-----------------------------------------------n-----------------------------------------------n
EURO 2024
Kane na Belingham wakishangilia

Timu ya Taifa ya England imefanikiwa kuandika rekodi ya kufika fainali 2 mfululizo za mashindano makubwa, baada ya usiku wa kuamkia leo Alhamisi kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Uholanzi katika mchezo wa Nusu Fainali ya mashindano ya Euro 2024 na kufanikiwa kutinga fainali.

Unaweza kubashiri mechi hizi za EURO 2024 na mashindano mbalimbali na Kampuni bora ya ubashiri ya SportPesa kwa kubonyeza www.sportpesa.co.tz

England ya kocha, Gareth Southgate ililazimika kufanya kazi ya ziada kusawazisha bao la kuongozwa ambalo lilifungwa na staa wa Uholanzi, Xavi Simons dakika za awali za mchezo huo.

Straika na nahodha wa England, Harry Kane aliisawazishia timu hiyo kwa mkwaju wa penalti, na kuufanya mchezo urudi kwenye usawazo. Kipindi cha pili England walirudi mchezoni licha ya kwamba walishindwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.

Dakika 9 tu, zilitosha kwa straika, Ollie Watkins akiingia kutokea benchi na kufanikiwa kuifungia England bao la ushindi. Staa huyo wa Aston Villa alifunga bao hilo akiwa ndani ya eneo la 18 baada ya kupiga shuti kali lililomshinda kipa wa Uholanzi.

EURO 2024 FAINALI NI ENGLAND Vs UHISPANIA

Baada ya ushindi huo uliowapa tiketi ya kutinga fainali ya mashindano ya Euro, England sasa wanatarajia kuvaana na Uhispania katika mchezo wa fainali utakaopigwa siku ya Jumapili wikiendi hii.

Mchezo huo ambao utapigwa jijini Berlin, utakuwa rekodi ya fainali ya pili mfululizo kwa England katika kampeni mbili mfululizo.

England wataingia katika fainali hiyo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza fainali ya kampeni iliyopita ya Euro baada ya kupoteza mbele ya timu ya Taifa ya Italy katika mchezo wa fainali uliopigwa katika ardhi yao ya nyumbani kwenye Uwanja wa Wembley.

Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ufaransa, kikosi cha Ufaransa tayari kimewasili jijini Berlin tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa fainali utakaopigwa Jumapili.

Hispania ndio kikosi ambacho kinatajwa kuwa bora zaidi katika mashindano ya mwaka huu, huku England ikitajwa kuwa miongoni mwa timu ziizojaza mastaa wengi wenye majina makubwa.

LAMINE YAMAL, NICO WILLIAM KIKWAZO KWA ENGLAND

EURO 2024
Lamine Yamal

Makinda wawili wa Uhispania, Lamine Yamal na Nico William wanatarajiwa kuwa kikwazo kikuwa kwa England kwenye mchezo huo wa fainali utakaopigwa siku ya Jumapili.

Yamal ambaye ana miaka 16 tu, kwa sasa amekuwa gumzo kwenye mashindano hayo kwani achana na bao kali alilofunga dhidi ya Ufaransa kwenye hatua ya Nusu Fainali, lakini pia ndiye kinara wa asisti kwenye mashindano hayo.

Nahodha wa England, Kane alibubujikwa na machozi baada ya filimbi ya mwisho na sasa ana nafasi moja zaidi ya kuipa England kombe kubwa ambapo amenukuliwa akisema bado hatua moja kufikia malengo yao.

Kane ameonekana kuwa na matumaini makubwa ya kushinda ubingwa huo baada ya kuukosa mbele ya Italy.

ALICHOSEMA KOCHA WA ENGLAND

Baada ya kukosolewa sana kufuatia mwanzo wa kusuasua wa England katika michuano ya Euro 2024, hatimaye Southgate amepata nafasi ya kuzungumza mara baada ya mchezo huo.

Southgate amenukuliwa akisema: “Natumai mashabiki watakuwa na nafasi ya kufurahi na angalau kupata bia kidogo. Tumekuwa na nyakati nyingi bora kwa miaka takribani saba au nane iliyopita. Mchezo huu umekuwa na umuhimu mkubwa hasa baada ya magoli ya dakika za mwisho.

“Sababu pekee nilikubali nafasi ya kuongoza timu hii ni kwa sababu nimetamani kuhakikisha naleta mafanikio ya soka kwenye nchi hii. Najivunia kuongoza timu hii kufika fainali ya mashindano haya ya EURO 2024 tena mbali na ardhi ya nyumbani.

“Tunajua haitakuwa kazi rahisi lakini tupo tayari kupambana.

Mainoo aiteka shoo

EURO
Kobbie Mainoo

Kiungo kinda wa ulinzi wa Manchester United, Kobbie Mainoo ameendelea kushangaza watu, huku akitajwa kuwa sababu kubwa ya ushindi wa England kwenda fainali.

Katika umri wa miaka 19, Kobbie anaelezewa kuwa na kiwango bora maradufu kuliko umri wake ambapo kiungo wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes alisema, Mainoo ni kiungo bora sana na hapaswi kulinganishwa naye.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.