Leo usiku katika dimba la Emirates tutaishuhudia dabi ya London kati ya vinara wa ligi kuu ya EPL, baina ya Arsenal na Chelsea.
Arsenal wanashuka dimbani wakiwa na shinikizo la kuhitaji ushindi utakaowarejesha kwenye njia ya ushindi waliyoipoteza katika michezo minne iliyopita.
Katika michezo hiyo vijana wa Mikel Arteta wametoka sare ya bao 3 dhidi ya Liverpool,sare nyingine ya bao 2 dhidi ya West Ham United kabla ya kuchomoka dakika za lala salama kwa sare ya bao 3 dhidi ya Southampton na kisha wakatandikwa na mabingwa watetezi Manchester City bao 4-1.
Kwa mara ya mwisho The Gunners kupata ushindi katika Ligi Kuu ya England ilikuwa ni April Mosi 2023 walipowanyuka Leeds United bao 4-1, tafsiri nyepesi ni kwamba wametimiza mwezi mmmoja kamili bila ya kupata ushindi katika Ligi hadi wanakwenda kukutana na Chelsea.
Kikosi cha Arsenal kinapitia wakati mgumu kwani baada ya kuondolewa katika michuano ya Ulaya dhidi ya Sporting CP, wameshinda mechi 2 kati ya 6 za mwisho kwenye Ligi Kuu ya EPL lakini katika kila mchezo wameruhusu bao ishara ambayo inatuambia safu yao ya ulinzi inamapungufu kwa miezi ya karibu.
Katika michezo 10 ya mwisho katika mashindano yote waliyocheza,ni mara moja tu (Fulham 0-3 Arsenal) ambapo walishinda bila kuruhusu bao lakini tisa waliruhusu wavu wao kuguswa jambo ambalo si zuri kwa upande wao.
Wanawakaribisha Chelsea ambao wapo hoi na licha ya kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi kwa kumuondoa Graham Potter na kumkabidhi mikoba Frank Lampard ambaye ataiongoza hadi mwisho wa msimu, lakini timu hiyo imepoteza mechi tano mfululizo katika mashindano yote.
Kama haitoshi katika mechi hizo tano za utawala wa Frank Lampard ,The Blues imeruhusu mabao 9 na imefunga bao 1 pekee jambo ambalo linadhihirisha wana matatizo kwenye idara nyingi kuanzia kwenye safu ya ulinzi na ushambuliaji.
Mara ya mwisho Chelsea kupata ushindi ilikuwa Machi 11,2023 walipowachuka Leicester City bao 3-1 na tafsiri yake iwapo iwapo Chelsea itashindwa kupata ushindi Mei 2,dhidi ya Arsenal watakuwa wamecheza miezi miwili kamili bila ya kuonja ushindi katika EPL.
Baada ya kupoteza dhidi ya Brentford kwa bao 2-0 kwenye dimba la Stanford Bridge,mashabiki wa Klabu hiyo waliwazomea wachezaji wao jambo ambalo lilimuibua Frank Lampard ambaye alisema anaelewa hisia za mashabiki wao kwakuwa timu yao haipati ushindi.
Kupoteza kwao dhidi ya Brentford kumewaporomosha Chelsea kwenye msimamo wa EPL kutoka nafasi ya 11 hadi ya 12 wakiwa na alama 39 wakati Arsenal wao licha ya matokeo hasi mchanganyiko yamewafanya waendelee kusalia nafasi ya kwanza wakiwa na alama 75.
Hivyo kuelekea mchezo huu ni dhahiri kwamba zinakutana timu mbili tofauti. Moja ni bora iliyopoteza matokeo mazuri yenye muendelezo na timu ambayo imepoteza ubora tangu kuanza kwa msimu ambayo ni Chelsea ambayo tayari imefukuza makocha wawili (Thomas Tuchel na Graham Potter).
Licha ya kuwa na matokeo ambayo si ya kuridhisha bado dabi huwa ni mchezo wa tofauti hivyo kwa ukubwa wa klabu hizi inawezekana tukashuhudia kitu cha tofauti katika mchezo huu wa leo.
Moja ya kitu cha kukitazama kuelekea mchezo huu ni takwimu za wachezaji pia ambapo tukianzia kwa Chelsea hadi sasa mfungaji wao bora ni Kai Haverts aliyefunga mara 7,akifuatiwa na Raheem Sterling(4),Mason Mount (3) huku Ben Chilwell na Joao Felix kila mmoja akifunga bao 2 wakati vinara wa pasi za mabao ni Ben Chillwel ,Marc Cucurella,Enzo Fernandez,Mason Mount,Mkhailo Mudryk,Thiago Silva na Raheem Sterling wote kila mmoja anazo 2.
Wachezaji waliopiga mashuti mengi kutoka Chelsea Kai Haverts (26) akifuatiwa na Raheem Sterling (12) huku Joao Felix amepiga mashuti (11).
Upande wa Arsenal kinara wao wa kupachika mabao ni Gabriel Martinelli (15) akifuatiwa na Bukayo Saka (11), Martin Odegaard (9) naye Gabriel Jesus kafunga bao (9) huku vinara wa pasi za mabao ni Bukayo Saka (11),Martin Odegaard (8), Leandro Trossard (8) huku Gabriel Jesus na Gabriel Martinelli kila mmoja akitoa pasi 5,ukizitazama takwimu hizi zinaonyesha The Gunners ni bora zaidi ya Chelsea.
Kwa ujumla Klabu ya Arsenal imeshinda mara nyingi zaidi kwenye Dabi ya London dhidi ya Chelsea ambapo katika michezo 106,The Gunners wameshinda mara 66, Chelsea imeshinda mara 59 na sare ikijitokeza mara 81.
Swali ni je ni timu ipi kati ya Arsenal na Chelsea itazinduka kupitia dabi hii ya London?
Mchezo huu tayari upo katika tovuti yetu. Kucheza tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

