Yanga Vs Simba - Uwanja wa MkapaYanga Vs Simba - Uwanja wa Mkapa
YANGA
Kiungo, Pacome Zouzoua akipambana na wachezaji wa Simba

HATIMAYE baada ya kelele za muda mrefu, na tambo za watani wa jadi Simba na Yanga kuuelekea mchezo wao wa Kariakoo ya Ngao ya Jamii zilimalizwa rasmi Alhamisi ya wiki hii.

Hii ni baada ya miamba hiyo miwili kushuka kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam katika mchezo ambao ulimalizika kwa Yanga ambao wanadhaminiwa na Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kupata matokeo ya suhindi wa bao 1-0.

Bao pekee la Yanga katika mchezo huo lilifungwa na kiungo, Maxi Nzengeli aliyetumia vizuri asisti ya straika, Prince Dube mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya Yanga kugongeana vizuri pasi fupifupi kwa haraka.

Kila mmoja amekuwa sehemu ya ushuhuda wa kilichotokea na kwa sasa ukipita pale kwenye mitaa ya Kariakoo Dar es Salaam basi kila upande unaendelea kubishana kutokana na matokeo ya mchezo huo. Vijembe na utani wa hapa na pale, ilimradi kusherehekea ladha ya ushindi na raha ya soka kwa ujumla.

Kimsingi utani na kebehi hizi ndizo ambazo zinaufanya mchezo huu kuwa miongoni mwa michezo mitano bora ya dabi kwenye ardhi ya Bara hili kubwa na lenye historia yake la Afrika.

Hii ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana msimu huu wa 20224/25. Lakini mchezo huu unakuwa wa tatu mfululizo kwa Yanga kuibuka na ushindi dhidi ya Simba kwenye Kariakoo Dabi.

NAMNA MCHEZO ULIVYOKUWA

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote mbili zikishambuliana kwa zamu, lakini kulikosekana umakini wa kutumia nafasi chache zilizotengenezwa katika dakika 30 za mwanzo.

Maxi Nzengeli aliipatia Yanga bao pekee la mchezo huo dakika ya 43 kwa shuti kali la mguu wa kushoto, baada ya kupokea pasi ya Prince Dube.

Kipindi cha pili Simba ambao pia wamewahi kudhaminiwa na SportPesa walirudi kwa kasi na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Yanga na kutengeneza nafasi lakini hata hivyo hawakuweza kuzitumia.

Pamoja na mashambulizi ya pande zote lakini hata hivyo hakuna kilichoweza kubadili matokeo mpaka dakika 90 zinakamilika.

NINI KINAFUATA?

Kufuatia matokeo hayo Simba sasa watakutana na Coastal Union katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu utakaopigwa Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa saa tisa alasiri, huku Yanga wao wakikutana na Azam FC katika mchezo wa fainali utakaopigwa usiku.

VIKOSI VILIVYOKUTANA KWENYE MCHEZO HUO

Simba

Camara, Kapombe (Kijili 78′), Zimbwe Jr, Che Malone, Chamou, Mzamiru (Okajepha 45′), Balua (Freddy 79′), Fernandes (Ngoma 70′), Mukwala (Kibu 70′), Ahoua, Mutale

Yanga

Diarra, Yao, Boka, Bacca, Job, Aucho, Abuya (Mudathir 66′), Nzengeli (Mwamnyeto 87′), Dube ( Mzize45′), Aziz Ki (Chama 81′), Pacome (Musonda 87′)

YANGA WANASEMAJE?

YANGA
Ally Kamwe

Baada ya ushindi huo Ofisa habari wa Yanga akiwa Tshirt yake ya SportPesa, Ally Kamwe amesema: “Tulikuwa na nafasi ya kupata matokeo mazuri zaidi ya mabao mengi dhidi ya Simba, lakini maamuzi ya waamuzi waliosimamia mchezo ni kama yaliwasaidia Simba kuepuka kipigo kikubwa.

“Sisi kama Yanga tumeridhishwa na ubnora wa kikosi chetu nah ii inaonyesha tumedhamiria kufanya nini msimu huu, sasa huu ni ujumbe kwa Azam FC kuwa Jumapili wanapaswa kujipanga kwa dozi nzito, tunafahamu ubora wa kikosi chao na tumejipanga kuhakikisha tunashinda ubingwa huu.”

SIMBA NAO WANASEMAJE?

YANGA
Ahmed Ally

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally akizungumzia kipigo hicho kutoka kwa Yanga amesema: “Asante Mungu, ni matokeo mabaya lakini yenye kutupa maono wapi tunaelekea kwenye ujenzi wa kikosi chetu bora msimu huu.

“Tunakila sababu ya kujivunia maendeleo ya ‘Project’ yetu ya muda mrefu iliyohusisha wachezaji wengi wapya, wenye vipaji vikubwa na umri mdogo. Wanasimba matokeo yasiwatie unyonge kwani tupo katika njia sahihi sana na punde tutaanza kuogelea kwenye mito ya asali na maziwa.

“Hii ni tofauti na msimu uliopita tulichukua ngao ya jamii lakini hatukua na timu imara ndio maana tulikosa Mataji yote, Msimu huu tumekosa Ngao ya Jamii lakini tunayo timu imara ya kutupa heshima hapo baadae. Ubaya UbwelMchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii utapigwa siku ya Jumapili sambamba na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu ambao unatarajiwa kuwa mchezo wa utangulizi siku hiyo ukipigwa majira ya mchana.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.