Ateba v AuchoAteba v Aucho

KIMATAIFA kazi kubwa inatarajiwa kufanyika kwa wawakilishi wa Tanzania ndani ya dakika 90 ambapo Yanga itakuwa na kazi kusaka ushindi dhidi ya Al Hilal ya Sudan mchezo unatarajiwa kuchezwa Novemba 26 2024 na Simba ni Novemba 27 2024 dhidi ya Bravos.

Yanga inayodhaminiwa na SportPesa mchezo wao ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo nahodha wa timu hiyo kwa niaba ya wachezaji wengine amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni na malengo ni kupata ushindi.

Bakari
Bakari Nondo nhodha wa Yanga, 2024/25. Source: Yanga.

“Mchezo wetu ni muhimu na tunatambua kwamba utakuwa na ushindani mkubwa, wachezaji tumekubaliana kupata ushindi na kucheza kwa kushirikiana mwanzo mwisho kwenye mchezo huo kutokana na kila mmoja kuwa tayari na matokeo ambayo yalipita ilikuwa kwenye ligi sasa ni Ligi ya Mabingwa Afrika.”

Kwa upande wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids ina kazi kwenye anga la kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika na itashuka uwanjani Novemba 27 2024 Uwanja wa Mkapa dhidi ya Bravos ya Angola kwenye msako wa pointi tatu muhimu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

SEMAJI NENO LAKE HILI HAPA

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally, ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wao na Jumatano itakuwa ni mapumziko hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo huo kwa ajili ya kuwapa nguvu wachezaji wao

“Tarehe 27 tuna jambo kubwa kwenye Uwanja wa Mkapa. Tunahitaji kuanza vizuri hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Ushindi wa Simba unakutegemea wewe Mwanasimba, tambua ya kwamba tiketi utakayonunua ni silaha muhimu ya kuisaidia Simba siku hiyo.

“Tunatambua siku hiyo ni siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa, ukishamaliza kupiga kura yako elekea Uwanja wa Mkapa. Asibaki Mwanasimba siku hiyo, tambua kwamba ushindi wa Simba unapatikana kwa ushirikiano wa nguvu wa kila Mwanasimba.

“Tumejiandaa siku hiyo kila Mwanasimba atakayekuja uwanjani aondoke na furaha. Tumedhamiria msimu huu kila anayekuja lazima tumfunge. Kwahiyo ndugu zangu Wanasimba jukumu letu la msingi ni kwenda uwanjani na ukienda uwanjani usitulie, unafanya balaa unaloweza.

HUYU HAPA MGENI RASMI

Ahmed
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba. Source: Simba.

Kwenye mechi za kimataifa Simba wamekuwa na utaratibu wa kumtaja mgeni rasmi kutokana na mwendo ulivyo. Kumbuka kwamba kwa Yanga mchezo wa kimataifa unakwenda kwa jina la Dube Day ikiwa ni heshima kwa nyota wao Prince Dube ambaye ni mshambuliaji.

Kwa upande wa Simba mgeni rasmi katika mchezo  dhidi ya Bravos atakuwa ni Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally ambaye alijitangaza yeye mwenyewe kuwa atakuwa mgeni rasmi kwenye mchezo huo.

“Mgeni rasmi kwenye mchezo wetu dhidi ya Bravos atakuwa ni Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally, mgeni rasmi nitakuwa mimi mwenyewe.”

HUYU HAPA KUANZA LANGONI

Camara Air
Camara Air kipa namba moja wa Simba 2024/25. Source: Simba.

Kuna uwezekano mkubwa kimataifa langoni akaanza kipa namba moja Mousa Camara ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids akiwa kakaa langoni kwenye mech izote 11 za ligi.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa 11 wa NBC Premier League kwa Camara kuanza kikosi cha kwanza ilikuwa dhidi ya Pamba Novemba 22 2024 na benchi alikuwepo Ally Salim ambaye hajapata nafasi ya kucheza msimu wa 2024/25 kwenye ligi.

MKALI WA MABAO HUYU HAPA

Ahoua
Kiungo mshambuliaji wa Simba Jean Ahoua mwenye mabao matano ndani ya ligi 2024/25. Source: Simba.

Mkali wa kucheka na nyavu Jean Ahoua yupo na alianza kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji Novemba 22 2024 na aliingia kwenye orodha ya wachezaji waliopoteza pasi nyingi katika dakika 45 ambazo alicheza hivyo ana kazi kubwa ya kufanya kimataifa.

Kwenye mchezo huo hakuwa katika utulivu mchezaji wa matukio muhimu lakini katika ukabaji bado hakuwa huenda hakuwa na siku nzuri kazini mbele ya Pamba Jiji. Miongoni mwa dakika ambazo alipoteza pasi kwenye mchezo huo ilikuwa dakika ya 15, 16, 30, 32, 33, 44.

Rekodi zinaonyesha huyu ni namba moja kwa utupiaji akiwa na mabao matano ndani ya kikosi cha Simba na pasi nne za mabao. Kahusika kwenye mabao 9 kati ya 22 yaliyofungwa na timu hiyo.

 

Share this: