C ClementC Clement

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wameweka wazi kuwa hesabu zao ni kupata pointi tatu muhimu kwenye mechi ambazo wanacheza ndani ya uwanja katika dakika 90 za msako wa ushindi kwenye ligi namba nne kwa ubora Afrika.

Ipo wazi kwamba Yanga inayodhaminiwa na SportPesa baada ya mechi 20 za ligi ni ushindi kwenye mechi 17 wakiambulia sare mchezo mmoja ilikuwa mbele ya JKT Tanzania ubao iliposoma 0-0 na kupoteza mechi mbili wakiwa na pointi 50 kibindoni. Kwenye mechi zao 18 ambazo ni dakika 1,800 wamepeta kwa kuvuna rekodi nzuri wakiwa namba moja na kinara wa utupiaji ni Clement Mzize.

WAKALI MBELE YA MASHUJAA

Dubeee
Dube Prince nyota wa Yanga aliyefunga mabao yote matatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mashujaa. Source: Yanga.

Kwa upande wa Mashujaa, safu yao ya ushambuliaji baada ya mechi 20 ni mabao 17 imefunga huku ukuta wat imu hiyo ukiruhusu mabao 18 ni pointi 23 wamekusanya Mashujaa wakiwa nafasi ya 7 kwenye msimamo.

Yanga kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza walikomba pointi tatu mbele ya Mashujaa kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 3-2 Mashujaa ilikuwa ni Desemba 19 2024 na nyota Prince Dube alifungua akaunti ya mabao kwenye ligi na kufunga hat trick ya kwanza.

YANGA BALAA LAO NI ZITO

Kwenye eneo la ushambuliaji Yanga balaa lao ni zito wakizipoteza timu zote Bongo mpaka watani zao wa jadi Simba kwa kuwa na safu kali ya ushambuliaji. Mfungaji wa bao la kwanza msimu wa 2024/25 ni Maxi Nzengeli alifunga kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

Maxi Nzengeli
Maxi Nzengeli kiungo mshambuliaji wa Yanga ambaye ni mfungaji wa bao la kwanza ndani ya msimu wa 2024/25. Source: Yanga.

Baada ya mechi 20 ambazo ni dakika 1,800 safu ya ushambuliaji ya Yanga imetupia mabao 50 ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 36 ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani.

Yanga ni timu namba moja ambayo imepata ushindi mkubwa kwenye mechi zake ikipata ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya KMC na iliwatungua mabao 6-1 Ken Gold kwenye mechi za ligi zote zilichezwa Uwanja wa KMC, Complex.

Wakati ikiwa namba moja kwenye ligi na pointi zake 52, watani zao wa jadi Simba wapo nafasi ya pili kwenye msimamo ni timu namba mbili kwa timu zenye mabao mengi  imetupia mabao 41 baada ya kucheza mechi 19. Ni dakika 1,710 imekomba uwanjani ina wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 41 ndani ya uwanja hivyo na kinara wautupiaji ni Jean Ahoua mwenye mabao 10 na pasi tano za mabao.

M- Camara
Camara kipa namba moja wa Simba ambaye ameanza kikosi cha kwanza mechi 19 za ligi msimu wa 2024/25. Source: Simba.

Mchezo pekee ambao Simba ilipata ushindi mkubwa ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar walipopata ushindi wa mabao 5-2 llikuwa Uwanja wa Kaitaba ikiandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kupata ushindi mkubwa ndani ya msimu wa 2024/25 baada yah apo haijavunja rekodi yake hiyo.

YANGA KUONGEZA MTAMBO MWINGINE

Jonathan Sowah raia wa Ghana inaelezwa kuwa yupo kwenye rada za mabosi wa Yanga ambao wanahitaji kuipata saini yake. Sowah ndani ya ligi amefunga mabao matatu anaingia kwenye orodha ya washambuliaji waliomtungua kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra kwenye mchezo wa ligi msimu wa 2024/25 akiwa katupia jumla ya mabao matatu.

Rekodi zinaonyesha kuwa bao la kwanza nyota huyo alifunga Februari 7 ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar walipotoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 Uwanja wa Liti. Bao la pili alifunga kwenye mchezo wake wa tatu kuanza kikosi cha kwanza dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Meja Isahmuyo, Februari 13 2025 baada ya dakika 90 ubao ulisoma JKT Tanzania 0-1 Singida Black Stars.

Kwenye mchezo huo ugenini alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo baada ya dakika 90 kwa kuwa bao hilo lilikuwa ni la ushindi kwa Singida Black Stars wakikomba pointi tatu mazima. Sowah alipachika bao la tatu kwenye mchezo dhidi ya Yanga inayotajwa kuwa itamalizana naye dirisha lijalo la usajili kwa kuinasa saini ya nyota huyo mwenye uwezo mkubwa kutumia mguu wake wa kulia kwenye kucheka na nyavu.

Sowah
Jonathan Sowah nyota wa Singida Black Stars mwenye mabao matatu ndani ya ligi akiwa ametupia mabao matatu msimu wa 2024/25 kwenye mechi za ushindani. Source: Singida Black Stars.

Ni Februari 17 2025 dakika za jioni Sowah alimtungua Diarra akiwa ndani ya 18 kwa mguu wake wa kulia akitumia makosa ya kipa huyo kutema mpira uliopigwa na Edmund John akiwa nje kidogo ya 18. Mwisho ubao wa Uwanja wa KMC Complex ukasoma Yanga 2-1 Singida Black Stars likiwa ni bao la tatu kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Medeama raia wa Ghana

Mchezo wa pili kwa nyota huyo ilikuwa dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa KMC Complex kwenye mchezo huu alianza kikosi cha kwanza na alishuhudia Februari 10 2025 ikiwa chungu kwa ubao wa Uwanja wa KMC Complex kusoma KMC 2-0 Singida Black Stars.

HIZI HAPA ZA FEBRUARI 22

Ken Gold v KMC, Uwanja wa Sokoine, Mbeya

Dodoma Jiji v Fountain Gate, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma

Share this: