FC 15 de Agosto vs Simba SC CAF Champions League yasogezwa mbele kupigwa 21/10/2026 Uwanja wa Uhuru

15 de Agosto vs Simba SCUhuruUhuru
  • Mechi ya hatua ya pili FC 15 de Agosto vs Simba SC CAF Champions League itapigwa 21/10/2026 Uwanja wa Uhuru saa 9:00 alasiri.
  • Simba SC wametoa taarifa rasmi kuhusu mchezo huo kusogezwa mbele kutoka 20/10/2026 Jumanne hadi Jumatano, 21/10/2026.
  • Mechi hiyo kali yakusaka mshindi wa kutinga hatua ya makundi haitakuwa na mashabiki kwa kuwa wenyeji FC 15 de Agosto wamegoma.
Libase Gueye
Libase Gueye nyota wa kikosi cha Simba SC

Mchezo wa hatua ya pili FC 15 de Agosto vs Simba SC CAF umesogezwa mbele kwa wababe hawa kukutana kusaka ushindi.Awali pambano hili kali lilitarajiwa kuchezwa 20/10/2026 siku ya Jumanne, Uwanja wa Uhuru.Rasmi itakuwa ni Oktoba 21, 2026 saa 9:00. Mabadiliko ni kutoka kesho Jumanne kwenda Jumatano.Sababu kubwa ni tatizo la usafiri kwa wapinzani 15 de Agosto kutoka Guinea ya Ikweta na haitakuwa na mashabiki.

SOMA HII PIA:15 de Agosto vs Simba SC: Latest News | H2H | Prediction | SportPesa Blog

Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa

Una nafasi yakushinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa. Rubani makini anapaa angani akiwa na uhakika. Mwanzo wa wiki muda sahihi kuvuna mamilioni. Bofya hapa chini ushinde sasa hivi.

image

FC 15 de Agosto vs Simba SC CAF taarifa za mechi

KipengeleMaelezo
MashindanoCAF Champions League
MchezoFC 15 de Agosto vs Simba SC
UwanjaUhuru,Dar
Tarehe21/10/2026
Timu mwenyejiFC 15 de Agosto

Sababu za mchezo kupelekwa mbele

Kwa mujibu wa Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema wenyeji wa mchezo waliomba iwe hivyo.Hii ilitokana na kukosa usafiri ambao ugewawahisha kuwasili Dar.Jambo hilo liliwasukuma kuandika barua CAF kuomba kubadilishiwa tarehe.

“Wapinzani wetu FC 15 de Agosto waliandika barua CAF kuomba mechi ipelekwe mbele.Sababu kubwa walikosa ndege ambayo ingewafanya wawahi kuja Dar.Hivyo wamekubaliwa na wanatarajiwa kuwasili Oktoba 19 usiku na watapata muda wa mazoezi siku ya Oktoba 20.

Hakuna mashabiki Uwanja wa Uhuru

“Msimamo wao mechi ya tarehe 21 haitakuwa na mashabiki, sisi Simba SC tumejaribu kuwashawishi mashabiki waingie uwanjani na tungewasaidia kutangaza mchezo lakini wamekataa katakata.Mchezo ambao mashabiki wetu mtaingia utapigwa Jumapili Oktoba 25, 2026 saa 10:00 jioni.

“Baada ya kutupa taarifa ya kukataa mashabiki baadae tukapata taarifa kwamba wanafanya mpango wa chinichini kuwe na mashabiki.Sasa msimamo wetu kama Simba SC ni hatutakwenda uwanjani, sisi tutasubiri mechi ya tarehe 25. Sisi tulitumia njia rasmi kuwasiliana nao wakakataa na wakatoa taarifa na CAF, sasa wanapita nyuma ya pazia kutafuta mifumo ya kuuza tiketi na hatujui wanashirikiana na nani. Wakiuza tiketi sisi mashabiki hatutanunua,” amesema Ahmed Ally.

SOMA HII PIA:Simba SC CAF Champions League: Fixtures, Results, Squad & Standings

Hitimisho

FC 15 de Agosto vs Simba SC CAF ni pambano kali linalosubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki.Licha ya kwamba hawatapata fursa kuingia uwanjani watafungiwa big screen, Uwanja wa Mwembeyanga.Mchezo wa marudio unatarajiwa kuwa na mashabiki kwa kuwa mnyama atakuwa nyumbani, Oktoba 25,2026, Uwanja wa Uhuru.

Share this: