
UNYONGE haupo kwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara Yanga inayodhaminiwa na SportPesa kutokana na kupanga kufanya usajili mkubwa ambao utakuwa na matokeo chanya kwa mechi za kitaifa na kimataifa.
Ikumbukwe kwamba Yanga ni mabingwa wa ligi msimu wa 2023/24 wakiwa na pointi 80 baada ya kucheza mechi 30.Nyota wao namba moja kwa utupiaji ni Aziz Ki anayevaa jezi namba 10 akiwa katupia mabao 21. Ki kwenye mabao hayo katupia mabao 17 kwa mguu wa kushoto.
Mabao matatu kafunga kwa mguu wa kulia na kafunga bao moja kwa pigo la kichwa ilikuwa Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo dhidi ya Tabora United alipofunga bao lake la 18 waliposepa na pointi tatu muhimu.
Nyota huyo wa Yanga mkataba wake uligota mwisho 2023/24 alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada ya timu mbalimbali Bongo na nje ya nchi mwisho kaongeza mkataba wa miaka miwili kusalia Jangwani.
Ikumbukwe kwamba kuna waliochana mikeka na wengi walikomba mkwanja mrefu kwa kubashiri kupitia SportPesa hata wewe unaweza kushinda hivyo cheza sasa na SportPesa ukunje mkwanja wako.
UNYONGE SPORTPESA HAKUNA

Wadhamini wakuu wa Yanga, kampuni ya SportPesa hawana dogo kutokana na kuwapa zawadi mabingwa wa ligi. Juni 5 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba aliwakabidhi Yanga mfano wa hundi Hundi wenye Thamani ya Tsh 537,500,000/= kama sehemu ya Bonus ya mafaniko ya msimu kwa Klabu.
Hundi hiyo alikabidhiwa Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ambaye alibainisha kuwa udhamini wa SportPesa umekuwa na manufaa makubwa kwa timu hiyo ambayo inafanya vizuri kwenye mechi za ushindani.
Ipo wazi kuwa 2023/24 ulikuwa ni msimu bora kwa Yanga walitinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika, walitwaa taji la CRDB Federation Cup na ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara. Watapeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2024/25.
KIUNGO MGHANA KUKUTANA NACHO

Wakati yote hayo yakitokea kwa timu kuwa kwenye mafanikio ndani ya msimu wa 2023/24 kuna nyota wanatajwa kwamba watapewa mkono wa asante kwa kushindwa kulishawishi benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi ndani ya msimu kwenye mechi alizopatata nafasi ya kucheza.
Ni Mghana Augustine Okrah inatajwa kwamba huenda mkataba wake ukavunjwa ama akatolewa kwa mkopo ndani au nje ya nchi ili akapate changamoto mpya kwa kuwa bado hajawa imara kwenye ligi ya Bongo.
Kiungo huyo alikuwepo katika kikosi cha Simba, katika msimu uliopita wa 2022/23 kabla ya kuomba mkataba wake uvunjwe ili akatafute changamoto nyingine mpya nyumbani kwao Ghana, kabla ya kurejea katika dirisha dogo msimu huu na alitambulishwa Zanzibar.
Mghana huyo alisajiliwa na Yanga, katika dirisha dogo ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho eneo la kiungo mshambuliaji kwenye mechi za ushindani.
JOYCE LOMALISA

Mwamba mwingine ambaye inatajwa kwamba ataondoka Yanga ni pamoja na Joyce Lomalisa beki wa kupanda na kushuka. Mchezo wake wa mwisho ilikuwa dhidi ya Azam FC ambao ulikuwa ni wa Kombe la CRDB Federation Cup.
Katika mchezo huo nyota huyo alianza kikosi cha kwanza alitimiza majukumu yake kwa umakini Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Ni miongoni mwa waliovaa medali za taji hilo kwa kuwa Yanga ilishinda kwa penalti 6-5 mbele ya Azam FC iliyokuwa inapewa nafasi kubwa kutwaa taji hilo.
Lomalisa anatajwa kuondoka akiwa anakwenda kupata changamoto mpya Ulaya. Kwenye ligi mchezo wake wa mwisho ilikuwa dhidi ya Tabora United uliochewa Uwanja wa Mkapa. Katika mchezo huo wa funga kazi alitoa pasi moja kwa Aziz Ki dakika ya 90 ikitajwa kuwa ilikuwa ni pasi yake ya mwisho.
Tayari Yanga wanalitambua hilo na wapo chimbo kusaka mbadala wake na inaelezwa kuwa watachukua nyota mwingine kutoka DR Congo kuja kubeba mikoba ya Lomalisa.
METACHA MNATA
Kipa wa mpira ambaye alirejea kwa mara nyingine ndani ya kikosi cha Yanga akitokea Singida Big Stars alikukuwa akitimiza majukumu yake.
Inaelezwa kuwa nyota huyo hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu wa 2024/25 kwa kuwa amepewa mkono wa asante hivyo atakuwa sehemu nyingine kutimiza majukumu yake inatajwa Ihefu kwa sasa. Yanga kipa wake namba moja ambaye wanaye kwa sasa ni Djigui Diara raia wa Mali.
MKUDE
Jonas Mkude kiungo mkabaji wa Yanga aliibuka hapo akitokea ndani ya kikosi cha Simba. Inaelezwa kuwa kandarasi yake ya mwaka mmoja imegota mwisho hivyo huenda akakutana na Thank You.
HUYU HAPA KAMWE
Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe ameweka wazi kuwa watafanya maboresho makubwa ndani ya timu hiyo kwa ajili ya kuendeleza ushindani kitaifa na kimataifa kwamsimu mpya ujao.
“Tunafanya maboresho kwenye timu ikumbukwe kwamba msimu uliopita tulikuwa na kikosi bora na msimu ujao tunahitaji kuwa na kikosi bora zaidi. Hakutakuwa na Thank You kwenye mitandao ya kijamii tutakuja na mpango kazi mwingine kabisa kwa wachezaji tutakaoachana nao.”

