KMC Vs YangaKMC Vs Yanga

Kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC ambao unatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa KMC leo jioni, kocha mkuu wa Yanga, Hamdi Miloud amechimba mkwara mzito kuwa wameweka mkakati mzito wa kushinda kila mchezo uliombele yao.

KMC Vs Yanga
KMC Vs Yanga

Yanga wataingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kutoa sare katika mchezo wao uliopita dhidi ya JKT Tanzania, matokeo ambayo yaliwafanya waporomoshwe kutoka kileleni mwa msimamo huo.

Ikumbukwe unaweza kujishindia mamilioni kwa kuweka ubashiri wako wa mchezo huu na mingine mingi kupitia Kampuni bora ya kubashiri michezo ya SportPesa kwa kuingia kwenye tovuti ya www.sportpesa.co.tz

ALICHOSEMA KOCHA YANGA

Miloud Hamdi
Miloud Hamdi

“Katika mchezo uliopita tulipata matokeo yasiyoridhisha dhidi ya JKT Tanzania na tunataka kubadilisha hali hii katika mchezo dhidi ya KMC FC. Kwa upande wangu, mchezo dhidi ya JKT Tanzania ulikuwa ni mchezo wangu wa kwanza nikiwa na Young Africans, na kama Kocha mpya, ningependa kushinda mchezo wangu wa kwanza, lakini tulitoka sare.”

“Tumejiandaa kiakili kuhakikisha tunapata ushindi na kuepuka kuwavunja mioyo ya mashabiki wetu. Sisi sote, benchi la ufundi na wachezaji tunatamani sana kushinda mchezo huu. Ninakubaliana na mashabiki wana kila sababu ya kutoridhika kwa sababu sisi ni Klabu kubwa na mashabiki wanataka kushinda kila mchezo. Amini, hata sisi makocha na wachezaji tunataka kushinda kila mchezo. Kwa hiyo, tutafanya kila tuwezalo kushinda mchezo huu kwa sababu tunahitaji alama tatu.

“Ninataka kuwapa ujumbe mashabiki wa Young Africans kwamba tunapambana na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili yao na wachezaji wanajua wanachopaswa kufanya siku zijazo. Tuko hapa kushinda mataji, hatuko hapa kwa ajili ya kazi tu, mashabiki wetu wasikate tamaa kwa sababu ya sare moja bado tuna michezo mingi ya kucheza. Kila kitu kinawezekana, bado hatujachelewa, tuna muda, lakini lazima tufanye kila tuwezalo kushinda michezo yote ili kuwapa furaha mashabiki wetu kwa sababu wao wako pamoja nasi, na sisi pia tuko pamoja nao,” amesema Miloud Hamdi.

Kwa niaba ya wachezaji, nahodha wa kikosi hicho, Bakari Mwamnyeto amesema: “Kwa niaba ya wachezaji wenzangu, tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo. Tunatambua ugumu wa kila mechi hasa katika mzunguko huu wa mwisho wa ligi. Tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti na tutafanya kila jitihada kupata alama tatu.”

Bakari Mwamnyeto
Bakari Mwamnyeto

AJALI YAPANGUA MECHI SIMBA Vs DODOMA

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania TPLB imetoa taarifa ya kuahirisha mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Dodoma Jiji ambao ulipangwa kuchezwa Jumamosi, Februari 15 katika Uwanja wa KMC Complex. TPLB imeweka wazi kuwa sababu ya kuahirishwa mchezo huo ni kutokana na wachezaji wa Dodoma Jiji kupata ajali katika Wilaya ya Ruangwa wikiendi iliyopita.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi inasema Maafisa na baadhi ya wachezaji hawapo sawa kiafya hivyo hawataweza kuwa sehemu ya mchezo hivyo mechi imeahirishwa. TPLB imesema itatoa taarifa muda si mrefu ya lini mchezo huo utapigwa tena.

Ikumbukwe Simba walikuwa wanauelekea mchezo huu mara baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wao uliopita dhidi ya Tanzania Prisons uliopigwa hapohapo KMC. Ushindi huo dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex uliwafanya Simba kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

MCHEZO ULIKUWAJE?

Simba Vs Tanzania Prisons
Simba Vs Tanzania Prisons

Simba waliuanza mchezo huo kwa kasi huku wakitafuta bao la mapema dakika 20 za mwanzo kiasi cha kufanya mashambulizi ya hatari sita langoni mwa Prisons lakini kikwazo kikawa mlinda mlango, Sebusebu Samson.

Jean Charles Ahoua aliipatia Simba bao la kwanza dakika ya 29 kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe. Elie Mpanzu aliwapatia Simba bao la pili dakika ya 45 kwa shuti kali la chinichini akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi ya Leonel Ateba.

Dakika moja baadae, Ladaki Chasambi aliwapatia bao la tatu baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Kapombe.

Kikosi cha Simba kilichocheza mchezo huo ni: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr (Nouma 64′) Che Malone, Hamza (Chamou 33′) Kagoma (Fernandez 45′) Chasambi (Balua 64′) Ngoma (Mukwala 75′), Ateba, Ahoua, Mpanzu

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.