- Kocha Mkuu wa TRA United, Ettiene Ndayiragije amebainisha utayari wa kikosi kuwakabili wapinzani
- TRA United vs Yanga SC NBC Premier League Machi 18/2026, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
- Pedro Goncalves Kocha Mkuu wa Yanga SC amesema watakuwa na mchezo mkubwa
TRA United vs Yanga SC NBC Premier League ni mchezo unaofuata kwenye ratiba. Machi 18 2026, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Wakusanya mapato mchezo wao dhidi ya Simba SC uliahirishwa kutokana na uwanja kujaa maji. Azam FC 0-0 Yanga SC matokeo yaliyopita kwa mpinzani wake.
SOMA HII: NBC Premier League ratiba na CAF Champions League robo fainali
Je, bado hujashinda mamilioni? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune pesa sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

TRA United vs Yanga SC rekodi itavunjwa?

Kuelekea mchezo wa TRA United vs Yanga SC swali kubwa ni rekodi inayoendelezwa na wageni itavunjwa. Wananchi kwenye ligi wamecheza mechi 14 bila kupoteza. Wamekutana na vigogo wote Yanga SC 0-0 Simba SC na walitoshana nguvu na matajiri wa Dar.
Maoni ya Ettiene Ndayiragije
Kocha Mkuu wa TRA United, Ndayiragije amesema anatambua ugumu wa mchezo. Aliongeza yote yanatokana na ubora wa mpinzani.
“Tunakutana na mpinzani mgumu hilo tunalitambua. Kwa maana hiyo ugumu utakuwa mkubwa, tumefanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mchezo wetu,”.
Pedro Goncalves, Kocha Mkuu wa Yanga SC

“Tumekuwa na ratiba yenye msongamano mkubwa wa michezo ya mfululizo na ukizingatia tumetoka katika mchezo mgumu wa ligi siku chache zilizopita, sasa tunajiandaa kuikabili timu ambayo imepata muda wa kutosha wa mapumziko na maandalizi,”.
SOMA HII: Ratiba ya Yanga SC 2025/26 ni moto/ Mechi 5 NBC Premier League ugenini/ Msimamo, matokeo

Msimamo TRA United vs Yanga SC
| POS | MP | W | D | L | PTS |
| 1. Yanga SC | 14 | 11 | 3 | 0 | 36 |
| 10. TRA United | 14 | 5 | 4 | 5 | 19 |
H2H TRA United vs Yanga SC
02/04/2025 TRA United 0-3 Yanga SC
07/11/2024 Yanga SC 1-3 TRA United
01/05/2024 Yanga SC 3-0 TRA United
23/12/2023 TRA United 0-1 Yanga SC
Kikosi cha TRA United kinachotarajiwa kuanza vs Yanga SC
Jean Noel atakuwa langoni.
Wachezaji wengine ni Nasry Kombo, Valentin Nouma, Amy Mapaka, Christopher Tebandeke, Ramadhan Ramadhan, John Lazarus, Chande Chewe, Omary Yusuph, Jamalia Dulaz na Denis Nkane.
Kikosi cha Yanga SC kinachotarajiwa kuanza

Langoni
Djigui Diarra
Mabeki
Israel Mwenda, Zimbwe Jr, Nondo, Yao. Viungo ni Damaro, Abuya, Maxi, Mudathir na Okello.
Mshambuliaji
Prince Dube.
SOMA HII: Taarifa mpya Depu na Boka wa Yanga SC haifurahishi/ Orodha ya wachezaji majeruhi

Hitimisho
TRA United vs Yanga SC NBC Premier ni mchezo mkali unaosubiriwa kwa shauku. Nani ataibuka mshindi Uwanja wa Sheikh Amri Abeid? Dakika 90 zitaamua yote.

