YANGA imeibuka na ushindi dhidi ya Al Hilal ugenini kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni dakika 90 za nguvu ndani ya uwanja mchezo ukikamilishwa katika dakika 45 za Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Sead Ramovic wakiwa wanakwenda kwa sera ya gusa achia.
Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ndani ya Ligi Kuu Bara ilikuwa kwenye umakini mkubwa katika kila eneo huku kiungo Khalid Aucho akiwa miongoni mwa wachezaji waliochezewa faulo zaidi ya mbili katika mchezo wa kimataifa.
DAKIKA 45 ILIKUWA GUSA ACHIA

Katika dakika 45 za mwanzo, Yanga waliutawala mchezo kwa kugusa na kuachia kuelekea lango la wapinzani wao Al Hilal amba oni vinara wa kundi A katika hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kiungo mshambuliaji wa Yanga alifunga bao la kuongoza mapema katika dakika 45 za mwanzo ilikuwa ni dakika ya 7 kwa shuti kali akiwa nje ya 18 akitumia pasi ya Dickson Job.
Djigui Diarra alikamilisha dakika 45 za mwanzo bila kuruhusu nyavu zake kutunguliwa huku beki Kibwana Shomari akiwa miongoni mwa mabeki walioanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Ibrahim Bacca aliokoa hatari dakika ya 37 ambapo Al Hilal walikuwa wakipambana kusaka bao la kuweka usawa ndani ya dakika 45 za mwanzo ambapo Yanga ilipata kona zilizopigwa na Pacome ilikuwa dakika ya 3, 4, 32.
Clement Mzize yeye alikuwa akiwasumbua mabeki wa Al Hilal na alicheza faulo dakika ya 43 ya mchezo huku Prince Dube yeye dakika yalikuwa akipanda na kushuka kuelekea langoni mwa Al Hilal
Ikumbukukwe kwamba wababe hawa walipokutana katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Mkapa, pointi tatu zilikuwa ni mali ya Al Hilal kwa ushindi wa mabao 2-0 huku Yanga ikiyeyusha pointi tatu kwenye mchezo wa kwanza.
KIPINDI CHA PILI KAZIKAZI

Kipindi cha pili ilikuwa kazikazi kwa timu zote mbili kutafuta matokeo huku beki Kibwana Shomari akiwa kwenye majukumu yake kuokoa hatari ikiwa ni pamoja na dakika ya 63, 68 na alicheza faulo dakika ya 63 naye alichezewa faulo dakika ya 64.
Prince Dube mshambuliaji wa Yanga dakika ya 53 shuti lake lilikwenda nje ya lango na alicheza faulo dakika ya 65.
Mchezo uliopita kwa Yanga ilikuwa dhidi ya TP Mazembe ambapo walipata ushindi wa mabao 3-1 mabao ya Yanga yalifungwa na Clement Mzize huyu alifunga mabao mawili na nyota Aziz Ki alifunga bao moja kwenye mchezo huo Yanga walipovuna pointi tatu mbele ya TP Mazembe ambayo imeumaliza mwendo kimataifa.
Issa Fofana kipa wa Al Hilal alikutana na balaa la Ki mapema dakika ya 7 na aliokoa hatari nyingine dakika ya 44 kwa shuti la Ki aliyekuwa akipambana kufunga bao lingine kwenye mchezo huo.
Yanga walipiga mashuti matatu na mawili yalilenga lango huku Al Hilal wakipiga mashuti matano na katika hayo ndani ya dakika 45 rekodi zinaonyesha kuwa hakuna shuti ambalo lilenga lango la Yanga ambapo mlinda mlango alianza Diarra.
HIKI HAPA KIKOSI CHA YANGA
Djigui Diarra, Kibwana Shomari, Ladack Boka, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Khalid Aucho, Clement Mzize, Mudathir Yahya, Prince Dube, Aziz Ki na Pacome.
Wachezaji wa akiba ni Aboutwalib Mshery, Nickson Kibabage, Bakari Nondo, Sureboy, Duke Abuya, Shekhan, Farid Mussa, Clatous Chama, Kennedy Musonda.
WATANI WAMETANGULIA

Watani wa jadi wa Yanga ambao ni Simba tayari wametinga hatua ya robo fainali kwenye Kombe la Shirikisho baada ya kuvuna pointi 10 kutoka kundi A ambalo lilikuwa na ushindani mkubwa.
Simba kutoka Tanzania ilikuwa na kibarua cha kusaka dhidi ya Bravos ambapo walishuhudia ubao ukisoma Bravos 1-1 Simba, bao la Leonel Ateba limefungua milango ya kutinga hatua ya robo fainali kimataifa wakiwa na mchezo mmoja mkononi kukamilisha mchezo wa mwisho kimataifa hatua ya makundi.
Simba inapeperusha bendera kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ambapo kwenye mechi zake mbili zote ilizocheza Uwanja wa Mkapa ilivuna pointi sita ina kete moja Uwanja wa Mkapa dhidi ya vinara wa kundi Constatine ambapo mshindi atamaliza akiwa namba moja.

