Czech U21Czech-U

Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 21 ya Jamhuri ya Czech Republic U21, kesho Alhamisi ya Tarehe 22 Juni 2023, itakuwa mwenyeji wa timu ya vijana wa England U21 wa umri huo huo utakaopigwa katika dimba la Batumi Arena huko Georgia ikiwa ni muendelezo wa michuano ya Euro Championship 2023  kwa vijana wa U21.

Timu zote mbili yaani Czech Repblic na England zote zimewahi kutwaa ubingwa wa michuano hii, ambapo vijana wa Jamhuri ya Czech walitawazwa mabingwa wa U 21, mwaka 2002, huku timu ya vijana ya England U21 wao mara ya mwisho kubeba Kombe hili ilikuwa mwaka 1984.

Tangu Jamhuri ya Czech itwae Kombe hili hawajawahi tena kurudi katika kiwango cha ushindani na kulitwaa kombe Euro Championship. Kwa kifupi mambo yamebadilika na kwa miaka ya hivi karibuni hawajawa na kizazi chenye kushawishi katika mafanikio ya soka la vijana.

Upande wa England licha ya kwamba wana muda mrefu bila kufanikiwa kwa takribani miaka 39, lakini kwa miaka ya hivi karibuni wamekuwa wanazalisha vijana wa U21 ambao wana muendelezo ulio bora.

Czech wanaingia katika mechi hii wakiwa katika kiwango kisichoridhisha, kwani hawajashinda katika mechi zao tano zilizopita. Wamepata sare tatu na kupoteza mbili, wakati England wao wameshinda tatu na wamepoteza mbili.

Katika mechi tatu za mwisho walizokutana na England, timu ya vijana ya Czech Republic U21 wamefungwa mechi zote, na mechi walizopambana zimezalisha mabao kuanzia mawili na kuendelea.

Tukirejea katika historia ya jamhuri ya Czech, timu yao imewahi kucheza hatua ya robo fainali mwaka 1996, lakini wakashindwa kufuzu mnamo mwaka 1998.

Timu hiyo ya vijana wa Czech walitinga fainali mwaka 2000 na 2002 ambapo walishinda kwa mikwaju ya penati.

Mara kadhaa Jamhuri ya Czech ilishindwa kufuzu kwenye mashindano ya Vijana wenye umri chini ya miaka 21, ambapo majaribio yao ya kufuzu kushiriki kwa mwaka 2004 na 2006 yaligonga mwamba. Hatimaye walifanikiwa kufuzu kwenye mashindano ya 2007, lakini wakaishia kumaliza mwa mwisho kwenye hatua ya makundi.

Kwa mara nyingine, hata baada ya kufanikiwa kufuzu mashindano ya mwaka uliopita, katika jaribio lao lililofuata napo walishindwa kufuzu katika mashindano hayo msimu wa mwaka 2009. Czec Republic walijitafuta na kufanikiwa kufuzu Mwaka 2011, lakini walimaliza katika nafasi ya nne.

 

England U21 vs CzechKikosi cha Jamhuri ya Czech kinanolewa na kocha Jan Suchoparex kitashuka katika mchezo huo kikiwania ushindi muhimu dhidi ya England. Ikumbukwe mara ya mwisho kwa timu hizi mbili za vijana za U21 ilikuwa 2022 Juni 3 ambapo timu ya vijana ya Czech Republic ilibamizwa kwa magoli 1-2, magoli yaliyofungwa na Emille Smith Rowe (22) na Jacob ramsey (62) kwa upande wa England na goli la kufutia machozi lilifungwa na Daniel Fila (87).

Upande wa Uingereza, timu ya Vijana wenye umri chini ya miaka 21 haijapoteza hata mechi moja katika mechi 22 kati ya 26 za mwisho walizocheza katika mashindano yote.

Jamhuri ya Czech wameshinda mechi moja tu kati ya saba za mwisho za michuano ya Ulaya kwa vijana wenye umri chini ya miaka 21.

Kumekuwa na mabao kuanzia mawili na kuendelea kwenye michezo mitatu ya mwisho ya Jamhuri ya Czech kwenye michuano ya Ulaya kwa vijana wenye umri chini ya miaka 21.

Tofauti na timu ya timu ya Czech England kwa vijana wenye umri chini ya 21 haijapoteza mchezo katika kipindi cha kwanza kwa michezo 14 ikiwa ugenini katika mashindano yote.

Katika mechi 48 za mwisho za mashindano yote waliyocheza, timu ya Taifa ya Vijana ya England U21 haijapoteza mechi takribani 43.

Vile vile timu ya vijana ya England U21 haijapoteza mchezo kwenye michezo sita ya mwisho iliyocheza ugenini katika mashindano yote na imeshinda mechi zote hizo.

Taarifa mbaya kwa timu ya vijana ya England U 21 ni kwamba haijawa na kiwango kizuri katika mashindano ya Euro U 21 kwakuwa wameshinda mechi moja pekee katika mechi saba za mwisho katika mashindano hayo.

Timu ya vijana ya England wanajivunia vipaji vya wachezaji kama Emil Smith Rowe, James Madueke na Gordon Brown wakati timu ya vijana ya Jamhuri ya Czech wana vijana kama Pavel Sulc, Lucas Cerv, Phillip Kaloc, Vaclav Sejk, Jurasek, Vicek n.k.

Mechi hii tayari ipo kwenye tovuti yetu. Kubashiria tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#.

Share this: