- Kikosi cha Mnyama leo kinashuka tena uwanjani kwa ajili ya mchezo muhimu wa Kombe la Shirikisho la CRDB.
- Ni mchezo wa Simba SC vs B19 FC, unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.
- Wenyeji Simba SC wametamba kuendeleza moto wao wa kusaka ushindi.
Kikosi cha Mnyama LEO kinashuka tena uwanjani kwa ajili ya mchezo muhimu wa Kombe la Shirikisho la CRDB. Ni katika mchezo wa Simba SC vs B19 FC unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo. Wenyeji Simba SC wametamba kuendeleza moto wao wa kusaka ushindi.
SOMA HII PIA: Ratiba ya Simba SC 2025/26 Machi dakika 450 za kazi/ Msimamo, matokeo
Je, Bado hujashinda mamilioni ya SportPesa?
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Kuhusu mchezo wa Simba SC vs B19 FC
Huu ni mchezo wa hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho la CRDB ambao unatarajiwa kupigwa majira ya saa 1:15 usiku. Ushindi kwa Simba SC katika mchezo huu, inamaanisha Mnyama atakwenda moja kwa moja hatua ya 16 bora. Lakini hautarajiwi kuwa mchezo rahisi kwa kuwa, Simba SC wamewahi kushangazwa na kuondoshwa katika hatua hizi.
Simba inauendea mchezo huu ikiwa na ratiba ya mechi 5 ndani ya mwezi machi ambapo mechi 2 ni za nyumbani na mechi 3 ugenini. Ikumbukwe mchezo uliopita Simba walivaana na Yanga SC ambapo mchezo uliisha kwa Suluhu.
Ratiba ya Simba mwezi Machi

Kwenye ratiba ya Simba SC mwezi Machi Simba SC tayari imeshavaana na Yanga SC na leo wanavaana na B19 FC. Baada ya hapo wanatarajia kuvaana na Singida Black Stars, kama mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Hii ni kutokana na uwekezaji mkubwa wat imu zote 2.
SOMA HII ZAIDI: Yanga SC vs Simba SC taarifa mpya kutoka Zanzibar, hali ya vikosi, Goncalves na Steve Barker
Kwa ufupi hii hapa ratiba ya Simba SC ndani ya mwezi Machi

Machi 7 2026, Simba SC vs B19 FC, CRDB Federation Cup.
Machi 11, 2026 Singida Black Stars vs Simba SC, NBC Premier League
Machi 14,2026, TRA United vs Simba SC, NBC
Machi 19,2026, Pamba Jiji FC vs Simba SC, NBC
Machi 22,2026, Simba SC vs TRA United, NBC
Msimamo wa ligi unasemaje?

Mpaka sasa simamo wa NBC Premier League unaonyesha Wananchi, Yanga SC wakiwa vinara na pointi zao 29 baada ya kucheza michezo 11. JKT Tanzania wanakamatia nafasi ya pili na alama zao 28 walizokusanya katika mechi 17. Mnyama Simba SC wao wanakamatia nafasi ya 3 na pointi zao 24 walizokusanya katika michezo 11.
SOMA HII PIA: Yanga SC vs Simba SC NBC Premier League: Nassoro Mwinchui mwamuzi wa kati, utabiri
Haya hapa matokeo ya mechi 5 zilizopita Simba SC
Februari 11,2026 KMC FC 0-2 Simba SC NBC
Februari 14, 2026 Simba SC 1-0 Stade Malien CAF
Februari 22,2026 Tanzania Prisons 0-2 Simba SC NBC
Februari 25,2026 Dodoma Jiji FC 0-0 Simba SC NBC
Machi Mosi 2026 Yanga SC 0-0 Simba SC NBC
Hitimisho

Kuelekea mchezo huu wa Simba SC vs B19 FC, uongozi wa kikosi cha Simba umetamba kuwa kikosi chao kinazidi kuimarika. Hii ni baada ya kuonyesha upinzani mkubwa, wakitawala mchezo wao dhidi ya Yanga SC. Akizungumzia ubora wa kikosi chao, Meneja wa Habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed amesema: “Kikosi kinazidi kuimarika, wachezaji wanajituma kwenye mechi zetu. Naomba nitoe rai kwa mashabiki kuendeleza mshikamano huu katika mechi zijazo. Kwa namna tunavyocheza tunazidi kuwa imara zaidi.”

