Alaves vs Eibartmp a ebccc - - -b fc- ac ff

Kesho Alhamisi ya Juni 8,2023, katika dimba la Estadio Mendizorrota (Vitoria Gasteiz), klabu ya Derpotivo Alaves, watakuwa wakiwaalika Eibar kwenye mchezo wa mtoano wa (Playoff) ya nusu fainali katika Ligi ya Segunda nchini Hispania.

Mchezo huu wa kesho ni wa marudiano ambapo katika mchezo wa mkondo wa kwanza, Eibar walikuwa nyumbani walilazimishwa sare ya bao moja na Alavez.

Kwa takribani miaka mitano Klabu ya Alavez ilikuwa na utulivu mkubwa katika Ligi kuu ya Hispania (La Liga) kabla ya kuporomoka ambapo msimu uliopita ilimaliza mkiani mwa ligi hiyo.

Wakiwa ni wageni katika ligi ya daraja la pili nchini Hispania, Alaves walikuwa wakipewa kipaumbele cha kufanya vizuri zaidi lakini ikashindikana.

Katika mzunguko wa kawaida, Alavez walikosa alama moja pekee, ili wapate tiketi ya moja kwa moja kupanda daraja. Lakini kutokana na muundo au mfumo wa timu za ligi ya chini ya La Liga, timu hii imetakiwa kucheza raundi moja ya playoff, ambao ndio unaowapa nafasi ya kucheza mchezo dhidi ya Eibar

Hii ndiyo nafasi nyingine kwa Alavez kusogea juu, kama wakifanikiwa ama wataweza kuitumia kupanda daraja.

Upande wa pili, Eibar wao walikuwa na maisha mazuri katika ligi ya taifa kwa takribani miaka kumi, lakini katika msimu wa 2020/21 walishuka daraja.

Mazingira ya Eibar yalikuwa kama ya Alavez msimu huu, ambapo nao walikosa alama moja pekee ili kupata tiketi ya kupanda daraja.

Alaves vs EibarHatua ya mtoano ni ya mahesabu makubwa iwapo timu inahitaji kupanda daraja lakini ndio njia pekee iliyosalia kwa kikosi cha Gaizka Garitano kujaribu nafasi ya kusogea daraja la juu ya Ligi.

Takwimu zinaonyesha timu hizi hazijawa na uwiano bora wa kufunga mabao ambapo mchezo huu umepewa wastani wa kutoa mabao chini ya 2.5.

Rekodi zinaonyesha katika michezo mitano ya mwisho walizokutana ,ni michezo miwili pekee ambayo yalipatikana mabao matatu,lakini michezo mitatu iliyosalia miwili na mmoja timu hizo hazikufungana kabisa.

Katika michezo hiyo mitano,Alavaez iliibuka mshindi katika michezo miwili,Eibar ilishinda mmoja na sare mmoja.

Nikola Malas ndiye mchezaji pekee wa Alves atakayekosekana katika mchezo huo wa siku ya Alhamis dhidi ya Eibar,nyota huyo ni muhimu sana katika kikosi hicho lakini amekuwa akiandamwa na majeraha tangu mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu.

Tayaro Alaves walishapata suluhisho la kukosekana kwa Nikola Malas hivyo wanacho kikosi kazi kitakachopambana katika kuhakikisha wanapanda kucheza Ligi Kuu.

Alaves wanao mastaa kama mlinda mlango Antonio Sivera,mabeki kama Nahuel Tenaglia,Abdelkebir Abqar,Aleksandar Sedlar,na Ruben Duarte.

Wanao viungo matata kama Salva Sevilla,Carlos Benavidez na Jon Guridi huku washambuliaji wanaotarajiwa kuwepo katika mchezo huo ni Luis Rioja,Mamadou Sylla na Jason.

Katika michezo mitano ya mwisho ambayo Alaves wamecheza wameshinda mchezo mmoja pekee dhidi ya Malaga huku wakitoka sare michezo minne,tafsiri yake hawajapoteza kati ya hiyo mitano.

Upande wa Eibar wana tatizo la kukosa wachezaji katika idara ya ulinzi, na Kocha wao Gaizka Garitano amesema anao walinzi watatu tu walio wazima huku wakiwaorodhesha Anaitz Arbilla,,Imanol Garcia,,Frederico Venancio,Rober Correa,Daniel Lasure pamoja na Jose Rios Reina wote hawatokuwepo huku kiungo Sergio Alvarez akitarajiwa kuanzishwa katika eneo la ulinzi.

Kikosi cha Eibar kinachotarajiwa kuanza katika mchezo huo wa alhamis kitaongozwa na mlinda mlango Luca Zidane, mabeki ni Alvaro Tajero,Sergio Alvarez,Juan Gonzalez na Chema.

Viungo ni Peru Nolaskoaain, Javier Munoz, Matheus Pererira, huku washambuliaji watakaoongoza kikosi hicho ni Jose Corpas Serna na Stoichkov.

Katika mechi tano za mwisho ambazo Eibar wamecheza, wao wamepoteza mechi mbili,sare mbili huku wakishinda moja pekee dhidi ya Huesca.

Sababu zinazoifanya mechi hii pengine ikatoa mabao chini ya mawili ni kama ifuatavyo,Alaves imefunga mabao matano katika mechi sita za mwisho,vilevile mechi zao sita za mwisho ,tano zimezalisha ,mabao chini ya 2.5.

Eibar wao wamefunga bao 5 katika mechi zao saba za mwisho, vilevile katika mechi zao saba za mwisho,kati ya hizo zimetoa bao chini ya 2.5,nenda kabashiri mchezo huu kupitia SportPesa ushinde donge nono.

Share this: