Awesu AwesuAwesu Awesu
CHAMOE
INGIZO jipya 2024/25 ndani ya Simba Chamoe. Source: Simba.

TAMBO hizi Simba lazima ukaei ikiwa zimeanza kutembea kuelekea msimu mpya wa 2024/25 unaotarajiwa kuanza Agosti 16 2024. Ipo wazi kuwa mabingwa wa ligi  msimu wa 2023/24 ni Yanga inayodhaminiwa na SportPesa walimaliza msimu wakiwa na pointi 80 kibindoni wana kazi ya kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba inayonolewa na Fadlu Davids aliyetambulishwa rasmi Julai 5 yenyewe iligotea nafasi ya tatu ina kazi ya kufanya kwenye anga la kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika. Timu hiyo ipo kambini Misri kwa maandalizi ya msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

TAMBO ZA KOCHA MPYA

Kocha mpya wa Simba amebainisha kuwa kazi kubwa inayofanyika kwa sasa ni kuhakikisha wachezaji wanakuwa na mafikirio ya kupata ushindi kwenye mechi zao jambo ambalo litawapa nguvu ya kupambana bila kuchoka ndani ya uwanja katika kusaka matokeo mazuri uwanjani.

“Ambacho kinafanyika kwa sasa ni kuhakikisha kwamba wachezaji wanakuwa na mafikirio zaidi kuhusu ushindi hili litawafanya wajijenge kwa umakini katika mlengo tofauti. Ninaona namna ambavyo wanafanya kile ambacho tunaelekezana hii inatoa picha kwamba wanazidi kuwa kwenye ari kubwa zaidi kwa muda ambao tunapeana maelekezo.”

TAMBO ZA SEMAJI BALAA

 

KIMATAIFA
SEMAJI la Simba, Ahmed Ally ameweka wazi 2024/25 itakuwa na ushindani mkubwa. Source: Simba.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba kuelekea kwenye Simba Day ambayo imepewa kauli mbiu ya Ubaya Ubwela ameweka wazi kuwa wana wachezaji wa kazi wenye umri mdogo utakaowapa ruhusa kucheza muda mrefu bila kuchoka wala kuomba maji kwa kuwa sio wazee.

“Wachezaji tulionao ni wachezaji sahihi wana uwezo mkubwa na wote ni vijana. Wengi ni miaka kuanzia 21 hivi wapo ndani ya kikosi. Hapo unaona namna gani uwezo upo na nguvu huu ni muda sahihi kwao kucheza.Wanaweza kucheza kwa muda mrefu bila kuomba maji. Agosti 3 2024 Simba Day tujitokeze kwa wingi.

“Simba Day inaingia kwenye orodha ya matamasha makubwa duniani yanayopendwa na kufuatiliwa kwa ukaribu. Hivyo hili ni tukio kubwa na la historia mashabiki popote mlipo mjitokeze kwa wingi kwenye hili jambo.”

RATIBA YA NGAO YA JAMII HADHARANI

Tayari Simba wanatambua kwamba wakimaliza kazi kwenye Simba Day watakuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga. Itakuwa ni hatua ya nusu fainali Ngao ya Jamii inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Agosti 8 2024.

Ipo wazi kwamba waliotwaa taji la Ngao ya Jamii 2023/24 ni Simba chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kwenye fainali iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Ushindi wa Simba ilikuwa kupitia penalti baada ya kutoshana nguvu kwenye muda wa kawaida.

Mbali na Simba kumenyana na Yanga, Azam FC iliyogotea nafasi ya pili kwenye msimamo ina kibarua cha kusaka tiketi ya kutinga fainali itakuwa dhidi ya Coastal Union ya Tanga, mchezo huu utachezwa Zanzibar. Mshindi wa mchezo wa nusu fainali atakuwa na kibarua cha kucheza mchezo wa fainali inayotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

MASHINE MPYA SIMBA

Mtu wa kazi Valentino Mashaka ambaye ni kiungo mshambuliaji alikuwa Geita Gold alitambulishwa kuwa ni Mnyama hivyo kibarua chake kitakuwa kwenye changamoto mpya. Alitambulishwa Julai 5 2024.

Rekodi zinaonyesha kuwa alicheza jumla ya mechi 24 za ushindani ndani ya ligi na alifunga mabao sita akitoa pasi moja ya bao. Ikumbukwe kwamba Geita Gold itashiriki Championship msimu wa 2024/25 baada ya kushuka daraja.

LAWI

Lameck Lawi yeye ni beki anaingia kwenye orodha ya nyota wa kwanza kutambulishwa katika kikosi cha Simba akitokea Coastal Union. Lawi alitambulishwa Juni 20 2024. Usajili wake umekuwa na mvutano mkubwa kutokana na Coastal Union kueleza kuwa mchezaji huyo ni wao hivyo bado hajajiunga na kambi ya Simba Misri mpaka sakata lake litakapopata muafaka.

MUTALE

Joshua Mutale alitambulishwa ndani ya kikosi cha Simba Julai Mosi 2024. Nyota huyo amebainisha kwamba yupo hapo kwa ajili ya kazi.

MUKWALA

Steven Mukwala ni nyota mpya ndani ya kikosi cha Simba alitambulishwa Julai 2 2024 kuwa ndani ya kikosi hicho ambacho kitashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

JEAN

Ingizo jingine jipya ndani ya Simba ni Ahoua Jean Charles ambaye alitambulishwa Julai 3 2024.

HAMZA

Nyota mwingine mpya ndani ya kikosi cha Simba ni Abdulrazack Mohamed Hamza alitambulishwa rasmi Julai 4 2024 kuwa ni nyekundu na nyeupe.

KAGOMA

Yusuph Kagoma kiungo aliyekuwa ndani ya Singida Fountain Gate alitambulishwa ndani ya Simba kuwa ingizo jipya ilikuwa ni Julai 8 2024.

CHAMOU

Raia huyu wa Ivory Coast yeye ni beki anaitwa Karaboue Chamou alitambulishwa ndani ya kikosi Julai 7 2024. Wanamuita mashine ya zege kutokana na uimara wake kwenye eneo hilo la ulinzi mkataba wa miaka miwili.

NOUMA

Beki mwingine ni raia wa Burkina Faso anaitwa Valentin Nouma alitambulishwa ndani ya Simba Julai 7 2024 kwa ajili ya changamoto mpya kwenye kikosi hicho

FERNANDES

Kiungo Debora Fernandes Mavambo mwenye uwezo wa kuchezesha timu akiwa na mpira ni ingizo jipya ndani ya Simba kuelekea msimu mpya wa 2024/25. . Ni Julai 6 2024 alitambulishwa kuwa ndani ya Simba kwa kandarasi ya miaka miwili.

OMARY

Omary Abdalha huyu ni kiraka alitambulishwa ndani ya kikosi cha Simba rasmi Julai 6 akitokea Mashujaa FC. Nyota huyo mwenye miaka 19 ana uwezo wa kucheza namba 10, 8, 9, 6 kwa umakini na ana sifa ya kuwa na spidi uwanjani.

KIJILI

Kelvin Kijili alitambulishwa rasmi ndani ya Simba Julai 12 2024 yeye ni beki. Tayari yupo kambini nchini Misri kwa maandalizi ya msimu ujao.

AWESU

Awesu
Awesu Awesu kiungo mpya wa Simba 2024/25. Source: Simba.

Julai 17 2024 ni kiungo mshambuliaji Awesu Awesu aliyekuwa anacheza KMC alitambulishwa ndani ya Simba kwa dili la miaka miwili. Ikumbukwe kwamba nyota huyo aliwahi kucheza Kagera Sugar, Azam FC kwa nyakati tofauti.

Share this: