Wachezaji wa Polisi Tanzania na Mtibwa Sugar katika moja ya mechi walizowahi kuktana.MtibwaPolisi

Klabu ya Polisi Tanzania leo alasiri inatimba uwanjani kupambana na timu ya Mtibwa Sugar, katika uwanja wa Ushirika Moshi, katika mechi za kumalizia msimu wa ligi kuu ya soka Tanzania, NBC Premier League ambayo inahesabika kama hatma ya moja kati ya timu hizo mbili, kwenda kwenye play off ama kushuka daraja, baada ya mechi mbili zijazo.

Ligi Kuu ya Tanzania bara msimu wa 2022/23 tayari imepata bingwa wake ambaye ni Yanga ambayo imeutetea baada ya Jumamosi kuicharaza Dodoma Jiji magoli 4-2 na kufikisha alama ambazo hakuna Timu yeyote itakayozifikia.

Kwa upande mwingine wa pili wa shilingi, nazungumzia timu nyingine zilizosalia, ukiondoa Yanga, Simba, Azam na Singida, zilizopo juu katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara, yaani NBC Premier League zinapambana kutokushuka daraja.

Tayari mpaka sasa timu ambayo imeshuka daraja moja kwa moja ni Ruvu Shooting pekee, ambayo iliupa mkono wa kwa heri ligi kuu baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Simba cha bao 3-0, sasa mlango upo wazi kwa timu moja ambayo iwapo itazubaa utaungana na masarange wa Ruvu Shooting kuelekea Championship.

Kitendawili cha timu zipi zitaungana na Ruvu Shooting kitateguliwa katika siku chache zijazo pale ambapo mechi za mwisho zitakapopigwa kuanzia wiki hii katika kukamilisha ratiba ya msimu wa 2022/2023.

Zipo timu kadhaa ambazo hazipo salama, moja wapo kati ya timu hizo ni Polisi Tanzania. Timu hii ya maafande wa Polisi Tanzania, ipo kwenye hatari zaidi. kwa kuangalia namna msimamo wa ligi ulivyo mpaka sasa.

Polisi Tanzania ipo nafasi ya 15, wakiwa wamejikusanyia alama 22, na leo hii inaweza ikawa ndio siku yao ya hukumu ya kushuka daraja, watakapokuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar, ambao wapo nafasi ya 13 wakiwa na alama 29.

Polisi Tanzania inanolewa na Kocha Mwinyi Zahera, watahitaji  kupata ushindi kwenye dimba la Ushirikia Mjini Moshi, ili kuweka hai matumaini ya kusalia katika Ligi Kuu msimu ujao.

Kwa upande mwingine wakatamiwa wa Manungu Mtibwa Sugar nao wanazitaka alama 3 ambazo zitawasaidia kusogea juu zaidi huku wakizipigia hesabu mechi 2 zitakazosalia ambazo zitaamua iwapo watabaki moja kwa moja  au watacheza mechi za mtoano, zinazojulikana kama mechi za Play-off.

Iwapo Polisi itashinda leo dhidi ya Mtibwa, basi watakuwa wamefikisha alama 25, na watalazimika pia kushinda mechi 2 zilizosalia ili kuwafanya wawe na alama 31, zitakazo wapa matumaini ya kutokwenda kwenye mechi za play off.

Kwa maneno mengine, baada ya mechi ya leo kuchezwa na matokeo kujulikana ndipo hesabu za kujumlisha na kutoa zitakapoanza kupigwa, ili kujua nani kavuna nini msimu huu.

Hata baada ya mechi hii hesabu zitaendelea kupigwa na wapenzi wanachama viongozi namashabiki wa Polisi Tanzania, huku wakitegemea matokeo ya timu za Mtibwa na Coastal Union mwenye jumla ya alama (31) kwa sasa, ili kuona kama watanufaika na matokeo hayo ambayo tunaita ni majaliwa.

wachezaji wakijiandaa mechi kati ya Polisi Tanzania dhidi ya Mtibwa SugarIwapo Polisi watafungwa na Mtibwa Sugar, alafu Mbeya City wakashinda mechi moja kati ya mbili zilizosalia, tafsiri yake ni kuwa maafande wa Polisi Tanzania, wataiaga rasmi Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu, ikizingatiwa wao wana mchezo mgumu ujao dhidi ya Wekundu wa Msimbazi Simba.

Takwimu kwa timu hizi mbili msimu huu sio nzuri. Tukianza kwa kuwatazama Polisi Tanzania,ni timu ya pili kwa kushinda mechi chache katika Ligi Kuu(5) sawa na Ruvu Shooting. Polisi ni timu ya pili kwa kupoteza mechi nyingi(15) ,ndio timu ya pili kwa kufunga bao chache katika Ligi Kuu(22), ni ya 3 kuruhusu bao nyingi (39) ingawa Mtibwa ndio kinara kwa kuruhusu bao nyingi(41).

Timu hizi zinakutana zikiwa zimetoka kushinda mechi zao za mwisho zilizopita,Polisi iliinyuka Ihefu, bao 2-1, wakati Mtibwa waliwatandika Coastal Union bao 1-0.

Katika mechi 5 zilizopita, Polisi Tanzania imeshinda 2, na kupoteza 3 wakati Mtibwa imeshinda 1 na kupoteza 4.

Katika historia yao tangu wakutane katika Ligi Kuu, Klabu hizi zimeumana mara 6, Polisi Tanzania imeshinda 3, Mtibwa imeshinda 2 na sare 1.

Katika mechi 5 za mwisho,Polisi imeshinda mara 3, Mtibwa imeshinda mara 1 na sare 1.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Novemba 22, 2023, Wakatamiwa waliibuka na ushindi wa bao 2-1, je watapiga pale pale panapouma?

Tayari mchezo huu baina ya Polisi Tanzania dhidi ya Mtibwa Sugar upo kwenye tovuti yetu sportpesa.co.tz. Pia unaweza kupiga *150*87# kucheza kwa kutumia simu za kitochi almaarufu kama viswaswadu.

Share this: