usajili wa Simba SC sio Clatous Chama tuLoemba
  • Inno Jospin Loemba Jayrutty asimamia kazi ujio wake
  • Usajili wa Simba SC dirisha dogo balaa! Gueye, Kibabage wametambulishwa
  • Orodha ya wachezaji waliosajiliwa Simba SC dirisha dogo isome hapa

Kwenye usajili wa Simba SC dirisha dogo balaa! Jumla ni nyota 7 watakuwa chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker. Lengo la timu hiyo ni kurejea kwenye makali baada ya kutokuwa kwenye mwendo mzuri hivi karibuni. Clatous Chama amezua gumzo kubwa kurejea kwake.

SOMA HII: Depu straika mpya Yanga, Gueye huyoo Simba: Tetesi usajili mpya Ligi Kuu Bara 2025/26

Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Ni zamu yako sasa, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Usajili wa Simba SC dirisha dogo balaa! Hawa hapa wapya

usajili wa Simba SC sio Clatous Chama tu
Chama Clatous kiungo mshambuliaji wa Simba SC.

Kwenye usajili wa Simba SC dirisha dogo kuna wapya wameanza kazi tayari. Jina la Chama limeibua maswali kila kona. Sababu kubwa ya Chama kuwa gumzo ni kurejea kwa mara ya tatu mara baada ya kuondoka. Kiungo huyo mshambuliaji alikuwa Singida Black Stars.

Ikumbukwe kwamba alitambulishwa Simba SC 2018 kisha akasajiliwa RS Berkane ya Morocco 2021/22. Alirejea unyamani 2022/24 kisha akajiunga na Yanga SC  2024/25. 2025/26 alisajiliwa Singida Black Stars kisha dirisha dogo akasajiliwa na Simba SC. Clatous Chama maarufu kwa jina la Mwamba wa Lusaka alitambulishwa Januari 20 2026.

Ahmed Ally Meneja wa Simba SC maoni yake

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema Chama ni silaha ya ushindi.Aliongeza kuwa hakutumia ujuzi wote alipokuwa kwa watani zao wa jadi.

“Clatous Chama ni mashine ya kazi. Hakutumia ujuzi wote alipokuwa kwa majirani zetu.Karejea kwenye timu anayoipenda atafanya makubwa kwelikweli,”.

SOMA HII: Usajili wa Chama Simba SC washtua! Mayele, Kagere, Okwi wafunguka Mazito

image

Hii hapa orodha ya waliotambulishwa Simba SC dirisha dogo

Loemba

Inno Jospin Loemba  ni ingizo jipya kutoka Colombe Sport ya Cameroon. Huyu ni raia wa DR Congo alitambulishwa Januari 28 2026. Huyu ni kiungo mshambuliaji. Mzabuni Jayrutty ametimiza ahadi ya kumleta mchezaji mkubwa.

Oura

Aliwahi kucheza Gnistan ya Finland mpaka mkataba wake ukaisha. Anaitwa Anicet Oura Raia wa Ivory Coast alitambulishwa Januari 26,2026 akiwa ni mchezaji huru huyu ni winga.

Toure

 Olivier Toure huyu ni beki kutoka Ivory Coast alitambulishwa Januari 20 2026 ametua Simba. Ni mkataba wa miaka miwili amesaini.

Kassali

Ni kipa wa Niger,MahamadouTanja Djibrilla Kassali Djibo mwenye miaka 29. Alitambulishwa Januari 20 2026. Tayari ameanza kazi unyamani.

Kibabage

Nickson Kibabage Januari 19 2026 alitambulishwa. Huyu ni beki alikuwa Singida Black Stars. Tayari ameanza kazi.

Gueye

Gueyee
Gueye ingizo jipya ndani ya Simba SC dirisha dogo. Source: Simba SC.

Mchezaji wa kwanza kutambulishwa dirisha dogo unyamani ni kiungo mshambuliaji. Anaitwa Libasse Gueye mwenye miaka 22. Januari 17 2026 alitambulishwa na alianza mazoezi siku hiyohiyo. Huyu ni raia wa Senegal.

SOMA HII: Clatous Chama kumalizana na Simba SC sababu zatajwa/ Awesu katambulishwa Police FC Kenya

image

Hitimisho

Usajili wa Simba SC dirisha dogo orodha ni kubwa wakifikisha jumla ya nyota 7. Jean Ahoua, Joshua Mutale, Mzamiru Yassin, Steve Mukwala hawa wameondoka dirisha dogo. Mnyama anapambana kurejesha makali yake kitaifa na kimataifa je itawezekana? Matokeo yatafahamika kwenye mechi zijazo.

Share this: