ChelseaChesleaReal

Kesho katika dimba la Stanford Bridge ni siku ambayo Chelsea maarufu kama ‘’The Blues’’, zamani The Roman Army, watakuwa na kibarua ambacho matokeo yake yataamua mustakhabali wa timu hiyo kuhusu ushiriki wao katika michuano ya Klabu bingwa msimu ujao, watakapowakaribisha mabingwa wa kihistoria wa kombe la klabu bingwa Ulaya Real Madrid, kwenye mchezo wa marudiano ya mchezo wa pili wa robo fainali.

Kwanini tunasema ni mchezo utakaoamua hatma ya klabu hiyo Ulaya? Ni kwa sababu hawapo kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi EPL, ambapo wanashika nafasi ya 11 wakiwa na alama 39 katika michezo 29, na timu zilizopo juu yao zimeonekana kushinda mechi zao kuliko wao ambao wameendelea kudondosha alama,hivyo njia pekee ya wao kurejea Ulaya ni kutwaa taji msimu huu kinyume na hapo huenda msimu ujao tusiwaone katika michuano hii

Tukirejea katika mechi yenyewe ya marudiano hiyo kesho, Chelsea wanaonolewa na Frank Lampard, walipoteza mechi hiyo ugenini kwa bao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa kwenye dimba la Santiano Bernabeu, huku mabao ya Los Blancos yakiwekwa kambani na Karim Benzema na Marco Assensio.

Haukuwa mchezo mzuri kwa Chelsea ambao walianza kwa kutengeneza nafasi, lakini umahiri wa kipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois ndio uliowanyima uongozi .  Baada ya dakika 15 za kipindi cha kwanza vijana wa Frank Lampard walionekana  wakipoteana kabisa mchezoni.

Kielelezo tosha kuwa Chelsea walizidiwa ni takwimu za mchezo ambapo Real Madrid walimiliki mchezo kwa asilimia 53 wakati Chelsea ni asilimia 42, Real Madrid ilipiga mashuti 9 yaliyolenga lango wakati Chelsea walipiga matatu tu yaliyolenga lango, Real Madrid walipiga mashuti matano ambayo hayakulenga lango.

 Chelsea walijaribu na kufanikiwa kufanya mashambulizi matau tu. Kipa wa Chelsea Kepa Alizaballaga aliokoa michomo ya hatari mara 7 wakati kip awa Real Madrid Courtois alifanya hivyo mara 3 tu,timu zote zilipata kona tatu.

Ukizitazama takwimu hizo bila shaka unaona namna Chelsea ilivyozidiwa katika mchezo huo na kupoteza muelekeo na kama haitoshi walicheza takribani dakika 20 wakiwa pungufu kufuatia beki wake wa kushoto, Ben Chillwel kulimwa kadi nyekundu kwa kumzuia Rodrygo aliyekuwa akielekea kufunga bao.

Uwezo wa Chelsea kushinda dhidi ya Real Madrid upo, lakini uhakika wa kuwaondoa mashindanoni Los Blancos haupo. The Blues wapo kwenye kipindi cha mpito cha ujenzi wa timu, ambapo wamefanya maingizo mapya ya wachezaji wengi katika dirisha dogo la usajili.

ACMilanNapoliKatika usajiri huo majina ya kina Enzo Fernandes, Joao Felix, Mikylo Mudryk, Benoit Badiashire, David Fofana,Noni Madueke yameingia kikosini.

Tofauti na Real Madrid ambayo licha ya maingizo mapya ya wachezaji Aurelien Tchouameni, Eduardo Camavinga, bado uti wa mgongo wa kikosi chao umeendelea kuwepo ukishikiliwa na Toni Kroos, Luka Modrik ambao wanatawala eneo la kiungo, wakati Karim Benzema akiendelea kuwaongoza makinda Rodrygo na nyota bora wa mchezo uliopita ambaye ni Vinicious Jr .

Inaeleweka, koch awa Real Madrid Carlo Ancelot, ambaye ni mshindi mara 4 wa UCL, amewekeza zaidi nguvu na akili katika mashindano haya ikizingatiwa kwamba hana nafasi ya kutwaa Kombe la La Liga ambapo Barcelona wanaongoza kwa tofauti ya alama 13 dhidi yao.

Mechi hii ya marudiano inatukumbusha ile ya msimu uliopita ambapo The Blues wakiwa nyumbani walitandikwa bao 3-1 katika dimba la Stanford Bridge huku Karim Benzema akifunga Hat Trick.

Real Madrid wanarejea tena Uingereza msimu huu ambapo katika hatua ya 16 bora waliwafunga Liverpool bao 5-2 katika dimba la Anfield jambo ambalo linatoa taswira halisi kuwa Los Blancos wanao uwezo wa kushinda popote pale ilimradi ni michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya.

Timu hizi zimekutana mara 7 hadi sasa . Chelsea imeshinda mara mara 2, huku Real Madrid imeshinda mara 4 na kutoa sare mechi moja.

Kwingineko ni nchini Italia, katika dimba la Diego Armando Maradona ambapo Napoli watakuwa wakijiuliza kipi kimewatokea pindi wanapoumana na AC Milan kwani katika mechi 2 za mwisho walizokutana wamepoteza tena kwa idadi ya mabao matano kwa sifuri ingawa mechi ya kwanza ilikuwa ni ya Seria A.

AC Milan chini ya Stefano Pioli, wana vina saba na michuano hii ya Ulaya wakiwa ndio mabingwa mara nyingi zaidi baada ya Real Madrid. Duru za kimichezo zinatuarifu kuwa AC Milan wamelitwaa taji hili mara 7, na baadae kupoteza utawala wao katika michuano hii, katika miaka ya hivi karibuni. Mara ya mwisho AC Milan kutwaa kombe hili ilikuwa Mwaka 2007, walipowafunga Liverpool 2-1 na kutwaa taji hilo, katika mchezo wa fainali uliopigwa katika dimba la Olympic Stadium jijini Athens, Ugiriki.

AC Milan wanaelekea katika mchezo huu wa marudiano wakiwa na faida ya bao moja walililopata katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la San Siro lililofungwa na Ismael Benaccer na sasa watahitaji sare ya aina yeyote ili wafuzu hatua ya nusu fainali.

Licha ya ushindi walioupata lakini AC Milan hawakuwa na takwimu bora kama Napoli kwani walizidiwa kidogo katika  umiliki wa mpira kwa asilimia 4(AC Milan asilimia 48,Napoli asilimia 52), huku mashuti yaliyolenga lango AC Milan walipiga mawili tu wakati Napoli walipiga Matano.

Mashuti aambayo hayakulenga lango, AC Milan walipiga matatu wakati Napoli walipiga 7, AC Milan ilipata kona 3 wakati Napoli walipata kona 10. AC Milan walifanya mashambulizi ya kushtukiza mara 5 wakati Napoli walishtukiza mara 6. Kipa wa AC Milan Mike Maignan aliokoa hatari 6 wakati wa Napoli Alex Merek aliokoa hatari moja peke yake.

Huenda mechi ya marudiano ikawa na faida kiasi kwa Napoli. Timu hii ilicheza mchezo wa kwanza bila ya mshambuliaji wake tegemeo Victor Osimhen, ambaye mpaka sasa ameshafunga mabao manne katika mashindano haya ya kombe la klabu bingwa Ulaya.

Iwapo mchezaji huyu mzaliwa wa Nigeria atakuwa fiti, ataongeza nguvu katika eneo hilo la ushambuliaji ingawa watamkosa mchezaji mwingine tegemeo wa eneo la kti kati ya Uwanja Andre-Frank Zambo Anguissa aliyeonyeshwa kadi nyekundu.

Mkongwe Olivier Giroud ataendelea kuwa sehemu ya uzoefu katika safu ya ushambuliaji ya AC Milan akisaidiana na Rafael Leao Brahim Diaz na akina Sandro Tonali katika eneo la kiungo ili kukamilisha safari waliyoianza msimu huu.

Kama kawaida yetu SportPesa tayari tumewawekea mechi hizi katika tovuti yetu, na unaweza kucheza kwa kutembelea sportpesa.co.tz au kwa kupiga *150*87#

Share this: