Timu ya taifa ya Spain U21 leo usiku itashuka uwanjani kupambana na timu ya taifa Ukraine U21, katika mfululizo wa mechi za Kombe la U21 European Championship katika Uwanja wa Super bet Arena, ikiwa ni mchezo wao wa tatu katika kundi B, ambapo mmoja wapo anasubiriwa kuwa kinara wa kundi baada ya mechi ya leo.
Timu ya vijana ya Spain ambayo imepewa nickname ya La Rojita wameendela kufanya vizuri katika mechi zao katika mashindano haya barani Ulaya.
Hakuna ubishi kwamba vijana wa La Rojita wanataka kufuata mafanikio waliyoyapata kaka zao wakubwa kwa kutwaa kombe la ulaya la mataifa European Nations League, hivyo nafasi ya kukutana na Ukrain ni hatua muhimu katika kujihakikishia wanamaliza vizuri na kulitwaa kombe hili la vijana.
Hata kama vijana hawa walikutwa na mkosi wa kuishia nusu fainali ya mashindano haya miaka miwili iliyopita, kikosi chao kinachoongozwa na kocha Santi Denia’s kiko vizuri na kinapambana kuweka rekodi sawa.
Ili kufikia hapa Spain U21 waliwachapa waandaji wenza wa mashindano haya ya vijana chini ya umri wa miaka 21 Romania magoli 3-0, kabla ya kuwachapa Croatia 1-0, ambapo mchezaji wa Sporting Braga Abel Ruiz alifunga bao hilo.
Vijana wa Spain U21 wana rekodi nzuri ya kutofungwa mechi 18 mfululizo katika mechi za mashindano yote wlizocheza. Hii ilikuwa ni baada ya kufungwa katika mechi ya nusu fainali na Portugal mwaka 2021.
Ukraine wao kwa upande wao walianza vizuri kampeni yao katika mashindano haya baada ya kuitandika 2-0, dhidi ya Croatia. Wachezaji Oleksiy Kashchuk na mshambuliaji wa Shakhtar Donekst Danilo Sikan ndio walioongoza kichapo hicho, kila mmoja akifunga katika kila nusu ya mchezo.
Baada ya kichapo hicho Ukraine walipata ushindi katika mechi dhidi ya Romania, wakifaidika na goli la dakika za majeruhi la kujifunga kupitia kwa mchezaji Victor Dican. Vile vile katika mchezo huo Ukraine walikosa magoli mengi ya wazi katika nafasi ambazo walizitengeza.
Moja ya sababu inayofanya mechi ya leo baina ya timu hizi, yaani Spain U21 na Ukraine U21 ni matokeo ya Ukraine kwa ujumla. Vijana hawa wa kocha Ruslan Rotan walianza mashindano haya kama underdog, lakini kadiri siku zinavyoenda ndivyo wanavyozidi kungára, huku wakiwa tayari wamevuka hatua ya makundi.
Kama itakumbukwa timu hii ya Ukraine U21 mara ya mwisho kufikia hatua kama hii ilikuwa mwaka 2006. Hata hivyo ukiachia kipigo walichopigwa na timu ya Italia U21, katika mechi ya kirafikia mwanzoni mwa mwaka huu, timu hii haijafungwa katika mechi tisa katika mechi za mashindano yote.
Kwa mujibu wa takwimu zinazohusiana na timu hizi mbili, mafahari hawa wa Ulaya wamehskutana mara nne. Na katika hizo Spain U21 ameshinda mara mbili, Ukraine ameshinda mara moja na wametoa Sare mara moja.
Mara ya mwisho timu hizi mbili kukutana ilikuwa Mwaka 2011 katika hatua ya makundi kama hii ambapo timu ya Spain U21 ilishinda kwa magoli 3-0 na kwenda moja kwa moja kulitwaa kombe hilo la vijana.
Timu ya Spain imefanikiwa kupoteza mchezo mmoja tu kati ya michezo 6 waliyocheza siku za hivi karibuni. Timu zote mbili yaani Spain U21 wametokea katika kundi B na sasa wanaenda kupambana na Ukraine ambao wametokea kundi C.
Jambo moja ambalo ni la kuvutia ni kwamba timu zote mbili zina wachezaji wazuri ama washambuliaji wanaoweza kutoa ushindani katika mechi ya leo. Mshambuliaji wa Spain U21 Abel Ruiz alifunga goli la mapema mno na kuweka rekodi wiki iliyopita na kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya michuano hiyo kufunga goli katika sekunde 20, wakati timu ya Spain U21 walipocheza na Croatia na kuwafunga goli 1-0.
Kwa upande wa Ukraine nao walifanikiwa kuingia robo fainali baada ya kushinda mechi dhidi ya Romania wakiwa pungufu kwa mchezaji mmoja na kubakia 10, baada ya mchezaji Vladyslav Vanat kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Kwa upande wa Spain mchezaji wa kuchungwa zaidi ni Abel Ruiz, huku pia ikitegemewa kiungo mshambuliaji Sergio Gomez kutumika pamoja na Alex Baena pamoja na Alavez Antonio Blanco.
Kwa upande wa Ukraine wachezaji wa kutumainiwa ni pamoja na kipa Anatolii Trubin, huku mshambuliaji Danylo Sikan ataongoza safu ya mashambulizi.
Mchezo huu tayari upo kwenye tovuti yetu. Kubashiri tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

