SIMBANgoma v Fei
https://sportpesa.co.tz/SIMBA
Aishi Manula

TAARIFA ambazo zimeripotiwa kutoka vyanzo mbalimbali zimethibitisha kuwa uongozi wa kikosi cha Azam FC umedhamiria kwa dhati kuibomoa Simba kwa mrudisha aliyekuwa kipa namba moja wa kikosi hicho, Aishi Manula baada tu, ya msimu huu kuisha.

Azam wanataka kumrudisha nyota huyo ambaye aliondoka ndani ya kikosi hicho Agosti 9, 2017 na kujiunga na Simba ambao walikuwa wakitamba na udhamini mnono wa Kampuni ya michezo ya SportPesa huku akiwa ni moja ya makipa bora nchini kutokana na kiwango chake anachokionyesha.

Manula ambaye Azam walimhitaji mapema mwanzoni tu, mwa msimu huu kujiunga na timu yake hiyo ya zamani ingawa dili hilo lilishindikana, huku ikielezwa kuwa Simba ilihitaji kubadilishana na kiungo nyota wa kikosi hicho, Sospeter Bajana jambo ambalo viongozi wa Azam hawakukubaliana nalo.

POKOU MIKONONI MWA SIMBA

SIMBA
Serge Pokou

Huku sarakasi za usajili wa Aishi Manula zikiendelea ndani ya AZAM, imeripotiwa kuwa uongozi wa Simba nao umeanza harakati za kuboresha kikosi chao huku wakitajwa kufukuzia saini ya kiungo mshambuliaji wa Asec Mimosas, Serge Pokou ambaye ameomba rasmi kuondoka ndani ya kikosi cha mabingwa hao wa Ivory Coast.

Fundi huyo anayetumia mguu wa kushoto aliwahi kuwa mwiba mkali baada ya kuifunga Simba hapa nchini, wakati timu hizo zilipokutana kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu ambapo timu hizo zilipangwa kwenye kundi B na Asec kumaliza nafasi ya kwanza huku Simba wakimaliza nafasi ya pili.

Akizungumzia dili hilo, Pokou amesema: “Nina ofa nyingi ikiwemo moja ya hapo Tanzania, lakini bado sijajua wapi nitakwenda ingawa napenda kuja kufanya kazi Tanzania, kuna marafiki zangu hapo wananiambia namna ligi ya huko ilivyo na ushindani.

“Nimewaomba viongozi wa klabu wasiniwekee ngumu kuondoka, nafahamu hii ni timu ambayo inapenda kuuza wachezaji wake Ulaya, napenda kwenda huko lakini nani anajua ni lini ofa kama hiyo itakuja?”

Wakati huohuo, kocha mkuu wa Asec Mimosa, Jullien Chevalier alisema kiungo huyo uamuzi wa kuondoka kwake unategemea na uongozi wa klabu yao endapo timu inayomtaka itawafuata kwa kuwa bado amesalia na mkataba wa mwaka mmoja.

CHASAMBI WAMEANZA KUMUELEWA SIMBA

https://blog.sportpesa.co.tz/https://sportpesa.co.tz/SIMBA
Kiungo, Ladack Chasambi

Licha ya kuanza kwa kusuasua tangu atue ndani ya kikosi cha Simba kwenye dirisha dogo la usajili, lakini balaa ambalo ameanza kulionyesha winga wa timu hiyo, Ladack Chasambi limeanza kuzaa matunda huku wadau mbalimbali wakikiri nyota huyo ni miongoni mwa mastaa ambao wana uwezo mkubwa.

Akizungumzia kiwango cha nyota huyo mchambuzi wa michezo, Edo Kumwembe amesema: “Nilikwenda uwanjani kutazama mechi ya Simba na Azam. Nilikutana na winga wa Simba anayeitwa, Ladack Chasambi. Naambiwa Simba walilipa pesa nyingi kupata huduma za kinda huyu ambaye kwa mujibu hati yake ya kusafiria ana miaka 20 tu.

“Awali niliambiwa ni winga mkali. Wakati ule akitokea Mtibwa Sugar kutua Simba. Baada ya kutua hapo nikaona kimya. Naambiwa kwamba kocha wa wakati huo, Abdelhak Benchikha hakuwa anampa nafasi kama ilivyotegemewa.

“Nilimwona Chasambi Alhamisi jioni katika pambano dhidi ya Azam, ana kitu. Kitu cha kwanza ni namna ambavyo anakokota kwa kujiamini mpira ukiwa katika miguu yake. Ana kasi lakini anajaribu kukokota kwa uhakika zaidi katika miguu yake.

“Sio kwamba anataka kuwaonyesha mashabiki kitu, hapana. Ndivyo alivyo. Kitu kingine ambacho kilisababisha nimpende zaidi ni namna anavyojaribu kucheza winga ya kisasa. Unakaa upande wa kushoto lakini unatumia mguu wa kulia. Ni kama ilivyo kwa kinda mwenzake, Edwin Balua ambaye alikaa upande wa kulia huku akitumia mguu wa kushoto.

“Sikuwa nawajua hapo awali sasa sijui kama walikuwa wanatumia staili hizo au wamekuja kubadilika hapo. Ninachojua ni kwamba Chasambi alinikosha zaidi. Unapotumia mguu wa kulia halafu unakaa upande wa kushoto kama kina, Gabriel Martinelli wanavyofanya ni kwamba unalazimika kuwa mpiga chenga mzuri, pia unalazimika kuwa mkatizaji mzuri kutoka katika winga yako na kuingia katikati.

“Lakini kuna jambo ambalo linamkabili Chasambi. Inabidi akomae kiakili mapema kwa nafasi chache ambazo ameanza kupewa. Inabidi awe ‘mjeuri’, mwenye kujiamini katika uwezo wake na kufanya maamuzi makubwa uwanjani. Mashabiki watamkubali tu. Nimeona ana kitu katika miguu yake. Asikubali kupotea kirahisi.”

 

 

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.