- FT: Mtibwa Sugar 1-1 Yanga SC NBC Premier League, 2025/26
- Pacome Zouzoua amefunga goal dakika ya 23 kipindi cha kwanza
- Ismail Mhesa amefunga goal dakika za jioni akitokea benchi, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma
- Mtibwa Sugar watibua mabadiliko Yanga SC, Machi 21, 2026
Mtibwa Sugar watibua mabadiliko Yanga SC NBC Premier League. Wananchi walibainisha wataonyesha utofauti mwisho wamegawana alama moja kwa kufungana 1-1. Huu unakuwa mchezo wa 3 kwa Yanga SC mfululizo bila kupata ushindi ndani ya ligi.
SOMA HII: Yanga SC haijapoteza mechi 2025/26 NBC Premier League / Kariakoo Dabi inanukia, matokeo, rekodi

Mtibwa Sugar watibua mabadiliko Yanga SC, Mhesa afunga dakika za jioni

Ni Mtibwa Sugar watibua mabadiliko Yanga SC NBC Premier League. Goli la uongozi lililofungwa na Pacome Zouzoua dakika ya 23 lilidumu hadi dakika ya 89. Ismail Mhesa ambaye alianzia benchi alifunga goli la usawa dakika ya 90+2.
Kabla ya mchezo, Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC alibainisha kutakuwa na mabadiliko. Licha ya kupata goli vinara walikwama kulinda ushindi huo. Mchezo wa mzunguko wa kwanza ilikuwa Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar, Uwanja wa KMC Complex, Dar.
SOMA HII: Yanga SC wanaanza mabadiliko leo NBC Premier League vs Mtibwa Sugar/ H2H, prediction

Takwimu za Mtibwa Sugar 1-1 Yanga SC, NBC Premier League
| Mtibwa Sugar | Yanga SC | |
| 6 | Mashuti | 14 |
| 3 | Lenga lango | 8 |
| 37% | Umiliki | 63% |
| 3 | Mashuti yasiyolenga lango | 6 |
| 0 | Kadi nyekundu | 0 |
| 1 | Kadi ya njano | 0 |
| 2 | Kona | 7 |
| 1 | Magoli | 1 |
Yanga SC yaangusha pointi 6

Mchezo wa leo unakuwa wa tatu mfululizo kwa mabingwa watetezi kukwama kuvuna pointi tatu. Ilikuwa Azam FC 0-0 Yanga SC, TRA United 0-0 Yanga SC na Mtibwa Sugar 1-1 Yanga SC. Pointi 6 wameangusha kwenye mechi za ugenini chini ya Kocha Mkuu, Pedro Goncalves.
Msimamo wa Mtibwa Sugar vs Yanga SC
| POS | MP | W | D | L | PTS |
| 1. Yanga SC | 16 | 11 | 5 | 0 | 38 |
| 7.Mtibwa Sugar FC | 17 | 5 | 7 | 5 | 22 |
Kikosi cha Mtibwa Sugar vs Yanga SC
Langoni ni Costantine Malimi
Wengine ni Oscar Masai, Haroun Lyawata, Datius Peter, Omari Selemani, Kassim Shaibu, George Chota, Magata Charles, Andrea Simchimba, Said Mkopi na Evance Fabian.
Wachezaji wa akiba ni Juma Nyangi, Nassoro Kiziwa, Ismail Mhesa, Erick Kyaruzi, Laurent Alfred, Said Kazi, Juma Louzio, Toba Kutisha, Omary Yahya na Riphat Mrisho.
Kikosi cha Yanga SC vs Mtibwa Sugar
Langoni
Djigui Diarra
Mabeki
Frank Assink
Bakari Nondo
Mohamed Hussen
Israel Mwenda
Viungo
Maxi Nzengeli
Mudathir Yahya
Pacome Zouzoua
Duke Abuya
Allen Okello
Mshambuliaji
Emmanuel Mwanengo
Wachezaji wa akiba

Aziz Andabwile, Buba Jammeh, Yao Kouassi, Kibwana Shomary, Lassine Kouma, Mohamed Damaro, Abutwalib Mshery, Sheikhan Ibrahim, Abdulnassir Abdallah na Abubakar Nozar.

Hitimisho
Mtibwa Sugar watibua mabadiliko Yanga SC kwa kuwazuia kuondoka na alama tatu muhimu. Pointi moja inawaondoa wakulima wa miwa kutoka nafasi ya 9 hadi nafasi 7. Vinara wanafikisha pointi 38 baada ya mechi 16.

