Yanga SC wanaanza mabadiliko leoAli Kamwe
  • NBC Premier League Mtibwa Sugar vs Yanga SC Jumamosi saa 10:00 jioni
  • Yanga SC wanaanza mabadiliko leo NBC Premier League
  • Mtibwa Sugar imecheza mchezo mmoja dhidi ya Yanga SC 2025/26 ilipoteza kwa kufungwa magoli 2-0
  • Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari Yanga SC amesema nyakati ngumu zimepita

Yanga SC wanaanza mabadiliko leo dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kuangusha pointi 4. Azam FC 0-0 Yanga SC, TRA United 0-0 Yanga SC matokeo ya mechi mbili zilizopita NBC Premier League. Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari amesema nyakati ngumu zimepita.

SOMA HII: Uchovu wa Yanga SC utawapa faida Mtibwa Sugar? Pedro Goncalves ataja changamoto

Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Je hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Aviator

Yanga SC wanaanza mabadiliko leo NBC Premier League

Yanga SC wanaanza mabadiliko leo
Zimbwe Jr nyota wa Yanga SC kwenye mchezo uliopita vs TRA United. Source: Yanga SC.

Wameamua Yanga SC wanaanza mabadiliko leo dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Wananchi wamecheza mechi mbili mfululizo bila kupata ushindi. Katika kusaka pointi sita walivuna mbili wakikosa alama 4.

Huyu hapa Ali Kamwe, anafichua mpango unaofuata

Ali Kamwe (-)
Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari Yanga SC. Source: Yanga SC.

“Msimu uliopita, katika nyakati kama hizi tulipoteza dhidi ya Azam FC pamoja na Tabora. Hata hivyo, napenda kuwataarifu wanachama na mashabiki wetu kuwa nyakati ngumu zimepita na mabadiliko hayo mtayaona kuanzia mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.

“Nimefurahishwa na namna wanachama na mashabiki wetu walivyopokea matokeo ya michezo yetu iliyopita. Aidha, tayari magari zaidi ya 50 yameondoka jijini Dar kuja Dodoma kwa lengo la kuja kuiunga mkono klabu yetu,”.

SOMA HII: Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar NBC Premier League KMC Complex | Highlights, magoli, Zimbwe Jr mchezaji bora

Aviator

Mtibwa Sugar vs Yanga SC utabiri upoje?

Kwa mujibu wa rekodi Yanga SC ana bahati yakushinda mbele ya Mtibwa Sugar iwe nyumbani ama ugenini. Kwenye mechi 7 zilizopita, wakulima wa miwa walipoteza mechi zote. Safu ya ushambuliaji ya Yanga SC ilifunga magoli 16, Mtibwa Sugar ikifunga matatu.

Jumla yalifungwa magoli 19. Hakuna sare iliyopatikana kwenye mechi za hivi karibuni. Matokeo haya yanaipa nguvu Yanga SC.Licha ya yote dakika 90 zitaamua leo nani atashinda.

H2H Mtibwa Sugar vs Yanga SC

Mtibwa Sugar
Mtibwa Sugar kikosi 2025/26. Source: Mtibwa Sugar

28/10/2025 Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar
13/05/2024 Mtibwa Sugar 1-3 Yanga SC
16/12/2023 Yanga SC 4-1 Mtibwa Sugar
31/12/2022 Mtibwa Sugar 0-1 Yanga SC
13/09/2022 Yanga SC 3-1 Mtibwa Sugar
29/06/2022 Yanga SC 1-0 Mtibwa Sugar
23/02/2022 Mtibwa Sugar 0-2 Yanga SC

SOMA HII: Yanga SC haijapoteza mechi 2025/26 NBC Premier League / Kariakoo Dabi inanukia, matokeo, rekodi

Aviator

Msimamo  wa Mtibwa Sugar vs Yanga SC

POSMPWDLPTS
1. Yanga SC15114037
9.Mtibwa Sugar FC1655521

Hitimisho

Yanga SC wanaanza mabadiliko leo dhidi ya Mtibwa Sugar. Wananchi wanabebwa na rekodi ya kuvuna pointi mbele ya wakulima wa miwa. Je wakulima watakuwa wanyonge ama watajitutumua kuwavuruga vinara?

Share this: