Yanga SC vs Al Hilal CAF Champion League | Taarifa kuhusu wachezaji | SportPesa Blog

ByLunyamadizo Mlyuka

November 25, 2024
Dube kimataifaDube kimataifaDube kimataifa

Yanga SC vs Al Hilal ya Sudan ni mchezo ujao CAF Champions League. Wababe hawa wawili wanatarajiwa kukutana Novemba 26, 2024 Uwanja wa Mkapa. Mchezo huo ni hatua ya makundi unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Kamwe Ali
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga itakayokuwa kazini kimataifa Novemba 26 2024 dhidi ya Al Hilal, Uwanja wa Mkapa. Source: Yanga.

Ikumbukwe kwamba Yanga SC inapeperusha bendera ya Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Timu hii inapewa nafasi kubwa kufanya vizuri. Hii inatokana na uwepo wa wachezaji wenye uzoefu mkubwa akiwemo Clatous Chama aliyekuwa Simba SC.

Mechi ya Yanga SC imepewa jina la Dube Day nyota ambaye ni mshambuliaji. Dube ni ingizo  jipya kwenye mechi za ligi msimu wa 2024/25 hajafunga bao licha ya kupata nafasi katika mechi hizo. Yanga SC ina kocha mpya mara baada ya kuachana na Miguel Gamondi.

Tayari Yanga SC imezindua jezi mpya kwa ajili ya mashindano hayo ya kimataifa ambazo zipo sokoni sasa wote walinzindua siku moja na mtani Simba ilikuwa ni Novemba 20 2024.

Taarifa kuhusu wachezaji wa Yanga SC

Prince Dube ni miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye mazezi ya mwisho kuelekea mchezo huo huku wakipewa matizi ya maana yatakayowapa matokeo mazuri kwenye mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Chama Clatous
Chama Clatous kiungo wa Yanga kwenye maandalizi ya mechi za kimataifa 2024/25. Source: Yanga.

Mbali na Dube, Clatous Chama kiungo mshambuliaji, Jean Baleke ambaye ni mshambuliaji, Aboutwalib Mshery na Djigui Diarra hawa ni makipa nao wapo kwenye orodha ya nyota wa Yanga SC wanaoendelea na mazoezi.

Alichokisema Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC kuelekea mchezo

Kocha mpya Yanga
Sead Ramovic, Kocha Mkuu wa Yanga 2024/25 akiwa na Aziz Ki kwenye uwanja wa mazoezi. Source: Yanga.

“Jumanne ni siku ambayo Tanzania yote itatulia na kuufatilia mchezo wetu dhidi ya Al Hilal, kocha wetu ‘German Machine’ Sead Ramovic ametambulisha soka linaloitwa ‘GUSA ACHIA TWENDE KWAO’ baada ya kutazama hili soka mazoezini nikaona kabisa Wananchi tunakwenda kupata raha siku ya Jumanne.

“Niwaombe msiwe watu wa kuikosa furaha hii, tukate tiketi muda huu tukutane Benjamin Mkapa kufurahi. “Tunafahamu kuwa mchezo wetu dhidi ya Al Hilal utakuwa mgumu lakini kwa umoja wetu, kwa wingi wetu, kwa hamasa tutakayowapa wachezaji wetu, mchezo huu utakuwa mwepesi na tutashinda.

“Wachezaji wetu wapo tayari, Bechi la Ufundi lipo tayari na viongozi wetu wapo tayari, kazi iliyobaki ni kwetu sisi Wananchi, jukumu letu ni kuwasapoti wachezaji wetu, basi tukate tiketi kwa wingi na twende kwa wingi kuishangilia Yanga.

“Siku ya mchezo natamani kumuona kila Mwananchi akiwa uwanjani kuwapa hamasa wachezaji wetu. Safari hii tumepata mwalimu anayependa shangwe la mashabiki.Yeye anatamani kuwaona siku hiyo mashabiki. Niwaombe tu Wananchi Wenzangu, tukate tiketi mapema tusisubiri siku ya mechi ifike hapo tuanze kuwa kwenye mahangaiko hapana tuanze maandalizi mapema.

“Safari hii hatutamani kabisa zile hesabu za kuomba fulani afungwe ili tufuzu, mnakumbuka msimu uliopita hatukuanza vizuri mechi yetu ya kwanza kule Algeria. Niwambie Wanayanga wote safari hii tunapaswa kuchukua pointi 3 kwenye mechi zote za nyumbani, hivyo basi tunawahitaji sana uwanjani siku hiyo.

“Sisi tunamtazama kwa sasa Al Hilal kwa jicho la roho mbaya tu. Hatuna msalie mtume siku ya Jumanne, hatukumalizana naye vizuri kwahiyo tuna kisasi naye na mechi zetu mbili za mwisho za ligi ndiyo zinampa wakati mgumu Al Hilal.

Maneno ya kocha mpya Yanga SC

SEAD
Kocha Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic 2024/25 mrithi wa mikoba ya Miguel Gamondi. Source: Yanga.

Kocha mpya wa Yanga SC, Sead Ramovic ambaye ametambulisha aina mpya ya soka inayokwenda kwa jina la gusa achia ameweka wazi kuwa wanatambua watakuwa na kazi ngumu kwenye mchezo wao wa kimataifa kwa kuwa bado hajaunda kikosi kazi vizuri.

“Unajua mimi nipo hapa na siku ambazo nimeanza nazo huwezi kusema ni nyingi kwani hata ukiwa unakwenda kufanya mazoezi ya kujenga mwili hautafanikiwa kubadilika ndani ya siku sita, ipo wazi unahitaji muda kuwa bora.

“Kwa namna ambavyo tumeanza hatupo vibaya nina amini tunakwenda kufanya vizuri na tutazidi kuimarika kadri ambavyo siku zinakwenda, wachezaji wapo vizuri na wanapenda kuona timu inapata matokeo tuna amini kwamba tutapambana ili kuwa imara kwenye mechi zetu zote.”

Share this: