Mpanzu v JKT TanzaniaMpanzu v JKT Tanzania

DESEMBA 2024 inafungwa kibabe kwa wababe kuwa uwanjani kusaka pointi tatu ndani ya dakika 90 ambapo Yanga tayari wamesharejea Bongo kuwavutia kasi wapinzani wao Fountain Gate Uwanja wa KMC, Complex na Simba ndani ya Singida kwa sasa kuwavutia kasi Singida Black Stars.

MASTAA Yanga
Mastaa Yanga chaguo la kwanza ndani ya Desemba 2024. Source: Yanga.

Ikumbukwe kwamba Yanga inayodhaminiwa na SportPesa kwenye mechi zake za hivi karibuni imerejea katika ubora matokeo yakipatikana uwanjani ikiwa ni mwendo wa gusa achia.

Simba ina kibarua kiziti ugenini itakuwa dhidi ya wakali kutoka Singida kwenye mchezo unatajwa kwamba utakuwa na ushindani mkubwa kwa vinara hao wa ligi ndani ya 2024/25 kushuka uwanjani kutokana na ubora wa timu zote mbili.

HUYU HAPA NAHODHA

Zimbwe Jr
Zimbwe Jr nahodha wa Simba 2024. Source: Simba.

Mohamed Hussen Zimbwe Jr nahodha wa Simba amesema kuwa mpango mkubwa kwenye mechi ambazo wanacheza ni kupata matokeo hivyo wataendelea kupambana katika mechi zao zote.

Katika mchezo uliopita wakiwa Uwanja wa KMC Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 1-0 JKT Tanzania bao likifungwa kwa mkwaju wa penalti na Jean Ahoua dakika ya 90+3 ambapo linakuwa ni bao lake la 7 ndani ya ligi.

Kituo kinachofuata kwa Simba ni Desemba 28 itakuwa ugenini dhidi ya Singida Black Stars mchezo unoatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa wababe hawa wawili.

Tayari kikosi cha Simba kimetia timu Singida kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wao huo baada ya kuvuna pointi tatu nyumbani dakika za lala salama.

Zimbwe amesema:”Kila mchezo kwetu ni muhimu na tunauchukulia kwa umakini, maandalizi mazuri na maelekezo ya benchi la ufundi yanatupa mwanga wa kupata kile ambacho tunahitaji, mashabiki wazidi kuwa nasi.”

 

YANGA WAIVUTIA KASI FOUNTAIN GATE

Desemba 26 Yanga waliwasili Dar wakitokea Dodoma. Ikumbukwe kwamba Yanga ilikuwa na kazi Dodoma Desemba 25 na ubao wa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ukasoma Dodoma Jiji 0-4 Dodoma Jiji FC. Baada ya kuwasili Dar, Yanga waliekea kambini moja kwa moja kuanza maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Jumapili dhidi ya Fountain Gate FC.

MASHINE YA KIJERUMANI HII HAPA

Ramovic
Ramovic Sead mashine ya kijerumani Desemba itakuwa kazini, Uwanja wa KMC, Complex. Source: Yanga.

Kocha Mkuu wa Yanga, Saed Ramovic amesema kuwa bado kazi inaendelea kwenye mechi za ushindani na malengo ni kuona wanakuwa bora katika mechi za ushindani.

Kituo kinachofuata kwa Yanga watakuwa nyumbani Desemba 29 wataikabilia Fountain Gate, mchezo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Complex Mwenge, Dar.

Ikumbukwe kwamba mchezo wao uliopita walikomba pointi tatu Uwanja wa KMC walipocheza na Tanzania Prisons ubao ulisoma Yanga 4-0 Tanzania Prisons mchezo wa kwanza kucheza hapo ilikuwa Yanga 3-2 Mashujaa.

Kwenye mechi mbili Uwanja wa KMC ni mabao 7 walifunga Yanga na kufungwa mabao mawili, mchezo wa tatu ugenini walishinda mabao 4-0 hivyo ndani ya dakika 270 safu ya ushambuliaji ya Yanga imefunga mabao 11 na ukuta umeruhusu mabao mawili pekee.

Ramovic amesema: “Tunatambua ushindani ni mkubwa na kila timu ipo imara ila kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri katika mechi zetu ambazo tunacheza, ninawapongeza wachezaji wanafanya kazi kubwa uwanjani.”

AZAM KAZINI MBELE YA WAJEDA

Toto Fei
FEI Toto kiungo wa Azam FC mwenye pasi 7 za mabao ndani ya ligi. Source: Azam FC.

Matajiri wa Dar, Azam FC chini ya Kocha Mkuu Rachid Taoussi watakuwa kazini kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya JKT Tanzania mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex. Ikumbukwe kwamba JKT Tanzania mchezo wao uliopita walipoteza dakika za lala salama dhidi ya Simba.

Ilikuwa namna hii baada ya dakika 90 ubao ulikuwa unasoma Simba 0-0 JKT Tanzania kutokana na mpango kazi wa kujilinda kwa JKT Tanzania kujibu huku kipa Yakoub Suleiman akiwa bora kwenye kuokoa hatari zilizokuwa zinapigwa na Leonel Ateba, Ellie Mpanzu na alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo.

Zikiwa zimebaki dakika chache mpira kugota mwisho katika dakika za nyongeza, Simba wakapata penalti ikafungwa na Jean Ahoua dakika ya 90+3 hivyo JKT Tanzania walipoteza na Simba ikasepa na pointi tatu.

Kocha wa Azam FC ameweka wazi wanatambua uimara wa wapinzani wao hivyo wataingia kwa tahadhari kubwa kwenye kusaka ushindi ndani ya uwanja kutokana na aina ya wapinzani wao.

“Tunatambua kwamba wapinzani wetu ni imara hivyo tutacheza nao kwa tahadhari kubwa malengo ni kuona kwamba tunapata pointi tatu hilo linawezekana.”

 

RATIBA YA LIGI KUU BARA

Desemba haipoi kwa kuwa ni bandika bandua ambapo kazi inaendelea kwa timu kuwa uwanjani kusaka pointi tatu muhimu ndani ya uwanja. Hii hapa ratiba ilivyo:-

Desemba 27 2024

Azam FC ipo nafasi ya tatu pointi 33 baada ya mechi  15 mchezo wake uliopita ilishinda mabao 2-0 Fountain Gate v JKT Tanzania, nafasi ya 8 pointi 19  baada ya kucheza mechi 15 itakuwa saa 1:00 usiku

Desemba 28 2024

Singida Black Stars iliyo nafasi ya nne na pointi 33 v Simba,nafasi ya kwanza pointi 37, saa 10:00 jioni

Dodoma Jiji nafasi ya 12 pointi 16 v Mashujaa, nafasi ya 7 pointi 19, saa 12:15, jioni

Desemba 29 2024

Seleman Mwalimu
Seleman Mwalimu mshambuliaji wa Fountain Gate 2024. Source: Fountain Gate.

Yanga nafasi ya pili pointi 36 v Fountain Gate, nafasi ya sita pointi 20, saa 10:00 jioni

Coastal Union nafasi ya 10 pointi 17 v KMC, nafasi ya 9 pointi 18 itakuwa saa 10:00 jioni

 

Share this: