Maokoto Deilee Winner---

Dar es Salaam, Oktoba 10, 2023 – Kampuni namba moja ya michezo ya kubashiri SportPesa kushirikiana na mtandao wa Tigo kupitia huduma ya TigoPesa leo asubuhi wamewazawadia washindi wanne, ambapo washindi wawili wamejishindia simu janja, Joseph Kabelwa amejishindia shilingi 1,000,000 na Diatus Ishengoma amefanikiwa kuwa mshindi wa shilingi 15,000,000 wa kampeni ‘Maokoto Deilee’. Promosheni ilizinduliwa tarehe 21 mwezi wa nane,ambapo iliwapa fursa watumiaji wa Tigo kuingia kwenye droo baada ya kuweka fedha zao kwenye akaunti zao za SportPesa, kupitia akaunti ya TigoPesa na kisha kuweka bashiri zao.

 

Maokoto Deilee Winner---
Akizungumza baada ya droo iliyochezeshwa makao makuu ya ofisi ya SportPesa, Jijini Dar-Es-Salaam, Afisa wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano SportPesa Lydia Solomon amesema ,leo tumefanya droo yetu ya mwisho ya promotion  ya Maokoto Deilee, ambapo promotion hii tulizindua tare 21 mwezi wa nane, hadi leo tumefanikiwa kuwazawadia wateja wetu zawadi mbali mbali ikiwemo fedha na Simu janja wateja zaidi ya 550, na leo tumefanikiwa kupata mshindi wetu mkubwa wa milioni 15 anaetokea…… tunapenda kuwashukuru wateja wetu wote walioshiriki promotion hii iliyodumu kwa siku 50, na huu ni mwanzo tu, sisi kama SportPesa tutaendelea kuwazawadia wateja wetu zawadi mbalimbali na tutaendelea kushirikiana na kampuni ya Tigo, na sio Tigo peke yake hata mitandao mengine.

“Tunapenda kutoa rai kwa wateja wetu kuendelea kucheza na SportPesa ukiachana na promotion hii tuna bidhaa zetu zingine kama jackpot ya katikati ya wiki na Supa jackpot, ambapo huwa tunatoa washindi wa bonus kila wiki.”

Akiongea kwa niaba ya Tigo, Meneja Biashara wa Tigo pesa, Fabian Felician alisema kupitia promosheni hii yaMaokoto Deilee tumefanikiwa kubadilisha Maisha ya watanzania wengi,kuna ambao walikuwa hawana smartphone wameweze kupata  na wengine wameweza kujiongezea mitaji kwenye biashara zao.

“Kupitia promosheni hii, Maisha ya watanzania wengi yamebadilika na kwa mshindi wetu mkubwa wa 15,000,000 ni mfanyabiashara hivyo basi ameweza kujiongezea mtaji kwenye biashara yake.”

Tunapenda kuwashukuru wateja wetu kwa kushiriki promosheni hii na kuendelea kutumia Tigo pesa.

 

Share this: