USM-Alger-USM-Alger-

Ikiwa ligi ya Algeria inazidi kushika kasi kadiri siku zinavyokwenda ligi ya hiyo inaendelea siku ya leo Ijumaa ambapo timu za USM Alger inakutana na timu ya MC Alger katika dimba la Stade Omar Hamadi katika mechi ya ligi kuu (Ligue 1) nchini humo.

Mabingwa hawa wa kombe la shirikisho barani Africa katika msimu wa 2022/23 wanarudi uwanjani baada ya kutoka suluhu ya 0-0 dhidi ya timu ya MC Oran, mechi iliyopigwa Tarehe 10 Mwezi wa sita 2023.

Mpaka sasa USM Alger wameshacheza mechi 23, na wamefanikiwa kuvuna pointi 36, huku wakiwa na mechi mbili mkononi.

Mechi hii dhidi ya MC Alger ni moja kati ya mechi za viporo ambazo timu ya USM Alger inacheza baada ya kuwa inapewa nafasi ya kujiandaa kwa ajili ya mechi za kimataifa katika kombe la shirikisho barani Afrika.

MC Alger kwa upande wao mpaka sasa wameshacheza mechi 24 za ligue 1 na wanashikilia nafasi ya 3, wakiwa na jumla ya pointi 39. MC Alger wanaingia katika mechi hii wakiwa wametoka kucheza na CR Belouizdad Tarehe 9 Mwezi wa sita, lakini na wao walipata matokeo ya suluhu ya 0-0.

Mechi hii inategemewa kuwa na upinzania kutokana na timu zote mbili zinasaka nafasi ya kujiimarisha kileleni kwa kuwa kama USM Alger watashinda basi watasogea mpaka nafasi ya nne na kumshusha ES Setif ikiwa timu hiyo itafungwa ama kutoa droo.

Ikiwa timu ya MC Alger itashinda basi itajiweka kwenye mazingira mazuri ya kuisogelea timu ya CS Constantine ambayo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 46, baada ya kucheza michezo 25 na kushinda mechi 13, wamepata sare 7 na kufungwa michezo 5.

Timu ya CR Belouizdad ndio timu kinara katika msimamo wa ligi ya Algeria ikiongoza kwa pointi 54, wakiwa na tofauti ya pointi 8 baina yao na CS Constantine.

Duru za michezo nchini Algeria zinaarifu kuwa timu hizi mbili katika mechi sita ambazi kila timu imecheza USM Alger wameshinda mechi 3, wametoa sare mechi 1 na kupoteza mechi 2. Rekodi za USM Alger wakiwa nyumbani zinaonyesha kwamba wameshinda mechi 4, wametoa droo moja na wamefungwa mechi moja.

Kwa upande wa MC Alger katika mechi 6 walizocheza wao wameshinda mechi 2, wametoa droo 3 na wamefungwa mechi moja. Takwimu za MC Alger wakiwa ugenini zinaonyesha kuwa wameshinda mechi 1, wametoa droo mechi mbili na wamefungwa mechi tatu.

Takwimu hizi zinakupa mwanga kwamba USM Alger wana advantage dhidi ya MC Alger katika mechi wanazocheza uwanja wa nyumbani.

 

Wachezaji wa MC Alger vs USM AlgerUkiacha mechi za kufunga na kufungwa timu hizi zote mbili katika mechi 5 ambazo wamecheza wenyewe kwa wenyewe USM Alger ndiye amemfunga MC Alger mara nyingi, lakini mechi ya mwisho kwa timu hizi kukutana ilikuwa Tarehe 20/12/2022 ambapo timu ya USM Alger ilifungwa goli 1-0 na MC Alger, goli lililofungwa na kiungo wa timu hiyo Aziz Benabdi katika dakika ya 67.

Kuhusu muundo wat imu kwa namna ambavyo timu zote mbili zinategemewa kucheza mechi ya leo, wachezaji wanaotegemewa kuanza leo tukianzia na USM Alger kipa anategemewa kuwa Ousama Benbot huyu ni golikipa namba moja na amecheza mechi 12 mpaka sasa, zote akiwa amecheza kuanzia mwanzo mpaka mwisho, kwa maana ya dakika 90.

Katika mechi 12 mbili alizocheza amefanikiwa kupata cleansheet 5.

Mchezaji mwingine ni Saadi Redouani. Huyu ni beki namba mbili ambaye pamoja na kuzuia lakini amefunga magoli mawili. Ana rekodi nzuri ya kuzuia na kuanzisha mashambulizi kuelekue kwa wapinzani.

Mchezaji wa kuchungwa sana kwa timu ya USM Alger ni mshambuliaji wa kati Aimen Mahious. Mchezaji huyu tayari ameshafunga magoli 6 katika mechi 16 alizocheza. Kama mtakumbuka mchezaji huyu ni mmoja wa waliyeifunga Yanga jijini Dar-es-Salaam katika mechi ya Fainali ya kwanza ya kombe la shirikisho baranio Africa.

Kwa upande wa MC Alger wachezaji wao wa kutumianiwa ni pamoja na mshambuliaji wao kinara Kheireddine Merzougui. Mchezaji huyu amecheza mechi 14 na amefunga magoli 4 mpaka sasa.

Mchezaji mwingine ambaye anayeweza kuleta ushindani dhidi ya USM Alger ni winga wa kushoto anayetumika kama mshambuliaji Chouaib Debbih. Mchezaji huyu amecheza mechi 16 za ligue 1 na amefunga magoli 2 tu mpaka sasa.

Ni matumaini yetu kwa makala na takwimu hizi zitawapa mwongozo wale wote wanaopenda au kufuatilia timu zinazocheza ligi ya Algeria.

Mechi hii tayari ipo katika tovuti yetu. Kama utapendelea kubashiria basi tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

 

 

 

 

 

Share this: