
BAADA ya subira ya muda mrefu, hatimaye droo ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika imefanyika rasmi leo Jumanne kwenye makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), nchini Misri ambapo Yanga na Simba zimejua wapinzani wao.
Droo hii imefanyika mara baada ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kumemalizika kwa staili ya aina yake, ambapo Tanzania imekuwa Taifa pekee ambalo limefanikiwa kutoa timu mbili ambazo zimefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali.
Ni Simba ambao wamefuzu kutokea kundi B la mashindano hayo wakimaliza kwenye nafasi ya pili na pointi zao tisa ambazo wamekusanya katika michezo sita. Kutoka kwenye kundi lao ni wao na Asec Mimosas ya Ivory Coast ndio wamefuzu Robo Fainali.
Kwa upande wa Yanga ambao wanadhaminiwa na Kampuni ya SportPesa wao wamefuzu hatua ya Robo Fainali kutokea kundi D ambapo nao wamemaliza kama ‘Runner up’ yaani wamemaliza kwenye nafasi ya pili nyuma ya bingwa mtetezio Al Ahly.
TIMU 8 ZILIZOFUZU ROBO FAINALI

Timub hizi 8 zilitoka kwenye makundi manne ya Ligi ya Mabingwa msimu huu wa 2023/24. Kutoka kundi A ni Mamelodi Sundowns na TP Mazembe ndio waliofikia hatua hiyo.
Kutoka kundi B ni timu za Asec Mimosas na Simba ndio ambazo zimefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali, kutoka kundi C ni Petro Atletico na Esperance ndio zimefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali, huku kund D likishuhudia bingwa mtetezi Al Ahly na Yanga zikifuzu.
RASMI NI YANGA Vs MAMELODI, SIMBA Vs AL AHLY ROBO FAINALI

Upangaji wa droo za Robo Fainali Caf
Droo ya hatua ya Robo Fainali ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika zimefanyika leo Jumanne yaani Machi 12, mwaka huu ambapo kila timu imefanikiwa kujua ni tajua ni mpinzani gani wanakwenda kukutana naye katika hatua hiyo. Kwa upande wa wawakilishi wa Tanzania timu za Simba na Yanga wao pia wamejua watavaana na nani ambapo Simba watakutana na mabingwa watetezi Al Ahly, huku Yanga wao wakivaana na Mamelodi.
KANUNI ZIPI ZIMESIMAMIA DROO HII?
Zipo kanuni nyingi kuihusu namna ambavyo droo ya hatua hii inavyochezeshwa, lakini miongoni mwa mambo muhimu ni kuwa timu ambazo zimemaliza kwenye nafasi ya kwanza basi huwa haziwezi kukutana kwa kuwa zinakuwa kwenye ‘pot’ moja, kama ilivyo kwa zile zilizomaliza kwenye nafasi ya pili.
Hivyo timu zilizomaliza vinara wa hatua ya makundi hukutana na timu zilizomaliza nafasi ya pili, lakini pia timu ambazo zilikuwa kwenye kundi moja kwenye hatua ya makundi haziwezi kukutana kwenye hatua ya Robo Fainali.
TIMU NYINGINE AMBAZO ZINGEWEZA KUKUTANA NA YANGA, SIMBA

Kwa kuzingatia kanuni tajwa hapo juu wawakilishi wa Tanzania Yanga na Simba ukiachana na wapinzani waliopangwa kuvaana nao katika hatua hiyo ya Robo Fainali pia walikuwa kwenye nafasi kubwa ya kukutana na na wapinzani wafuatao;
Yanga
Wakiwa wametinga hatua hii kwa mara ya kwanza Yanga (kwa msaada mkubwa wa udhamini wa (SportPesa) walikuwa na nafasi kubwa pia ya kukutana na ASEC MIMOSAS na Petro Atletico.
Simba SC
Wazoefu wa hatua hii wakiwa wametinga kwa mara ya nne katika kipindi cha miaka mitano iliyopita achana na Al Ahly waliopangwa nao lakini pia walikuwa na nafasi kubwa ya kuvaana na Mamelodi Sundowns na Petro De Luanda.
EDO ATOA ONYO ZITO KWA YANGA, SIMBA ROBO FAINALI
Kufuatia droo hiyo mchambuzi wa habari za michezo, Edward Kumwembe amezipa onyo zito timu za Simba na Yanga ambapo amesema: “Hawa kina Al Ahly na Mamelodi sio watu wazuri sana katika hatua za robo fainali. Kwao inakuwa kama vile michuano ndio imeanza angalau Al Ahly hawaonekani kuwa sawa kama walivyokuwa katika miaka ya nyuma.
“Simba anaweza kupambana na Al Ahly kama alivyofanya katika michuano ya Super League. Mamelodi ni ndoto ya kutisha ni ngumu kwa Yanga na Simba kupambana nao kwa sasa hivyo ni muhimu kufanya maandalizi mapema.

