- Zimesalia siku 74 tu, kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kombe la Dunia 2026, huku kambi ya timu ya Taifa ya Argentina imepata mshtuko!
- Hii ni baada ya kutoka kwa taarifa kuwa Nyota na nahodha wao, Lionel Messi bado hajafanya maamuzi ikiwa atacheza, au hatacheza mashindano hayo.
- Ikumbukwe Argentina ndio mabingwa watetezi wa mashindano hao, ubingwa waliotwaa mwaka 2022 nchini Qatar wakiongozwa na Messi.
Zikiwa zimebaki siku 74 tu, kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kombe la Dunia 2026 kambi ya timu ya Taifa ya Argentina imepata mshtuko! Hii ni baada ya kutoka kwa taarifa kuwa Nyota na nahodha wao, Lionel Messi bado hajafanya maamuzi ikiwa atacheza, au hatacheza mashindano hayo. Ikumbukwe Argentina ndio mabingwa watetezi wa mashindano hao, ubingwa waliotwaa mwaka 2022 nchini Qatar wakiongozwa na Messi.
SOMA HII PIA: Sheria mpya za mechi Kombe la Dunia 2026 zashtua! Nini kimebadilishwa?
Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Taarifa ya kushtua ya kocha wa Argentina kumhusu Lionel Messi

Huku kikosi cha Argentina kikiendelea na ratiba ya mechi zilizo kwenye Kalenda ya FIFA, kocha mkuu wa Argentina, Lionel Scaloni amefichua kuwa nahodha wake huyo bado hajafanya maamuzi ya mwisho. Hivyo swali linabaki kuwa je, Messi atakwenda kwenye Kombe la Dunia au, ataamua inatosha. Hii ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Ikumbukwe mashindano makubwa ya Kombe la Dunia 2026 yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi tarehe 12 Juni, 2026. Bingwa Mtetezi, Argentina wanatarajiwa kucheza mechi yao ya kwanza ya Kundi J dhidi ya Algeria siku tano baadaye.
Kocha, Scaloni amefichu kuwa ana hamu ya kumwona Messi akiwa sehemu ya kikosi kitakachosafiri kwenda Marekani, Canada na Mexico baadaye mwaka huu. Lakini akathibitisha kuwa, bado hajapata uamuzi wa mwisho kutoka kwa nahodha huyo kuhusu ushiriki wake.
“Kama Messi atakuwa sehemu yetu, hilo ni swali kwake yeye. Kuhusu mimi, tayari mnajua msimamo wangu. Nitafanya kila niwezalo kuhakikisha yupo. Ninaamini kwa ajili ya mchezo wa soka, anapaswa kuwepo.
“Lakini sio mimi ninayeamua. Inategemea na yeye mwenyewe, hali yake ya akili na hali yake ya kimwili. Ni vigumu kwa sababu si Waargentina tu, wanaotaka kumuona, bali kila mtu anataka kumuona. Nataka awepo, ni juu yake kuamua, anastahili haki ya kufanya uamuzi huo kwa utulivu. Hatuna haraka, tunajua uamuzi wowote atakaofanya utakuwa bora kwa timu na kwake, tunatumaini atakuwepo.”
Kuhusu mechi za kimataifa ambazo timu hiyo inajiandaa nazo, kocha Scaloni amesema: “Messi atacheza mechi zote mbili, lakini tutaona kama ataanza kikosini dhidi ya Zambia na Mauritania. Kuwa na mechi mbili zaidi nyumbani ni fursa nzuri kwa Wargentina kumuona uwanjani, na kufurahia kile tunachokifurahia anapokuwepo.”
SOMA HII ZAIDI: Inter Miami CF – Muhtasari, Kikosi cha Wachezaji, Ratiba, Matokeo, Takwimu, Tuzo na Habari za Hivi Punde
Argentina yapangwa Kundi J

Katika Kampeni yake ya kutetea ubingwa huo wa Kombe la Dunia, kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina kimepangwa Kundi J. Pamoja na Argeria ambao watafungua nao mashindano, Argentina pia watavaana na timu za Austria na Jordan.
Kombe la Dunia la 6 kwa Lionel Messi

Iwapo Messi atafikia maamuzi ya kucheza mashindano yam waka huu, itakuwa mara ya 6 kwake kujumuishwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina kinachoshiriki Kombe la Dunia. Messi, ambaye amezaliwa Juni 24, mwaka 1987 anatarajia kufikisha umri wa miaka atatimiza miaka 39 wakati wa mashindano yam waka huu. Mpaka sasa amefanikiwa kuweka rekodi ya kucheza mechi 26 katika mashindano hayo, huku akifunga mabao 13 yakiwa ni mabao mengi kuliko mchezaji mwingine yeyote wa Argentina.
SOMA HII PIA: Lamine Yamal akabidhiwa jezi namba 10 ya Messi Barcelona, asaini Mkataba mpya mpaka 2031
Hitimisho

Je, Lionel Messi atakwenda Marekani kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026? Bado linabaki kuwa swali muhimu ambalo wadau wengi wa soka wanasubiri kujua majibu yake. Akiwa anakaribia kutimiza umri wa miaka 39, hili linatabimashindano haya ya Kombe la Dunia yanatarajiwa kuwa ya mwisho kwa Messi, kwani mashindano ya mwaka 2030 atakuwa na miaka 43. Kutokana na hilo mashabiki wengi wa soka wanatamani kumuona Messi na kumuaga rasmi, muda utatoa majibu sahihi.

