MICHEZO YA KUBASHIRI KAMA MOJA YA BURUDANI
Moja kati ya tasnia za Burudani zinazogusa maisha ya watanzania moja kwa moja ni pamoja na michezo ya kubashiri ambayo ipo kwenye kundi la michezo ya kubahatisha.
Katika tasnia hii SportPesa ni mmoja wa wadau wakuu akiwa kama mwekezaji wa michezo hii, akiwa kama jukwaa la kimtandao kwa maana ya mfumo wa biashara wa michezo ya ubashiri kwa kutumia tovuti na huduma za USSD kwa kutumia simu janja, Kompyuta mpakato, Kompyuta ya mezani na Kishikwambi.
VIGEZO NA MASHARTI
Katika eneo hili SportPesa imekuwa ikiwakumbusha wachezaji wake kucheza kwa ustaarabu kupitia kila matangazo inayoyatoa, iwe ya kimtandao, ama ya Radio na TV ili kuhakikisha huduma inaenda kwa watu sahihi.
Na pia SportPesa imekuwa husimamia umri sahihi unaoruhusiwa kisheria kushiriki michezo hii ambapo wachezaji wake wote ni lazima wawe na umri kuanzia miaka 18 kama vigezo na masharti.
FAIDA KWA BAADHI YA WASHINDI.
Kwa upande chanya, michezo ya kubahatisha ni chanzo cha ziada cha mapato kwa wale ambao wamefanikiwa kushinda katika madau yao.
Baadhi ya watu wameripotiwa kujishindia kiasi kikubwa cha pesa kupitia michezo ya kubahatisha, jambo ambalo linaweza kuboresha hali yao ya kifedha na kuwawezesha kufikia malengo yao, kama vile kulipa madeni, kununua nyumba, au kuanzisha biashara.
Michezo ya kubahatisha imetoa fursa za ajira kwa watu ambao wanaofanya kazi katika tasnia, mfano madereva, wanasheria, wahasibu, wafanya usafi, wataalamu wa kuchakata timu, wachambuzi wa mechi na watoa huduma kwa kwa wateja.
Kwa uchache faida itokanayo na michezo ya ubashiri ambayo SportPesa anachangia katika maendeleo ya uchumi ni pamoja na kodi ya mapato, ambayo inatokana na washindi wanaopatikana.
UDHAMINI.
Faida nyingine ni pamoja na udhamini ambao SportPesa imekuwa inatoa tangu kuanza kwa shughuli za kibiashara nchini Tanzania. Ikumbukwe SportPesa inatoa udhamini mkubwa kwa sasa kupitia Yanga wa Bilioni 12 na ushehe kwa miaka 3.
Kabla ya mkataba huu ambao SportPesa na Yanga, ambao umesainiwa mwaka jana, SportPesa ilikuwa inadhamini timu ya Simba kama mdhamini mkuu kwa kipindi cha miaka mitano ambapo sote tunajua hatua za mafanikio kwa timu hiyo ni kwa kiasi gani zilichochewa na zawadi nono, pamoja na bonasi kwa kila taji na hatua za kimashindano zilizoainishwa kwenye mikataba iliyokwisha.
Kwa sasa SportPesa inaidhamini timu ya Namungo ya Lindi pamoja na timu ya Singida Big Stars ya Singida.
FURSA KWA WASHINDI.
Ili kuwarudishia wachezaji ushindi wao, SportPesa walianzisha Jackpot bonus, Multibet bonus, bet spinner, ili kumuongezea mteja wigo wa zawadi ambazo zinawapatia watanzania wengi nafuu, hata kama bashiri yake haikushinda.
Bonasi hizi zimekuwa na mwitikio mzuri kumzawadia mchezaji endapo hatabashiri kwa usahihi mechi zote.
Mfano mzuri ni pale washindi kadhaa ambao wamewahi kucheza kiwango cha chini kabisa cha pesa Sh 100, 200 na 300 walipoweza kuibuka na zaidi ya milioni 25 kama zawadi kwenye mechi za multi bet.

Tayari SportPesa imeshapata zaidi ya washindi 8 wa Jackpot kwa viwango vya zaidi ya milioni 200, 250, 300,400 na pia mshindi mmoja wa bilioni 1, ambaye katika mazingira ya kawaida asingeweza kupata kiasi hicho cha fedha hata ngefanya kazi miaka mingi.
Kwa ufupi tu, michezo ya kubahatisha ni fursa nzuri kwa mteja ambaye anajali miongozo inayotolewa na pia anayeishi kwa wajibu, kama ambavyo SportPesa imekuwa inasisitiza, kupitia matangazo mbali mbali, kucheza kistaarabu na kuzingatia umri wa kuanza kucheza na kuhakikisha kwamba unaweza kujizuia endapo utapungukiwa pesa.
