Jean Ahoua --Jean Ahoua --

MKALI wa kucheka na nyavu ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids msimu wa 2024/25 ni Jean Ahoua ambaye ni chaguo la kwanza katika kikosi hicho upande wa viungo washambuliaji.

 

Ahoua kwenye mchezo uliopita dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex aliibuka mchezaji bora hiyo ni baada ya kufunga jumla ya mabao mawili na alicheza katika kiwango bora mwanzo mwisho ndani ya uwanja walipokomba pointi tatu mazima.

 

Miguel Gamondi
Miguel Gamondi Kocha Mkuu wa Yanga, 2024/25. Source: Yanga.

Ni Yanga inayodhaminiwa na SportPesa hawa ni mabingwa watetezi kwenye msimamo wa ligi wapo nafasi ya pili na pointi 24 baada ya kucheza mechi 10 na kinara wa utupiaji kutoka kikosi cha Yanga ni Maxi Nzengeli ambaye amefunga jumla ya mabao matatu.

 

Ahmed Ally
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba 2024/25. Source: Simba.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa kiwango ambacho anaonyesha kiungo Ahoua bado hakijafikia hata asilimia 50 kwa kuwa bado anazidi kuimarika kadri anavyopata nafasi ya kucheza mechi za ushindani.

 

“Kuna mchezaji wa mpira kiungo wetu Ahoua huyu ana balaa akiwa uwanjani na balaa lote ambalo unaona anaonyesha uwanjani bado hajafikia asilimia hata 20 ya uwezo wake unadhani akifikia asilimi hata 50 itakuwa kwenye kiwango cha aina gani hapo?

 

“Ni moja ya wachezaji ambao wana vipaji na Simba tulimtafuta kwa kuzingatia vigezo, bado hajachanganya na amekuja kucheza hapa akionyesha kiwango cha hali ya juu hili ni jambo la kujivunia Wanasimba wote.”

 

REKODI ZA AHOUA

Ahoua
Ahoua nyota wa Simba ambaye anatumia jezi namba 10 uwanjani 2024/25.Source: Simba.

Rekodi zinaonyesha kuwa Ahoua kafunga mabao matano ndani ya ligi baada ya Simba kucheza jumla ya mechi 10 ambapo timu hiyo imefunga jumla ya mabao 21 ikiwa ni namba moja kwa timu zenye mabao mengi Bongo.

 

Timu namba mbili kwa kufunga mabao mengi ndani ya ligi ni Fountain Gate na inadhaminiwa na SportPesa. Fountain Gate baada ya mechi 11 ni mabao 20 imefunga ikiwa nafasi ya 5 na pointi 17 kibindoni.

 

Mbali na kuwa namba mbili, nyota anayeongoza kwa kutupia mabao mengi ndani ya ligi ni Suleiman Mwalimu huyu yupo ndani ya Fountain Gate akiwa ametupia jumla ya mabao sita msimu wa 2024/25.

 

TIMU AMBAZO AMEZIFUNGA AHOUA

Fountain Gate alifunga bao moja ilikuwa dakika ya 59, Dodoma Jiji aliwafunga bao moja ilikuwa dakika ya 63 kwa mkwaju wa penalti, Namungo aliwafunga bao moja dakika ya 33 na alifunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya KMC ilikuwa dakika ya 38 na dakika ya 69.

Katika mabao hayo matano kafunga mabao mawili kwa mkwaju wa penati aliwafunga Dodoma Jiji na KMC huku akiwa ametoa pasi nne za mabao akihusika kwenye mabao 9 kati ya 21 msimu wa 2024/25.

PASI ZA MABAO ZA AHOUA

 

CHE Malone
Beki Che Malone wa Simba anashikilia rekodi ya kuwa nyota wa kwanza kufunga bao ndani ya kikosi hicho msimu wa 2024/25. Source: Yanga.

Pasi yake ya kwanza ya bao alimpa Che Malone ambaye ni mfungaji wa bao la kwanza ndani ya ligi ilikuwa dhidi ya Tabora United dakika ya 13, alitoa pasi mbili kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate dakika ya 13 alimpa Balua na dakika ya 80 alimpa Valentino Mashaka.

Ahoua anaingia kwenye rekodi ya kuwa nyota wa kwanza kutoa pasi ya bao ndani ya kikosi hicho msimu wa 2024/25 kwenye mechi za ligi ndani ya uwanja akiwa na uzi wa Simba na anavaa jezi namba 10 mgongoni.

Pasi moja alitoa kwenye mchezo dhidi ya matajiri wa Dar, Azam FC alimpa Ateba walipokomba pointi tatu mazima ugenini kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa huku Leonel Ateba akifunga bao lake la kwanza akiwa na uzi wa Simba kwenye mechi za ligi.

 

NENO LA AHOUA HILI HAPA

Kiungo huyo amesema kuwa furaha yake ni kuona timu inapata matokeo kwenye mechi za ushindani ambazo wanacheza kwa kuwa wanachohitaji ni ushindi huku akifurahia kutwaa tuzo kwenye baadhi ya mechi ambazo alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.

 

Kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate na KMC nyota huyo alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo baada ya dakika 90 na mech izote hizo zilichezwa Uwanja wa KMC, Complex.

“Furaha kubwa ni kuona timu inapata matokeo kwani kikubwa ni ushindi kwenye mechi zetu, bado tuna nafasi ya kufanya vizuri na tutaendelea kushirikiana zaidi, tuzo ambazo ninapata sio kwa ajili yangu bali nit imu kiujumla.”

Share this: