Fei v YangaFei v Yanga

MATAJIRI wa Dar, Azam FC wamebainisha kuwa kupoteza mchezo wao wa fainali ya Ngao ya Jamii mbele ya Yanga Agosti 11 2024 haina maana kwamba wao sio bora kwenye mashindano hivyo wasichukuliwe poa kwa kuwa watafanya makubwa kwenye mechi zao za ushindani.

Timu hiyo inanolewa na Kocha Mkuu, Yusuph Dabo iligotea nafasi ya pili kwenye Ngao ya Jamii 2024/25 huku ikishuhudia mabingwa wapya kuwa Yanga inayodhaminiwa na SportPesa.

MATAJIRI
MATAJIRI wa Day, Azam FC fainali yao ilikuwa dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa. Source: Yanga.

Katika mchezo wa nusu fainali Azam FC iliibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Coastal Union ya Tanga mchezo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar waliporejea Bongo wakapoteza mbele ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

MATAJIRI MWENDO WAO

MATAJIRI
MATAJIRI wa Dar wakishangilia moja ya bao kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Coastal Union. Source: Azam FC.

Matajiri hao walianza kwa ushindi mbele ya Coastal Union ilikuwa ni Agosti 8 kwenye mchezo huo walitembeza mkono kwa mpinzani wao ambaye aligotea nafasi ya nne kwenye Ngao ya Jamii 2024/25.

Katika mchezo huo nyota Feisal Salum, Gibril Silla, Blanco, Adam Adam na Meza hawa wote walitupia bao mojamoja kweye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Kiungo Feisal aliweka wazi kuwa wapo tayari kucheza na timu yoyote kati ya Simba ama Yanga itakayotinga fainali kwa kuwa wao walianza kufunga safari ya kutinga fainali na mwisho walikutana na Yanga.

Yanga ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba kwenye nusu fainali ya pili iliyochezwa Uwanja wa Mkapa na bao likifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 44 akitumia pasi ya Prince Dube.

Fei alisema: “Kwetu sisi kikubwa ni kuona kwamba tunacheza fainali na timu yoyote ile tupo tayari kucheza nayo,wa watamalizana wenyewe na sisi tunamalizana na wapinzani wetu kwanza kisha tutakutana fainali.”

MATAJIRI KWENYE FAINALI  

DABO
MPANGA mipango ndani ya matajiri wa Dar, kocha Yusuph Dabo. Source: Azam FC.

Agosti 11 ilikuwa ni fainali na matajiri hao walikutana na Yanga katika mchezo uliochezwa saa 1:00 usiku na kila timu ilikuwa tayari kwa kazi kutwaa taji la kwanza ambalo msimu wa 2023/24 lilikuwa mikononi mwa Simba.

Kwenye mchezo huo Azam FC ilianza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Feisal Salum ambaye aliwahi kucheza Yanga ilikuwa mapema dakika ya 13 liliwekwa usawa na mshambuliaji Prince Dube na mwisho wakapoteza taji la Ngao ya Jamii.

Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa wanatambua ulikuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa kwa timu zote licha ya kuwa bora walipoteza lakini wasichukuliwe poa na wapinzani wao.

“Wapinzani wetu wasituchukulie poa wanaona kwamba tumefungwa mabao manne kwenye mchezo wetu wa fainali wasiamini kwamba wanaweza kutufunga nao pia mabao hayo kwani yale yalikuwa ni makosa na tumepoteza licha ya kwamba tulikuwa bora.

“Wapinzani wetu ambao wametuangalia wasifikirie kwamba huu ni uwezo wetu na wao wanatumudu kwa kutufunga kwenye mechi ambazo tutacheza hapana. Tupo imara na tulikuwa bora kuliko wapinzani wetu lakini tumepoteza tutarejea tukiwa imara.”

KOCHA HUYU HAPA WA MATAJIRI

Yusuph Dabo, Kocha wa Azam FC amebainisha kuwa walikuwa na mpango wa kupata ushindi kwenye mchezo huo mwisho walishindwa kutokana na makosa ambayo walifanya hivyo watafanyia kazi kwenye eneo la mazoezi.

“Ulikuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa na kila mmoja aliona namna ambavyo tulianza na mpango ulifanikiwa mwanzo kwa kupata bao la mapema. Mwisho tukashindwa kuhimili mwendo ule na kukosa matokeo.

“Tulijitahidi kubadili mbinu kutokana na aina ya wapinzani wetu haikuwa hivyo kwani walitumia makosa yetu kutuadhibu na wana aina ya wachezaji ambao walikuwa kwenye ubora jambo ambalo lilitupa ugumu kwetu.

“Mchezaji kama Djigui Diarra ambaye alikuwa langoni alikuwa makini kwenye kutimiza majukumu yake na wachezaji walijitahidi kufanya kazi yao mwisho tukashindwa kupata ushindi, haya ni matokeo na tuna amini kwamba tutafanyia kazi makosa ambayo yametokea kwenye mchezo wetu.”

MASTA GAMONDI AFICHUA SIRI

 

MIGUEL
MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga, mabingwa Ngao ya Jamii 2024/25. Source: Yanga.

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa ilikuwa kazi ngumu kwenye mchezo wetu kwa kuwa tulifungwa mapema lakini niliwaambia wachezaji wasiwe na presha watulie kwani mchezo wa mpira ni mpaka mwisho.

“Tulifungwa mapema nikawaambia wachezaji watulie na tukafanikiwa kupata matokeo kwenye mchezo wetu uliokuwa na ushindani mkubwa. Ninawapongeza wachezaji kwa kuanza na Ngao ya Jamii kwenye msimu mpya, tupo tayari kwa ushindani na tunaamini kwamba tutaendelea kufanya vizuri.”

 

 

Share this: