Leo Jumamosi usiku, itapigwa mechi kali na ya kibabe kati ya mabingwa watetezi wa michuano ya Ulaya kwa vijana wa umri chini ya miaka 21 Spain U21, dhidi ya wana robo fainali wa msimu uliopita Croatia U21.
Timu hizi mbili zipo kundi B, pamoja na timu za mataifa ya Romania U21 na Ukraine U21 katika kinyang’anyiro cha ubingwa wa michuano ya Ulaya ( U21 European Championship) mwaka huu kwa vijana wanaochipukia.
Croatia na Hispania ni kumbukumbu nzuri katika medani ya soka la vijana. Hii ni kama mechi ya kisasi kwani hivi majuzi tu. Wiki iliyopita timu zao za wakubwa zilikutana katika fainali ya Uefa Nations League.
Timu ya wakubwa ya Hispania iliibuka washindi wa taji hilo, hivyo vijana wa Croatia U21, watakuwa wanataka kulipa kisasi cha kaka zao ambao nao kizazi chao cha dhahabu kinaelekea ukingoni bila ya kubeba taji lolote katika mashindano makubwa.
Katika mchezo wa kwanza ambao ulikuwa wa ufunguzi, Uhispania walianza vyema kwa kuwachapa Romania mabao 3-0 na wanaelekea katika mchezo dhidi ya Croatia wakiwania kufuzu hatua ya mtoano.
Wakati Hispania wakianza vizuri, Croatia U21 wao walikutana na kadhia dhidi ya Ukraine U21 katika mchezo wao wa kwanza.
Wakiwa na rekodi nzuri ya kucheza bila kupotea katika michezo 14 zilizopita ndani ya miaka miwili, hawakujali kuwa walikutana na wenyeji na kuwaangushia kipigo kizito na sasa wanataka kutuma ujumbe kupitia mechi dhidi ya Croatia U21.
Kwa takwimu za mchezo wa kwanza ilidhihirisha Romania waliwadhibiti Spain U21 katika kipindi cha kwanza kabla ya mabao ya Alex Baena, Juan Miranda na Sergio Gomez ambayo yaliwavuruga kabisa wenyeji wa mchezo.
Katika mchezo wa kwanza ambao ulishuhudiwa nazaidi ya mashabiki 21000 na kulikuwa na shinikizo kubwa lakini mchezo ujao utakaopigwa Santi Denia utakuwa tofauti .
Rekodi zinaonyesha kuwa ni katika mechi mbili tu, kati ya kumi na tano ambazo timu ya vijana ya Spain U21 ilishindwa kufunga bao chini ya mawili na ilikuwa ni dhidi ya timu ya vijana Mexico U 21 na Ufaransa U 21.
Wakati huo huo Spain U 21 wamecheza mechi nne bila kuruhusu bao hata moja, kati ya sita za mwisho walizocheza. Spain U 21 wanaonekana hawana mapungufu ikizingatiwa wanakutana na Croatia U 21 ambayo imepoteza hali ya kujiamini.
Timu ya vijana ya Croatia U 21 waliifunga England U 21 magoli 2-1 wakiwa ugenini mnamo mwezi machi mwaka huu, lakini matokeo hayo ya mechi ya kirafiki hayapaswi kuzingatiwa katika takwimu rasmi za michezo ya kimataifa ya kimashindano.
Timu ya vijana ya Croatia U 21 walipoteza rekodi yao ya mechi saba bila kupoteza walipokutana na timu ya Ukraine U 21ambayo iliwafunga mabao 2-0, huku nyota Mkhaylo Mudryk akiwa benchi katika kikosi cha Ukraine U 21.
Zaidi ya hapo, kikosi hicho cha Dragan Skocic sasa wameshindwa kufunga kwenye mechi mbili za mwisho kati ya nne walizocheza, huku wakiwa wamefunga mabao matatu tu, katika michezo hiyo.
Hali hii ya ubutu inaonyesha ni kwa kiasi gani timu hii ya viajana inatakiwa kufanya kazi ya ziada iwe kimbinu au kwa kutumia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja ili waweze kupata matokeo ambayo yatakuwa na faida katika mwendelezo wa mashindano hayo. Hasa hasa katika mechi ya leo dhidi ya Spain U21.
Mechi ya mwisho kwa Croatia katika kundi lao wataumana na Romania U 21 ambao ndio wanaonekana ndio timu dhaifu kuliko timu zote katika kundi B.
Taarifa za vikosi ni kwamba mchezaji wa Spain U 21 Denia anatarajiwa kurejea kikosini baada ya kuumia kwenye mchezo wa kwanza, huku Victor Gomes, Gabri Veiga, Rodrigo Requelme wanayo nafasi ya kuwepo kikosini leo.
Wachezaji Jon Pacheco na Baena walionyeshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya Romania, na huenda Kocha akawapumzisha ili kuepusha majanga ya kukosekana katika mechi zijazo.
Kwa upande wa timu ya Croatia U21, wachezaji Michele Sigo na Gabriel Vidocic wanatarajiwa kujumuishwa kwenye kikosi cha Croatia maeneo ya kati kati mwa uwanja, wakati pembeni katika winga ya kulia na kushoto Veldin Hodza na Ante Palversa wanatarajiwa kukiwasha.
Mechi hii tayari ipo kwenye tovuti yetu na kama utapendelea kubashiri basi tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#.

