- CAF Champions League hatua ya makundi kwa kundi D Simba SC rekodi yake inashutua
- Simba SC vs Esperance Tunis CAF Champions League kisasi kitalipwa Uwanja wa Mkapa?
- Matumaini ya mnyama mikononi mwa Esperance, rekodi ya kuanza safari kutinga hatua ya robo fainali kutafutwa.
Baada yakupoteza mechi tatu mfululizo swali kubwa ni Simba SC vs Esperance Tunis CAF Champions League kisasi kitalipwa? Majibu yatapatikana kesho Februari Mosi 2026, Uwanja wa Mkapa saa 10:00 jioni. Ikumbukwe kwamba mchezo uliopita hatua ya makundi mnyama alipoteza kwa goli 1-0 na mfungaji ni Jack Diarra dakika ya 21.
SOMA HII: Mechi za Simba SC 2025/26 CAF Champions League, NBC Premier League ni moto| Matokeo na wafungaji
Unasubiri nini? Vuna mamilioni sasa hivi
Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini.

Simba SC vs Esperance Tunis CAF Champions League kisasi kitalipwa?

Wababe wawili kutoka kundi D wanatarajiwa kukutana uwanjani, Simba SC vs Esperance Tunis CAF Champions League. Mchezo wa ugenini Simba SC alipoteza ataingia uwanjani akiwa amejeruhiwa. Wakati akiwa na hasira anakutana na mpinzani anayejiamini baada ya kupata ushindi nyumbani.
Vita ni kali kwa wawili hawa kutokana na mwenyeji kutopata matokeo katika mechi tatu mfululizo hatua ya makundi. Nafasi kubwa ya ushindi anapewa mnyama lakini wageni nao sio wakubeza kutokana na kiwango walichonacho. Kisasi cha kupoteza ugenini kitalipwa kwa Mkapa? Tusubiri majibu baada ya mchezo.
Msimamo wa kundi D
| MP | W | D | L | PTS | |
| 1. Stade Malien | 3 | 2 | 1 | 0 | 7 |
| 2. Esperance de Tunis | 3 | 1 | 2 | 0 | 5 |
| 3. Petro de Luanda | 3 | 1 | 1 | 1 | 4 |
| 4.Simba SC | 3 | 0 | 0 | 3 | 0 |
SOMA HII: Simba SC ina mgogoro mzito kwa sasa? Ukweli huu hapa/ Mo na Mangungu sakata lipo hivi

H2H
Januari 24 2026
Esperance de Tunis 1-0 Simba SC
Februari Mosi 2026
Simba SC vs Esperance de Tunis
Takwimu za mchezo uliopita Simba SC ilipokuwa ugenini
| Esperance Tunis | Simba SC | |
| 6 | Mashuti | 5 |
| 1 | Kipa okoa | 3 |
| 47% | Umiliki | 53% |
| 13 | Faulo | 23 |
| 0 | Kadi nyekundu | 0 |
| 0 | Kadi za njano | 2 |
| 4 | Kona | 1 |
| 4 | Lenga lango | 1 |
Kikosi cha Simba SC kinachotarajiwa kuanza

Djibrilla Kassali
Mabeki
Shomari Kapombe
De Reuck
Wilson Nangu
Nickson Kibabage
Viungo
Yusuph Kagoma
Gueye
Naby Camara
Clatous Chama
Kibu Dennis
Mshambuliaji
Jonathan Sowah
Wachezaji tegemeo kwa Esperance Tunis
Onuche Ogbelu huyu ni kiungo mshambuliaji
Houssem Teka huyu ni kiungo
Chiheb Jbeli huyu ni mshambuliaji
Diarra huyu ni mshambuliaji
Hitimisho
Simba SC vs Esperance Tunis CAF Champions League ni mchezo unaotarajiwa kuamsha matumaini kwa mnyama. Ikiwa atapoteza mchezo wanne, safari yake kutinga robo fainali inakwisha jumla. Lakini ili afanikishe hayo ni lazima ashinde mech izote zilizobaki. Je ataweza, hapa tutakupa kila matokeo.

