- Baada ya ligi mbalimbali duniani kusimama kwa muda kupisha ratiba ya mashindano ya FIFA Series, ambayo ni mashindano maalum yanayoratibiwa na Shirikisho la soka Duniani.
- Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ipo nchini Rwanda ambapo watakuwa na michezo mitatu.
- Kesho Alhamisi kutakuwa na mchezo wa Tanzania vs Liechtenstein.
- Ikumbukwe FIFA Series ni mashindano maalum, yaliyo kwenye kalenda ya FIFA ambayo yanalenga kuhakikisha timu zinajiandaa na mashindano mbalimbali makubwa.
Ligi mbalimbali duniani zimesimama kwa muda kupisha ratiba ya mashindano ya FIFA Series, ambayo ni mashindano maalum yanayoratibiwa na Shirikisho la soka Duniani. Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ipo nchini Rwanda ambapo watakuwa na michezo mitatu. Kesho Alhamisi kutakuwa na mchezo wa Tanzania vs Liechtenstein. Ikumbukwe FIFA Series ni mashindano maalum, yaliyo kwenye kalenda ya FIFA ambayo yanalenga kuhakikisha timu zinajiandaa na mashindano mbalimbali makubwa. Makala hii inauchambua kwa ufupi mchezo huo, kama ifuatavyo;
SOMA HII PIA: AFCON 2025: Matokeo na Ratiba, hizi hapa timu zilizofuzu hatua ya mtoano (16 bora)
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Kuhusu mchezo wa Tanzania vs Liechtenstein
Mara baada ya kuonyesha kiwango bora katika mashindano ya AFCON 2025, kikosi cha Miguel Gamondi kinatarajia kushuka tena Uwanjani kesho Alhamisi. Tanzania itavaana na Liechtenstein katika mchezo muhimu ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Kigali Pele. Huu ni mmoja kati ya michezo mitatu muhimu ya kundi B ambalo Tanzania wapo katika mashindano hayo ya FIFA Series.
Tanzania vs Liechtenstein h2h

Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuvaana na taifa hilo la Ulaya. Hivyo hii ni nafasi ya kila upande kuandika historia mpya katika rekodi ya soka la kimataifa. Mchezo huu unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Kigali Pele Stadium uliopo Kigali, Rwanda.
Fomu ya Tanzania katika mechi 5 zilizopita
Morocco 1-0 Tanzania
Tanzania 1-1 Tunisia
Uganda 1-1 Tanzania
Nigeria 2-1 Tanzania
Kuwait 4-3 Tanzania
Habari za timu

Tanzania imesafiri na kikosi cha mastaa 23 kwa ajili ya mashindano hayo, mastaa hao walitajwa na Kocha mkuu wa Taifa Stars, Miguel Gamondi. Ikumbukwe Tanzania inaingia katika mashindano haya ikitoka kufanya vizuri katika mashindano ya AFCON 2025, ambapo iliandika rekodi ya kucheza hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hili.
Safari ya Tanzania katika mashindano hayo ilianza vibaya kwa kupoteza kwa mabao 2-1 mbele ya Nigeria, katika mchezo wa kwanza wa mashindano hayo. Lakini vijana wa kocha Miguel Gamondi wakafanya kweli katika michezo miwili iliyosalia, ambapo walifanikiwa kuvuna pointi 2 dhidi ya Uganda na Tunisia. Hii iliwafanya kuandika rekodi ya kufuzu hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo.
Tanzania haijawa katika fomu nzuri katika ujumla wa takwimu. Sare yao dhidi ya Tunisia kwenye AFCON na baadae kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Morocco kiliwafanya waandikishe mechi 13 bila ushindi kwenye mashindano ya AFCON. wamefungwa mara 8 na kutoa sare 5.
SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025 hatua ya 16 bora ratiba/ Morocco vs Tanzania kuwashangaza wengi, msimamo
Taarifa za majeraha

Tanzania inayaendea mashindano haya ya FIFA Series wakiwa na changamoto kubwa ya majeraha ya baadhi ya Nyota wao muhimu wawili wa ulinzi. Tanzania itawakosa kiungo, Yusuph Kagoma na mlinzi wa Kati, Ibrahim Baka ambao wote ni majeruhi. Nyota mwingine ambaye ameshindwa kujiunga na kambi ni Simon Msuva kutokana na changamoto ya usafiri. Kutokana baadhi ya Nyota wameitwa kujaza nafasi zao, akiwemo kiungo mshambuliaji wa Simba. Moris Abraham.
SOMA HII PIA: Tanzania vs Nigeria mchezo wa kwanza AFCON 2025 Morocco/ Orodha ya wachezaji, kazi imeanza
Hitimisho

Tanzania vs Liechtenstein unatarajiwa kuwa mchezo mgumu kwa pande zote mbili hasa kutokana na ukweli kwamba hakuna upande ambao unawajua wapinzani zaidi. Ni mara ya kwanza timu hizi kuvaana, ninafasi kwa kila timu kuandika historia. Pamoja na historia Stars itatumia mchezo huo kujiandaa na mashindano makubwa ya AFCON 2027 yatakayofanyika kwa maandali ya Pamoja ya Tanzania, Kenya na Uganda. Dakika 90 ndizo zitatupa majibu, ikiwa na Stars au Liechtenstein.

