Vita ni kali-Job na Kiba

Ukuta wa Simba hauna bahati kwenye mechi zake umekimbizwa vibayavibaya

Yanga wana balaa zito uwanjani kila idara wapo fiti kukutana na matajiri wa Dar

Gamondi ametembeza mkwara wa maana huko 

VITA ni kali ndani ya 3 bora kwenye kila idara ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 huku mabeki wakiwa wanashindana kuhakikisha timu zao haziruhusu mabao huku ule ukuta wa Simba ukikimbizwa vibayavibaya.  

Kazi kubwa ni kukamilisha dakika 90 kwenye kuvuja jasho bila kufungwa lakini imekuwa ngumu kutokana na kila timu kufanya kweli katika kutumia nafasi ambazo zinatengenezwa uwanjani.

Kwa upande wa timu zilizopo ndani ya tatu bora, Yanga inayodhaminiwa na SportPesa, Azam FC na Simba mbali ya kuwa kwenye vita ya kuwania taji la ligi wanapambania kwenye rekodi za kutofungwa mabao mengi uwanjani.

UKUTA WA SIMBA

Che Malone, Henock Inonga, Kennedy Juma, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein hawa ni baadhi ya wachezaji chaguo la kwanza kwenye ukuta wa Simba ni mashuhuda wakiwa wametunguliwa jumla ya mabao 18.

Mabao yote hayo 18 ukuta huo umeruhusu ukiwa umecheza mechi 18 ndani ya ligi ambazo ni dakika 1,620 ina wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 90 kweye mechi za ligi.

DAKIKA 270 MATESO SIMBA

Kwenye mechi tatu mfululizo ambazo ni dakika 270 ilikuwa ni mateso kwenye safu ya ulinzi ya Simba ambalo ilikuwa inaruhusu mabao kwenye mechi hizo.

Ilikuwa Simba 1-2 Tanzania Prisons kwenye mchezo huu ilikosa kabisa pointi Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Coastal Union 1-2 Simba Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Simba 3-1 Singida Fountain Gate mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Kwenye mchezo huo Simba ilianza kufunga mapema kupitia kwa Saido Ntibanzokiza dakika ya 6 na 9 huku bao moja likufungwa na Michael Fred ilikuwa ni Machi 12 2024 bao la Singida Fountain Gate lilifungwa na Thomas Ulimwengu dakika ya 84.

BEKI ZIMBWE WA SIMBA KUHUSU UKUTA

MOHAMED Hussein
BEKI wa Simba Mohamed Hussein akiwa kwenye uwanja wa mazoezi pamoja na wachezaji wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mechi za ushindani. Soure: Simba

Mohamed Hussein Zimbwe Jr nahodha msaidizi wa Simba amesema kuwa makosa ambayo yanatokea kwenye safu ya ulinzi yatafanyiwa kazi na benchi la ufundi kwenye uwanja wa mazoezi.

Zimbwe ameweka wazi kuwa bado wapo imara kwenye kutimiza majukumu lakini makosa yanatokea jambo ambalo linawafanya wazungumze kwa pamoja wachezaji kuwa imara kwa mechi zinazofuata.

“Kwenye suala la mpira wa miguu makosa yapo lakini sisi bado tupo imara, makosa ambayo yametokea tunayafanyia kazi eneo la mazoezi kuwa bora na tunaamini itakuwa hivyo, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,’.

 

HAWA HAPA AZAM FC

Azam FC yenye Daniel Amoah baada ya kucheza jumla ya mechi 20 ukuta wake umeruhusu mabao 15 yakufungwa ikiwa na wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 102.

Kwa timu zilizo ndani ya tatu bora ikiwa na pointi zake 44 ni namba mbili kwa kufungwa mabao mengi kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ikiwa imetofautina pointi tano na vinara Yanga wenye pointi 49.

YANGA INA BALAA

Job na Kibabage
DICKSON Job beki wa Yanga mwenye jezi namba 5 akiwa na Kibabage miongoni mwa wanaounda safu ya ulinzi ya Yanga: Source: Yanga

Yanga wamekuwa imara kwenye upande wa ukuta ambao haujavuja sana baada ya kucheza mechi 18 ambazo ni dakika 1,620 ni mabao 9 pekee ukuta huo wenye nahodha Bakari Mwamnyeto na Dickson Job umeruhusu.

Wastani wa Yanga ni kuruhusu bao moja kila baada ya dakika 180 kwenye mechi za ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24.

MSIKIE GAMONDI MWENYEWE

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ni muhimu kuwa na mwendelezo mzuri hasa katika safu ya ulinzi kupunguza makosa na kutoruhusu kufungwa kwenye mechi za ushindani.

Kocha huyo amebainisha kwamba wamekuwa wakijeruhiwa wanapofungwa na wapinzani jambo ambalo huwa linaongeza ugumu kwenye kupata pointi hivyo ni muhimu kuongeza umakini maradufu kila wakati.

 “Kwenye upande wa ulinzi ni muhimu kutokuwa kwenye presha kubwa ya kufanya makosa na kuruhusu kufungwa kwa kuwa ikitokea hivyo inakuwa ni ngumu kwetu kupata pointi hasa kutokana na aina ya wapinzani tunaowakabili.

“Wachezaji wapo tayari na tunatambua kwamba kila mmoja anahitaji kuona timu inapata pointi tatu muhimu kwenye mechi zetu na kutokufanya makosa mara kwa mara hilo linawezekana.

“Makosa ambayo yanatokea kwenye mechi zetu huwa tunyafanyia kazi na kuhakikisha kwamba wakati ujao tunakuwa imara hivyo kazi bado inaendelea,”.

FEI TOTO
KIUNGO wa Azam FC Feisal Salum chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Yusuph Dabo akiwa kwenye furaha baada ya kufunga moja ya bao kwenye mechi za ushindani. Source: Azam FC

MZIZIMA DABI HII HAPA

Kituo kinachofuata kwa wababe ndani ya tatu bora ni Mzizima Dabi inayotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ambapo wenyeji wa mchezo watakuwa ni Azam FC.

Ikumbukwe kwamba awali mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex kutokana na ukubwa wa timu hizi mbili na matokeo wanayopata uwanjani ngoma ikahamishiwa Uwanja wa Mkapa.

Itakuwa ni Jumapili ya Machi 17 kwa wababe hao kuwa uwanjani kusaka pointi tatu, Ipo wazi kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza, Azam FC ilidondosha pointi tatu Uwanja wa Mkapa,

Share this: