- Moto utawaka leo Alhamisi katika Uwanja wa Gillette huko Massachusetts, Marekani.
- Ni katika mchezo mkubwa wa kirafiki wa kujiandaa na mashindano ya fainali za FIFA World Cup 2026 kati ya Brazil vs France.
- Majina makubwa kama Mbappe, Vinicius, Raphinha, Dembele yanatarajia kukiwasha. Makala hii inachambua kwa ufupi.
Kinawaka leo Alhamisi katika Uwanja wa Gillette huko Massachusetts, Marekani. Ni katika mchezo mkubwa wa kirafiki wa kujiandaa na mashindano ya fainali za FIFA World Cup 2026. Brazil vs France mechi ambayo inatoa taswira ya mwendelezo wa maandalizi ya timu hizo, kuelekea mashindano hayo.
SOMA HII PIA: Yamal na Dembele watikisa listi mastaa 30 Tuzo ya Ballon d’Or 2025
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Brazil vs France h2h

Timu hizi zilikutana kwa mara ya kwanza mwaka 1958, ambapo toka wakati huo zimecheza mechi 15. Mpaka sasa hakuna mbabe kati yao kwani kila timu imefanikiwa kushinda mechi 6, huku mechi 3 zikimalizika kwa matokeo ya sare. Mabao 47 yamefungwa kwenye makutano yao, ambapo Brazili wamefunga mabao 26, huku Ufaransa wakifunga mabao 21.
Vikosi vinavyoweza kuanza Brazil vs France
Brazil:

Kipa: Ederson
Walinzi: Wesley, Bremer, Marquinhos, D. Santos
Viungo: Raphinha, Casemiro, A. Santos, Vinicius Jr;
Washambuliaji: Cunha, Pedro
France
Kipa: Maignan
Walinzi: Gusto, Konate, Upamecano, T. Hernandez
Viungo: Tchouameni, Rabiot; Olise, Cherki, Mbappe
Mshambuliaji: Dembele
SOMA HII ZAIDI: Gianluca Prestianni vs Vinicius Jr, Tuhuma za ubaguzi wa rangi ‘Racism’ Mbappe, UEFA watoa msimamo mzito
Habari za timu
Katika mfululizo wa maandalizi haya, timu ya Taifa ya Brazil pia itakutana na Croatia wakati wa ziara yao fupi Marekani. Kikosi cha Didier Deschamps, kinaitarajia pia mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Colombia.
Ikumbukwe Brazil amba oni mabingwa mara 5 wa kombe la dunia walikuwa na nyakati ngumu kukata tiketi ya kushiriki mashindano hayo. Kikosi cha, Carlo Ancelotti kilimaliza nafasi ya tano katika hatua ya kufuzu kwa CONMEBOL, nyuma ya Argentina, Ecuador, Colombia na Uruguay.
Brazil wamekuwa wakisuasua kurejesha ubabe wake kimataifa, ikishinda mechi mbili tu kati ya tano zilizopita (za kirafiki na mashindano). Mwishoni mwa mwaka jana, walifungwa na Bolivia na Japan, lakini Novemba ilikuwa bora kidogo walipoifunga Senegal 2-0 na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Tunisia huko Lille. Ikumbukwe katika Kundi C la Kombe la Dunia, Brazil itavaana na Morocco, Haiti na Scotland, na kama wataongoza kundi hilo, wanaweza kukutana tena na France katika hatua za juu.
Kwa upande wa France, hawakupata shida kufuzu Kombe la Dunia, wakimaliza kileleni mwa Kundi D la UEFA kwa kupoteza pointi mbili tu. Kocha, Didier Deschamps, ambaye ni mmoja wa watu wachache kushinda Kombe la Dunia akiwa mchezaji na kocha (pamoja na Franz Beckenbauer na Mario Zagallo), ataiongoza France katika mashindano yake ya mwisho kabla ya kumpisha kocha, Zinedine Zidane. France haijapoteza mechi saba mfululizo, (ikishinda sita tangu ilipofungwa na Spain katika nusu fainali ya Nations League).
Taarifa za majeruhi
Brazil
Kocha, Carlo Ancelotti amekumbwa na majeraha ya wachezaji wa ulinzi, ambapo Gabriel Magalhães, Alisson Becker na Alex Sandro wamejiondoa kikosini. Neymar ameachwa kwa uamuzi wa kocha, huku nafasi ikipewa wachezaji wapya kama Igor Thiago na Rayan. Katika ushambuliaji, ushindani ni mkubwa kati ya Matheus Cunha, Vinícius Júnior, Raphinha na João Pedro.
France

William Saliba na Manu Kone hawapo kikosini kutokana na majeraha, huku Jules Koundé akiendelea kuuguza majeraha ya misuli ya paja. Hata hivyo, France bado ina kikosi imara, ambapo nahodha Kylian Mbappé anakaribia kuvunja rekodi ya mabao ya timu ya taifa (ana mabao 55, mawili nyuma ya Olivier Giroud mwenye 57).
SOMA HII PIA: Best Fifa Men’s 11 in 2025 – Mastaa wa PSG wateka tuzo nyingi za kikosi bora duniani mwaka huu
Hitimisho na Utabiri
Ingawa uwezo wa kocha wa Brazil, Carlo Ancelotti hawezi kubezwa lakini bado Brazil ya sasa haiogopeshi kama ilivyokuwa zamani. Kwa kuzingatia kiwango kizuri cha France na safu yao hatari ya ushambuliaji, France inatabiriwa kuibuka na ushindi katika mchezo huu. Lakini bado Brazil ina namba kubwa ya mastaa wenye uwezo binafsi ambao wanaweza kuamua matokeo.

