- Petro de Luanda vs Simba SC mchezo ujao hatua ya makundi ugenini
- Matokeo ya Simba SC CAF Champions League 2025/26 hakuna ushindi
- Barker kwenye mtihani mzito kimataifa nyumbani na ugenini
Matokeo ya Simba SC CAF Champions Leagues mechi 4 hatua ya makundi hakuna ushindi. Safu ya ushambuliaji imefunga magoli 3, ukuta umeruhusu magoli 6. Kutokana na mwendo huo nafasi yakutinga hatua ya robo fainali ni finyu kwa mnyama labda maajabu ya mpira yaamue. Ni timu mbili zinazomaliza nafasi ya juu husonga mbele kwenye mashindano.
SOMA HII: Simba SC 0-1 Petro de Luanda CAF Champions League 2025/26/ Highlights, stats, match report
Unasubiri nini? Vuna mamilioni sasa hivi
Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini, muda ni wako na nafasi ya ushindi inakusubiri.

Haya hapa matokeo ya Simba SC CAF Champions League

| 23/11/2025 | Simba SC | 0 | 1 | Petro de Luanda |
| 30/11/2025 | Stade de Malien | 2 | 1 | Simba SC |
| 24/01/2026 | Es Tunis | 1 | 0 | Simba SC |
| 01/02/2026 | Simba SC | 2 | 2 | Esperance de Tunis |
Msimamo wa kundi D
| MP | W | D | L | PTS | |
| 1. Stade Malien | 4 | 2 | 2 | 0 | 8 |
| 2. Esperance de Tunis | 4 | 1 | 3 | 0 | 6 |
| 3. Petro de Luanda | 4 | 1 | 2 | 1 | 5 |
| 4.Simba SC | 4 | 0 | 1 | 3 | 1 |
SOMA HII: Mechi za Simba SC 2025/26 CAF Champions League, NBC Premier League ni moto| Matokeo na wafungaji

Mechi zijazo kwa Simba SC CAF Champions League

Chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker mnyama ana mechi mbili mkononi. Kocha huyo ambaye ni mrithi wa mikoba ya Dimitar Pantev mchezo mmoja atakiongoza kikosi ugenini na mmoja Uwanja wa Mkapa. Katika mechi mbili hatua ya makundi nyumbani, mnyama alipoteza mchezo mmoja na kulazimishwa sare moja.
| 7/2/2026 | Petro de Luanda | vs | Simba SC |
| 13/02/2026 | Simba SC | vs | Stade de Malien |
Hitimisho
Matokeo ya Simba SC CAF Champions League yanaifanya timu hiyo kuburuza mkia kwenye kundi. Baada ya mechi nne ni pointi moja pekee imevuna. Mkononi kuna mechi mbili kwa mnyama, ugenini moja na nyumbani moja.

