Simba SC vs Yanga SC Oktoba10,2026ShalulileShalulile

Yanga SC vs Simba SC
Clatous Chota Chama
  • Simba SC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itapambana na Yanga SC iliyo nafasi ya kwanza, zote zikiwa na pointi 18 baada ya mechi 6.
  • Kwenye mechi 12 zilizopita, Yanga SC imepata ushindi kwenye mechi 5, Simba SC imepata ushindi mchezo mmoja na sare zikiwa 6
  • Matokeo ya mchezo uliopita kwenye ligi Simba SC 2-2 Yanga SC waligawana pointi mojamoja wababe hawa

Dabi ya Kariakoo joto linazidi kupanda asilimia 98 sasa.  Simba SC vs Yanga SC watakutana katika pambano la kukata na shoka la Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) ni Oktoba 10, 2026. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na mvuto mkubwa na kuamsha hisia za mashabiki wa soka nchini Tanzania.

Pambano hili la jadi litafanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Saa 1:00 usiku kazi ya msako wa pointi tatu muhimu itaanza. Yanga SC kwenye msimamo ni nafasi ya kwanza inafuatiwa na Simba SC iliyo nafasi ya pili zote zina pointi 18 baada ya mechi 6.

SOMA HII PIA:Simba SC vs Yanga SC 10/10/2026: Hawa hapa wachezaji hatari wa kuchungwa Jumamosi kwenye mechi ya NBC Premier League 2026/27

Shinda mamilioni na SportPesa

Una nafasi kubwa kushinda mamilioni ukibashiri mchezo wa Simba SC vs Yanga SC kupitia SportPesa. Rahisi mno, suka mkeka wako na ubashiri kwa uwajibikaji. Bofya link hapa uchague option uipendayo ukombe mihela.

Simba SC vs Yanga SC
Simba SC vs Yanga SC

Simba SC vs Yanga SC habari za timu

Wenyeji Simba SC wamebainisha kwamba wachezaji wapo tayari kwa mchezo huo mkali. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano amesema kuwa kila kitu kinakwenda vizuri. Amewatoa hofu mashabiki kuhusu kiungo Libase Gueye kwa kubainisha kuwa yupo kamili.

“Tetesi kuhusu kuumwa, sijui kutofanya mazoezi kwa mchezaji wetu Libase Gueye zisipewe nafasi. Mchezaji wetu yupo kamili anaaendelea na mazoezi. Maandalizi yanaendelea kuelekea mchezo wetu mgumu dhidi ya Yanga SC,”.

Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari, Yanga SC amesema wanatambua kazi kubwa ipo Oktoba 10, 2026. Ameongeza kwa kubainisha kuwa kila mchezaji yupo tayari. Kuhusu kukosekana kwa Aziz Ki ameweka wazi kwamba wapo wengine katika nafasi hiyo.

“Kuna mashabiki wanahofu kuhusu kukosekana kwa Aziz Ki mchezo wetu dhidi ya Simba SC. Hilo lisiwape tabu kwa kuwa tunajua mchezaji ana adhabu ya kadi nyekundu. Katika nafasi yake tuna Albert Kangwanda anaubonda bila tabu,”.

H2H Simba SC vs Yanga SC

Katika mechi 12 zilizopita walipokutana wababe hawa wawili Yanga SC ameibonda Simba SC mechi 5. Mnyama alipata ushindi mchezo mmoja huku wakitoshana nguvu kwenye mechi 6. Matokeo ya mchezo wa mwisho walipokutana kwenye ligi ilikuwa Simba SC 2-2 Yanga SC, Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo.

Tarehe Mashindano Nyumbani Matokeo Ugenini
03/05/2026 Ligi Kuu Bara Simba SC 2 – 2 Yanga SC
01/03/2026 Ligi Kuu Bara Yanga SC 0 – 0 Simba SC
25/06/2025 Ligi Kuu Bara Yanga SC 2 – 0 Simba SC
19/10/2024 Ligi Kuu Bara Simba SC 0 – 1 Yanga SC
20/04/2024 Ligi Kuu Bara Yanga SC 2 – 1 Simba SC
05/11/2023 Ligi Kuu Bara Simba SC 1 – 5 Yanga SC
23/10/2022 Ligi Kuu Bara Yanga SC 1 – 1 Simba SC
30/04/2022 Ligi Kuu Bara Yanga SC 0 – 0 Simba SC
11/12/2021 Ligi Kuu Bara Simba SC

0 – 0 Yanga SC
03/07/2021 Ligi Kuu Bara Simba SC 0 – 1 Yanga SC
07/11/2020 Ligi Kuu Bara Yanga SC 1 – 1 Simba SC
16/04/2023 Ligi Kuu Bara Simba SC 2 – 0 Yanga SC

Mitambo ya mabao Simba SC vs Yanga SC

Clatous Chama wa Simba SC ni mtambo wa mabao. Huyu anaongoza orodha ya wafungaji katika kikosi hicho kwenye mechi za ligi.Chama amefunga mabao 4 akicheza mechi 5 nakukomba dakika 440.

Maxi Nzengeli huyu ni mtambo wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga SC. Amehusika kwenye mabao 4 kati ya 18 yaliyofungwa na timu hiyo inayoongoza ligi. Amefunga mabao 3 na kutoa asisti 1 akicheza mechi 6 nakukomba dakika 521.

SOMA HII PIA:Simba SC vs Yanga SC: Vikosi vinavyoweza kuanza Kariakoo Dabi 2026 | Prediction | Odds

Utabiri na uchambuzi wa wahariri

Yanga SC wamekuwa na rekodi nzuri dhidi ya Simba SC kwenye mechi za hivi karibuni. Kwa mujibu wa takwimu ya mechi za hivi karibuni matokeo yatakuwa ni sare kwa utabiri. Simba SC 1-1 Yanga SC. Haya ni maoni ya mhariri na sio matokeo kamili.

Hitimisho

Simba SC vs Yanga SC ni timu pekee ambazo hazijapoteza pambano ndani ya uwanja. Kwa upande wa ulinzi zote zimeruhusu kufungwa mabao 2 pekee na ushindi kwenye mechi zote 6 zilizopita walipata. Oktoba 10, 2026 inatarajiwa kuwa na msisimko mkubwa kwa wababe hawa kutoka mitaa ya Kariakoo.

Share this: