SIMBA------------------------------------------------n
SIMBA
Benchi la ufundi la Simba

Uongozi wa Simba umethibitisha rasmi kuwa mchezo wao wa mzunguko wa 29, wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC unatarajiwa kupigwa Mei 25, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Kwenye mtanange huo Simba ndio wenyeji unatarajiwa kupigwa katika Uwanja huo saa 10 jioni, huku ukitarajiwa kuwa mchezo mgumu kutokana na ubora wa wapinzani.

Uongozi wa Simba ambao umewahi kudhaminiwa na Kampuni ya michezo ya Sportpesa umeweka wazi kuwa umeamua kuchagua Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kutokana na Viwanja vyao vya nyumbani tunavyotumia kuwa na ratiba nyingine.

MGUNDA NA MFULULIZO WA USHINDI

SIMBA
Mgunda na Chasambi

Simba wanaingia katika mchezo huu wakiwa na kumbukumbu nzuri ya matokeo ya ushindi mbele ya Geita Gold katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi ambao ulimalizika kwa Simba kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.

Katika mchezo huo Geita Gold ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa, Jofrey Julius dakika ya 11 baada ya mlinda mlango wa Simba, Hussein Abel kukosea kucheza vizuri mpira wa krosi uliopigwa na Edmund John.

Baada ya bao hilo Simba waliendelea kulishambulia lango la Geita na kutengeneza nafasi lakini walikosa umakini katika eneo la mwisho.

Saido Ntibazonkiza aliisawazisha bao hilo dakika ya pili ya nyongeza ya kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya, Shomari Kapombe kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Geita walimaliza mechi wakiwa pungufu kufuatia nahodha wao, Michael Onditi kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 68 baada ya kumfanyia madhambi Willy Onana.

Ntibazonkiza aliipatia bao la pili dakika ya 71 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja baada ya Onana kufanyiwa madhambi.

Dakika ya 85 kinda mpya wa Simba aliyesajiliwa kwenye dirisha dogo, Ladaki Chasambi aliipatia bao la tatu baada ya kumalizia pasi safi kutoka kwa Willy Onana.

Chasambi alipigilia msumari wa nne dakika ya 93 kwa shuti kali la mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18, baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mzamiru Yassin.

Kikosi cha Simba kilichoanza mchezo huo ni; Abel, Kapombe, Zimbwe Jr, Kennedy, Che Malone, Ngoma (Karabaka 80′), Balua (Onana 65′), Mzamiru, Jobe (Kanoute 65′), Ntibazonkiza, Chasambi.

ALICHOSEMA KOCHA JUMA MGUNDA

https://blog.sportpesa.co.tz/
Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda

Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo, Juma Mgunda amesema mara baada ya matokeo ya ushindi dhidi ya Geita Gold kikosi chao kimejipanga kukutana na mchezo mgumu dhidi ya KMC kutokana na ubora wa wapinzani wao, lakini wanaamini kuwa wachezaji wao watafuata maelekezo waliyowapatia na kufanikisha kuibuka na ushindi.

“Maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya KMC yanaendelea, tunafahamu utakuwa mchezo mgumu kutokana na ukweli kuwa Ligi inaelekea ukingoni, lakini tupo tayari kupambana ili kupata ushindi,” amesema Mgunda.

VITA YA NAFASI YA PILI
Simba wataingia bkatika mchezo huo dhidi ya KMC wakiwa na lengo moja kubwa ambalo ni kuhakikisha wanaibuka na ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kumaliza kwenye nafasi ya pili ili kusaka tiketi ya kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

CHAMA, MIQUISSONE WAONGEZA MZUKA
Nyota wawili wa Simba, Clatous Chama na Luis Miqussone wameendelea kushiriki mazoezi kamili pamoja na wenzao na uongozi wa timu hiyo umeweka wazi kuwa nyota hao wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.

Viungo hao washambuliaji wamekosa mechi kadhaa kutokana na kuwa majeruhi lakini sasa wako fiti na huenda benchi ufundi likawatumia.

LAKRED AFANYA MAZOEZI KAMILI NA TIMU

https://sportpesa.co.tz/SIMBA
Kipa wa Simba, Ayoub Lakred mazoezini

Baada ya kukosekana kwenye michezo miwili iliyopita, kutokana na maumivu mlinda mlango, Ayoub Lakred nae amerejea kikosini na amefanya mazoezi kamili na yupo tayari kwa mechi zijazo.

Lakred amekuwa na wakati mzuri tangu amejiunga na Simba ambapo kwa sasa anatajwa kuwa ndio mlinda mlango namba moja wa timu hiyo hasa kutokana na changamoto za majeraha ya mlinda mlango, Aishi Manula ambaye anaendelea kuuguza majeraha akionekana kuambana kuwa fiti tangu aliporejea kutoka kwenye matibabu ya nyonga nchini Afrika Kusini.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.