Hamdi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu kulingana na aina ya timu ambayo wanakwenda kukutana nayo hivyo wataingia kwa tahadhari malengo ikiwa ni kupata pointi tatu muhimu.

Miloud Hamdi
YANGA V Coastal Union, Miloud Hamdi, Kocha Mkuu wa Yanga atakuwa benchi kuongoza kikosi kusaka pointi tatu muhimu. Source: Yanga.

“Ni mchezo ambao utakuwa na ushindani mkubwa, tunajua kwamba hautakuwa mchezo rahisi hivyo kikubwa ni kuwa tayari na wachezaji wanatambua kwamba ambacho tunahitaji ni kupata pointi tatu muhimu.

“Tumetoka kufanya vizuri kwenye mchezo wetu uliopita wa ligi dhidi ya Tabora United hivyo kasi ile tunahitaji kuendelea nayo ukizingatia kwamba kwenye mchezo huu tutakuwa nyumbani na mashabiki wamekuwa wakijotokeza kwa wingi.”

COASTAL UNION KUHUSU YANGA

Joseph Lazaro, kocha msaidizi wa Coastal Union amesema kuwa wanatambua wapinzani wao wanahitaji ubingwa hivyo wataingia kwa tahadhari kubwa ndani ya dakika 90.

“Tunatambua tunakutana na timu ya aina gani kulingana na ushindani ulivyo, wapinzani wetu wanahitaji kutwaa ubingwa, sisi hatuhitaji kuona tunashuka daraja.

“Makosa ambayo yamepita tumefanyia kazi ili kuwa bora ndani ya uwanja, tupo tayari na maandalizi yapo vizuri kuwakabili wapinzani wetu.”

YANGA V COASTAL UNION MATOKEO

Yanga v Coastal Union hawa mchezo wao wa mzunguko wa kwanza ilikuwa Coastal Union 0-1 Yanga msimu wa 2024/25. Kwenye mchezo uliopita ambao ulikuwa ni Kombe la CRDB Federation Cup baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 3-1 Coastal Union.

Miongoni mwa mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa kwa wababe hawa ni fainali ya CRDB Federation Cup, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ilikuwa Julai 2 2022, Yanga 3-3 Coastal Union, bingwa alikuwa Yanga kwa ushindi wa penati 4-1.

YANGA V COASTAL UNION REKODI

Yanga kwenye rekodi msimu wa 2024/25 wamekuwa bora kila idara ambapo safu ya ushambuliaji ni namba moja kwenye eneo la kufunga mabao mengi zaidi kuliko timu zote.

Dubeee
PRINCE Dube nyota wa Yanga ametupia mabao 11 ndani ya ligi msimu wa 2024/25. Source: Yanga.

Ni mabao 61 Yanga imefunga baada ya kucheza mechi 23, wachezaji wawili kutoka Yanga ni wakali kwenye kucheka na nyavu, Prince Dube na Clement Mzize hawa wote wawili wametupia mabao 11 kila mmoja.

Kwenye mchezo uliopita wa Yanga dhidi ya Tabora United wakati wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0, Dube na Mzize walifunga bao mojamoja kwa kila mmoja na bao lingine lilifungwa na Israel Mwenda ambaye alipachika bao hilo kwa pigo huru akiwa nje ya 18.

Ni mabao 9 safu ya ulinzi iliokota kwenye nyavu ikiwa nit imu namba mbili kufungwa mabao machache zaidi kwenye ligi. Timun amba moja kufungwa mabao machache ni Simba ikiwa imetunguliwa mabao 8.

Ndani ya dakika 2,070 safu ya ushambuliaji ya Yanga ina wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 33. Ni pointi 61 zipo kibindoni wakiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo.

Ushindi kwa Yanga ni kwenye mechi 20, walipata sare kwenye mchezo mmoja ilikuwa JKT Tanzania 0-0 Yanga, ugenini, mechi mbili ilipoteza dhidi ya Azam FC na Tabora United.

COASTAL UNION REKODI ZAO

Sportpesa-Alphonce mkeka

Ni muda wako kupitia simu ya mkononi kuvuna mkwanja kwa kubashiri mechi na SportPesa.

Coastal Union ni mechi 24 ilishuka uwanjani ikiwa nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi, ushindi kwenye mechi 5, sare mechi 10, ilipoteza jumla ya mechi 9. Safu ya ushambuliaji ya timu hiyo imetupia jumla ya mabao 19 na ukuta umeruhusu mabao 25.

Coastal Union kibindoni ni pointi 25 wanazo saw ana idadi ya mabao ambayo wameruhusu kufungwa kwenye mechi za ligi. Ndani ya dakika 2,160 ina wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 113.

Share this: