Mohamed HussenMohamed Hussen

DESEMBA inazidi kukatika kwa kasi huku wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la kimataifa Yanga na Simba wakiwa na kazi nzito kusaka ushindi ndani ya dakika 90 kwenye mechi ambazo wanacheza. Ipo wazi kuwa katika mechi za ugenini wote wawili waliambulia maumivu baada ya kushindwa kupata ushindi.

Aziz Ki
Aziz Ki kiungo wa Yanga 2024. Source: Yanga.

Yanga inayodhaminiwa na SportPesa haijaanza kwa mwendo mzuri kimataifa hatua ya makundi kwenye mechi mbili mfululizo ikipoteza pointi sita msimu wa 2024/25 kituo kinachofuata itakuwa ugenini dhidi ya TP Mazembe.

Ikumbukwe kwamba Desemba 8 2024, Al Hilal walikomba pointi tatu dhidi ya TP Mazembe kwa ushindi wa mabao 2-1 ambapo bao la ushindi kwa Al Hilal lilifungwa dakika ya 90 kupitia kwa Jean Cloude na bao la uongozi lilifungwa dakika ya 21 kwa mkwaju wa penalti kupitia kwa Mohamed Abdelrahman huku lile la TP Mazembe likifungwa dakika ya 64 na mtupiaji ni Oscar Kabwit.

RATIBA YA YANGA DESEMBA BALAA

Chama
Chama Clatous nyota wa Yanga ambaye kwenye mchezo dhidi ya MC Alger ugenini alionyeshwa kadi moja ya njano. Source: Yanga.

Kundi A vinara ni Al Hilal wakiwa na pointi sita kibindoni wanafuatiwa na MC Alger wenye pointi nne, TP Mazembe ni pointi moja wakiwa nafasi ya tatu na kutoka Tanzania wawakilishi Yanga wapo nafasi ya nne wakiwa hawajakomba pointi baada ya kucheza mechi mbili ambazo ni dakika 180.

Desemba 14 itakuwa ni TP Mazembe v Yanga watakuwa ugenini kwa mara nyingine tena kimataifa baada ya kutoka ugenini na sasa wapo njiani kurejea Dar kwa ajili ya maandalizi mengine ya kuelekea DR Congo kwenye mchezo wao ujao kimataifa ugenini.

Desemba 19 itakuwa dhidi ya Mashujaa mchezo wa ligi unatarajiwa kuwa mchezo wa kwanza ndani ya Uwanja wa KMC, Complex. Desemba 22 2024 itakuwa ni Yanga v Tanzania Prisons huu pia ni NBC Premier League Uwanja wa KMC Complex.

Desemba 25 itakuwa ni dhidi ya Dodoma Jiji watakuwa ugenini na funga kazi ni Desemba 29 2024 dhidi ya Kagera Sugar, watakuwa nyumbani.

UBAYA UBWELA WABUMA

Zimbwe Jr
Zimbwe Jr nahodha wa Simba kwenye majukumu kimataifa 2024 dhidi ya CS Constantine. Source: Simba.

Ubaya ubwela, Simba  Desemba 8 2024 ulibuma ugenini licha ya dakika 45 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi kuwa mali ya Simba mwanzo mwisho na walipata bao la mapema kupitia kwa nahoda Mohamed Hussen Zimbwe Jr dakika ya 24.

Kipindi cha pili ubaya ubwela ukabuma ambapo beki wa Simba, Abdulazack Hamza alijifunga dakika ya 47 na alipata maumivu kwenye mchezo huo alishindwa kusepa na dakika 90 nafasi yake ilichukuliwa na Mavambo dakika ya 55.

Bao la pili lilifungwa na Jean Dib ambaye ni nahodha anavaa jezi namba 10 alifunga bao la pili dakika ya 51 likadumu mpaka mwisho wa mchezo likiwapa pointi tatu wapinzani hao ambao kwa sasa ni vinara wa kundi A wakiwa na pointi sita.

SEMAJI HILI HAPA

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa matokeo waliyopata dhidi ya CS Constantine ni mabaya kwa kuwa walikuwa na nafasi ya kupata ushindi hivyo wanajipanga kwa mechi ijayo wakiwa nyumbani.

“Kwenye hatua ambayo tupo kwa sasa kila timu inapambana kupata matokeo nyumbani, unaona tulikuwa na nafasi yakushinda mchezo wetu bahati mbaya tukashindwa hivyo hayajawa matokeo mazuri kwetu.

“Matokeo tuliyopata dhidi ya CS Constantine ni mabaya na kilichotokea hatuwezi kubadili sasa ni hesabu kuelekea mchezo wetu wa tarehe 15 ambapo tutakuwa nyumbani. Mashabiki tunawaomba tuwe pamoja kuelekea mchezo wetu muhimu.”

Katika mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya CS Constantine baada ua dakika 90 ubao ulisoma CS Constantine 2-1 Simba na bao la Simba likifungwa na Mohamed Hussen dakika ya 24.

Mchezo ujao kwa Simba itakuwa ni dhidi ya CS Sfaxine iliyotoka kupoteza kwa kufungwa mbaoa 3-1 dhidi ya Bravos wote wakiwa kundi A ambalo vinara ni CS Constantine wenye pointi sita.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa kufunga Novemba  kwa Simba ilikuwa katika kombe la Shirikisho Afrika walipopata ushindi wa bao 1-0 Bravos, Uwanja wa Mkapa ilikuwa Novemba 27 2024.

HIZI HAPA KETE ZIJAZO KWA SIMBA

 

Fadlu Davids
Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba 2024. Source: Simba.

Desemba 15 itakuwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Fadlu Davids v Sfaxine kimataifa Uwanja wa Mkapa. Desemba 18 itakuwa dhidi ya Ken Gold, NBC Premier League Uwanja wa KMC, Desemba 21 itakuwa dhidi ya Kagera Sugar ugenini na funga kazi itakuwa ugenini dhidi ta Tabora United.

Mchezo dhidi ya Tabora United unatarajiwa kuchezwa Desemba 28 2024 Simba itakuwa ugenini. Ipo wazi kwamba Simba walipocheza na Tabora United kwenye mzunguko wa kwanza walikomba pointi tatu mazima.

Share this: