MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ndani ya dakika 180 kwenye mechi za Uwanja wa KMC wamekuwa kwenye ubora wao wakipata ushindi kwa kukomba jumla ya pointi sit ana kufunga mabao 7 huku safu ya ulinzi inayongozwa na Dickson Job ikiruhusu mabao mawili yakufungwa.
Kwa mwendo ambao wamekwenda nao Yanga katika mechi mbili zinawafanya mashabiki wa timu hiyo kutamba kwa hawacheki na wowote bali ni msako wa matokeo na Desemba 23 waliwasili salama Dodoma Jiji kwa maandalizi ya mwisho.

.
Ikumbuwek kwamba mechi zote hizo zilichezwa Uwanja wa Azam Complex na sasa kituo kinachofuata kwa Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ni ugenini dhidi ya Dodoma Jiji mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
MATOKEO YAO UWANJANI

Katika mechi mbili zilizopita Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Sead Ramovic ilipata matokeo chanya ilikuwa Yanga 3-2 Mashujaa na Yanga 4-0 Tanzania Prisons. Mchezo wa kwanza kwa mshambuliaji Prince Dube wa Yanga kufunga aliondoka na mpira kwa kufunga hat trick.
Desemba 25 Yanga inatarajiwa kushuka uwanjani kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya Dodoma Jiji mchezo wake uliopita ilikuwa ugenini Uwanja wa Liti dhidi ya Singida Black Stars baada ya dakika 90 ubao ukasoma Singida Black Stars 2-1 Dodoma Jiji.
Katika mechi mbili mfululizo mshambuliaji Prince Dube ameandika rekodi yake kwa kufunga mechi mbili mfululizo alianza na hat trick dhidi ya Mashujaa na alifunga bao moja dhidi ya Tanzania Prisons.
Kwa upande wa washambuliaji ni namba kwa watupiaji akiwa ametupia mabao manne na upande wa mabeki namba moja ni Ibrahim Bacca ambaye ametupia mabao manne.
Dube ameweka wazi kuwa ni furaha kwake kufunga kwa kuwa alikuwa anapita nyakati ngumu hasa pale alipokuwa hajafunga kwa muda ndani ya ligi.
“Ninafurahi kuona timu inashinda, wakati sijafunga kwenye ligi nilikuwa napita kwenye kipindi kigumu lakini mwisho nimefunga kwa ajili ya timu hili ni jambo kubwa ninamshukuru Mungu.”
NAFASI ZA WASHINDANI LEO
Singida Black Stars iliyo nafasi ya nne na pointi 30 baada ya kucheza mechi 14 itakuwa na kibarua cha kusaka pointi dhidi ya Ken Gold iliyo nafasi ya 16 na pointi 6 baada ya mechi 15.

Dodoma Jiji nafasi ya 11 pointi 16 baada ya mechi 14 ndani ya ligi msimu wa 2024/25. Michezo yote hii una nafasi ya kubashiri kupitia SportPesa.
RATIBA YA MECHI NYINGINE
Singida Black Stars itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu dhidi ya Ken Gold mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Liti. Mchezo uliopita kwa Singida Black Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji.
Desemba 24 leo Simba itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya JKT Tanzania mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex saa 10:00. Simba imetoka kuvuna pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba.
DESEMBA 25 CHRISTMAS
Fountain Gate itawakaribisha Namungo saa 8:00 mchana na Dodoma Jiji dhidi ya Yanga itakuwa nis aa 10:00 mchana.
Siku ya kufungua maboxi ya zawadi Desemba 26 itakuwa ni Tanzania Prisons ambayo imetoka kupoteza pointi tatu dhidi ya Yanga itamenyana na Pamba Jiji mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine.
KUNA MASHINE ZINAFUATILIWA KWENYE MECHI

Ikiwa ni mwendelezo wa mechi za ushindani ndani ya uwanja kwa kila timu kusaka pointi tatu kwa mbinu kali uwanjani kuna mashine za kazi zinafuatiliwa ili kuingia kwenye changamoto mpya katika timu nyingine.
Tayari Yanga wamemalizana na Israel Mwenda ambaye ni beki aliyekuwa ndani ya Singida Blacks Stars, kwa sasa wanaendelea kusaka wachezaji wengine kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho huku baadhi ya nyota wakitajwa kuwa kwenye rada za Yanga.
Miongoni mwa nyota ambao wanatajwa kuwa kwenye rada za Yanga ni Josephat Bandawa Singida Black Stars ambaye amekuwa kwenye ubora wake ndani ya timu hiyo.
Ikumbukwe kwamba Mwenda alitambulishwa ndani ya Yanga akiwa ni mchezaji wa kwanza kwenye dirisha dogo jina lake kuwa ni njano na kijani ameanza mazoezi na wachezaji wenzake yeye ni beki mwenye uwezo wa kucheza kulia na kushoto.
Aly Kamwe Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa baada ya Mwenda kuna wachezaji wengine wapo njiani hivyo watawashangaza kutokana na jambo hilo.
“Unaona tumemtambulisha Israel Mwenda huyu ni mchezaji wa kazi haina maana kwamba kazi imeisha hapana bado tunaendelea na tutawambulisha wengine hivi karibuni.
“Ukitaka kujua ni nani anakuja sikuambii kwa sasa na wala hatutawaambia bali mpaka usajili utakapokamilika tunajua malengo yetu na yote yatatimia.”

