Ligi Kuu ya Italia almaarufu kama Serie A, imefikia patamu, ambapo timu ya AS Roma itachuana na AC Milan katika mwendelezo wa mechi ya ligi kuu ya Italia. Ukiachana na mbio za ubingwa ambazo tayari zinakaelekea ukingoni, timu ya Napoli inahitaji alama chache tu, ili kumaliza ligi na kuwa bingwa wa Serie A kwa msimu wa 2022/2023.
Chini ya Napoli kuna Lazio. Timu hii ina jumla ya ponti 61. Hii inamaanisha tofauti ya pointi 17 baina yao. Chini ya Lazio kuna Juventus alafu anafuata AC Milan na AS Roma. Hapo hapo bado kuna mbio za kuwania nafasi ya kucheza ligi ya klabu bingwa Ulaya na ligi ya Europa Ulaya ambayo zinazidi kushika kasi.
Sasa hapo kesho April 29, kwenye dimba la Stadio Olimpico, klabu ya AS Roma watakuwa wenyeji wa AC Milan ambao kwa sasa wapo nusu fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya.
Mtanange huu mzuri unachagizwa na nafasi ambazo timu zote za juu zilivyokaa katika msimamo wa ligi. AC Milan ambao ndio mabingwa watetezi wa Scuddeto wapo nafasi ya 4 wakati AS Roma wapo nafasi ya tano lakini cha kuvutia zaidi wote wana alama sawa (56) vilevile wana wastani sawa wa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa (+14) na wote ni baada ya michezo 31.
Hadi sasa Rossoneri wapo kwenye nafasi ya kucheza Ligi ya mabingwa Ulaya wakati Giallorossi wapo kwenye nafasi ya kucheza Europa sawa na Inter Milan (Nerrazuri) ambao wapo nafasi ya 6 wakiwa na alama 51 kibindoni lakini mambo yatabadilika kulingana na michezo itakavyozidi kuchezwa.
AC Milan iliinyuka Lecce bao 2-0 na kuendeleza rekodi bora ya michezo ya Ligi hivi karibuni wakishinda miwili na sare 2 kati ya minne waliyocheza,wakati AS Roma walitoka kupoteza 3-1 dhidi ya Atalanta huko Gewis Stadium na kuvuruga ushindi wao wa michezo mitatu mfululizo kwenye Serie A.
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Januari ,2023 katika dimba la San Siro timu hizi zilitoshana nguvu kwa kufungana 2-2 ambapo ilishuhudiwa Pierre Kalulu na Tommaso Pobega wakifunga kwa upande wa Rossoneri, wakati Ibanez na Tammy Abraham walifunga kwa upande wa Giallorossi.
Rossoneri wamekuwa na matokeo bora kwenye michezo 6 ya mwisho waliyokutana katika Serie A na Giallorossi kwani wameshinda mara 4 na sare 2, na mara ya mwisho AS Roma kuifunga AC Milan ilikuwa Oktoba, 2019 hivyo mechi hii watakuwa wanasaka ushindi wa kwanza dhidi ya vijana wa Stefano Pioli baada ya miaka minne kupita.
Rafael Leao ndiye mshambuliaji tegemeo wa AC Milan ambaye ameifungia jumla ya mabao 13 yakiwemo matano katika mechi tano za mwanzo katika Serie A, na sasa yupo kwenye orodha ya vinara watano wanaowania tuzo ya mshambuliaji bora wa msimu wa 2022/23.
Upande wa AS Roma wanaye Paulo Dyabala na ndiye mkali wao wa kupachika mabao akiwa amecheka na nyavu mara 11, manne kati ya hayo alifungwa mwanzoni mwa msimu huu.
Wakiwa katika ardhi yao ya nyumbani AS Roma wameshinda mechi 10, sare 1 na imepoteza mara 4 katika michezo 15, wakati AC Milan wao wamecheza mechi 16 ugenini katika Serie A msimu huu. Wameshinda mechi 6, kutoa sare 5, wamepoteza 5 na wamechukua alama 23, kati ya 48 zilizokuwepo.
Kwenye michezo 6 ya mwisho ya Ligi, AS Roma imeshinda michezo mitatu na kupoteza mitatu wakati AC Milan imeshinda miwili,sare tatu na kupoteza mmoja.
Jose Mourinho na vijana wake watahitaji ushindi wa kufa au kupona ili waiache AC Milan na wawasogelee Juventus ambao wapo nafasi ya 3 wakiwa na alama 59 na hata Lazio waliopo kwenye nafasi ya pili na alama zao 61, lakini vilevile Pioli na kikosi chake nao wanawania mbio za aina hiyo.
Baada ya mchezo huo,AS Roma watakuwa na mechi 2mfululizo za Ligi ambazo ni dhidi ya Monza na Inter Milan kabla ya kuivaa Bayer Leverkusen kwenye nusu fainali ya Europa wakati AC Milan watacheza mechi 2 za Ligi dhidi ya Cremonese na Lazio kabla ya kuivaa Inter Milan kwenye nusu fainali ya Klabu bingwa Ulaya hivyo matokeo ya mchezo huu utakuwa unawapa mwanga kuelekea katika michezo hiyo.
Mechi hii tayari ipo kwenye tovuti yetu. Ili Kuibashiria tembelea tovuti yetu sportpesa.co.tz au piga *150*87#.

